Leak
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 52,845
- 43,318
Wasalaam wana jamvi.
Mtoto kwenye hiyo picha inasemekana alikufa lakini alifufuka baada ya kuombewa kwenye kanisa la Ngwajima huko Arusha.
Bado najiuliza walijuaje amekufa? si kwamba alizimia?
Mtoto kwenye hiyo picha inasemekana alikufa lakini alifufuka baada ya kuombewa kwenye kanisa la Ngwajima huko Arusha.
Bado najiuliza walijuaje amekufa? si kwamba alizimia?
- bishopgwajima KUTOKA UFUFUO NA UZIMA ARUSHA: Mtoto Julia wa miaka 9 baada ya kukufuka Jana baada ya maombi. Alichomwa na mwenzake na kalamu kichwani na akaanguka na kufa palepale. Walimu wakiwa wameuhifadhi mwili wake kwenye gari wakiwa ofisini wanapanga namna ya kuupeleka mochwari huku wanawasubiri wazazi wake ndipo mwalimu mmoja akatoa wazