Picha na matukio ; mafuriko posta

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
DK. MAGUFULI ACHUKUA FOMU TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KWA KISHINDO, AIWASILISHA KWA KIKWETE KUTHIBITISHA
​
Mgombea mteule wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli na Mgombea mwenza wake, Samia Suluhu Hassan wakiondoka kwa gari la wazi kutoka Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo kwenda Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuchukua fomu ya kuwania Urais katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.​
​
Msafara wa Mgombea Mteule wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli akipita kwenye makutano ya baabara ya Morogoro na Bibi Titi Mohammed, wakati mgombea huyo akienda kuchuua fomu Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
​
​
Mwananchi akipunga mkono kufuarhia msafara wa Mgombea Mteule wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli akati ukipita kwenye makutano ya baabara ya Morogoro na Bibi Titi Mohammed, wakati mgombea huyo akienda kuchuua fomu Tume ya Taifa ya Uchaguzi.​
​
Wananchi akipunga mkono kufuarhia msafara wa Mgombea Mteule wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli wakati ukipita



​
Dk. Magufuli akisaini fomu maalum​





​
​
Maelfu ya wananchi wakimsindikiza Dk. Magufuli kurejea Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, baada ya kuchukua fomu​
​
Maelfu ya wananchi wakimsindikiza Dk. Magufuli kurejea Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, baada ya kuchukua fomu​
​
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihamasisha umati wa wananchi waliokuwa wamefurika kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, wakimsubiri kumpokea Dk. Magufuli akirejea kwenye Ofisi hiyo baada ya kuchukua fomu NEC.​
​
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, ili amkaribishe jukwaani, kuonyesha fomu zake, mgobea Mteule wa Urais wa tiketi ya CCM, Dk. John Maguli, kwenye Ofisi ya CCM Lumumba​
​
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akizungumza na umati wa wananchi kabla ya kumkaribisha Dk. Magufuli kuzungumza na wananchi baada ya kurejea na fomu zake, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba​


"Fomu ndiyo hizi", Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimsaidia Mgombea mteule wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli kuonyesha fomu za kuwania Urais kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, alizowasili nazo Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam

​




​
Rais Kikwete, Naye akajiunga kucheza muziki kidoogo wa TOT kabla ya kuwashusha jukwaani Dk. Magufuli na mgombea mwenza Samia Suluhu Hassani​
​
Dk. Magufuli akiwaaga wananchi baada ya kumalizika mkutano huo wa mapokezi yake​
​
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwaanga wananchi baada ya mapokezi hayo ya Dk. Magufuli, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba.​

​
>HALI ILIVYOKUWA KWENYE OFISI NDOGO YA MAKAO MAKUU YA CCM LUMUMBA KABLA YA DK. MAGUFULI KWENDA KUCHUKUA FOMU​
​
Kikundi cha Tanzania One Theatre, kikitumbuiza, mbele ya Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam, wakati akisubiriwa Dk. Magufuli na mgombea mweza wake kuwasili kwenye Ofisi hiyo kabla ya kwenda Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua fomu leo​
​
Mjumbe wa Kamati Kuu ambaye pia ni Mkumbe wa NEC, Uchumi na Fedha Mama Zakia Meghji akiongoza baadhi ya wana CCM kuserebuka wimbo wa TOT​
[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"] "Sikia Bwana, asikudanganye mtu CCM ndiyo Chama dume..." Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimwambia Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dinas Masaburi, wakati akisubiwa Dk. Magufuli kufika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
​
"Hapa tumejipanga hadi wapinzani waisome namba" Kinana akimwambia Naibu Katibu Mkuu wake, Rajabu Luhavi wakati akisubiwa Dk. Magufuli kufika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba ​
​
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha mgombea mwenza Samia Suhulu Hassan, baada ya kuwasili​
​
Katibu wa NEC, Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akisalimiana na mgombea Mwenza Samia Suluhu Hassa baada ya kuwasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM. Dk. Asha-Rose ni miongoni mwa waomba kuwania Urais kwa tiketi ya CCM ambaye alifanikiwa kuingia tatu bora katika mchakato wa kumpata mgombea wa CCM uliomuibua Dk. Magufuli​
​
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akifurahia jambo na Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa, wakati akisubiwa Dk. Magufuli kufika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba​
​
Baadhi ya viongozi na wana CCM na Makada wa CCM wakimsubiri Dk. Magufuli​
​
​
Msafara wa mgombea mteule wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli ukiwasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba​
​
Dk. Magufuli akisalimia umati wa wananchi baada ya kuwasili Ofisi ya CCM, Lumumba​
​
Wananchi wakimpungia mikono Dk. Magufuli baada ya kuwasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba

​
Dk. Magufuli akimsalimia Dk. Fenela Mkangara baada ya kuwasili chumba cha mapumziko kwa muda katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba​
​
Dk. Magufuli akimsalimia Dk. Didas Masaburi​


​
Dk. Magufuli akiwa na baadhi ya viongozi waandamizi wa CCM​




​
​
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akizungumza na Dk. Asha-Rose Migiro na Muhammed Seif Khatib​
​
​


​
Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali akimsalimia mgombea mwenza​
​
Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali akimsalimia Dk. Magufuli​
​
Dk. Magufui akimsikiliza kwa makini wakati Madabida akimweleza jambo​
​
Dk. Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Ilala Mussa Zungu​
​
Dk Asha Rose Migiro akiteta jambo na Sophia Simba na Amina Makilagi​
​
Dk Magufuli akisalimiana na Abbas Mtemvu​
​
Dk. Magufuli akitoka chumba cha mapumziko ya muda tayari kwa safari ya kwenda Tume ya Taifa ya Uchaguzi​
​
Dk. Magufuli akiwasalimia wananchi kabla ya kuanza safari​
​
Dk. Magufuli akiwasalimia wananchi kabla ya kuanza safari​
​
Mgombea mteule wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli na mgombea mwenza wake wakiwa katika gari la wazi kutoka Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, kwenda Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Picha zote na Bashir Nkoromo
​
 
Uchafu mtupu, yaani makada mletwe na magari, mpewe posho na msosi halafu mje kumshangalia Magufuli. Mwaka huu namba hazisomeki, Magufuli habebeki, jamaa ni Mzigo kwa CCM, Hana political Fan base yake, anajaribu kusafiria nyota za wenzake tu.
Mtambeba mpaka lini?
 

Kwani lowassa naye anafanyaje?
 
pinda simuoni hapa kwenye picha
 
pinda simuoni hapa kwenye picha

ccm imesambaratika yale makapi yote hayaonekani ameonekana kapi january na migiro makapi mengine yote yamesepaaa..hayajakubali matokeo
 

Ndio rais wetu anayesubiri kuapishwa...uchaguzi ni "fait accompli" tu
 
Duuh siamini kama magamba hayachangii uzi wao wako busy na Lowasa.
 
Ndio rais wetu anayesubiri kuapishwa...uchaguzi ni "fait accompli" tu

Hivi si ni tume hii hii ambayo EL atakwenda kuchukua fomu au? sasa siku hiyo ndo mtajua maana ya mafuriko ni nini ? sio haya majitu yenu mnayasomba kwa mabasi kwenda Lumumba siku hiyo mtakaa kitako kabisa ...subirini mbona mtafurahi sana
 

Ana nyota chafu sana huyu jamaa, habebeki wala nyota haing'ari.
 
Hayo mafuriko yasubiri tsunami ya Rais wa tano
 
I wish Pinda, Wasira and Sitta were present to cement the solidarity outlook.
 
Kama ni michuano basi CCM ameshalibeba kombe.

Nyie wenye vyama vyenu hao CCM hamuwawezi kwa chochote kuanzia mbinu na kila kitu
 
Uuuuwwwiiiiii October naenda kuwachinjia baharin
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…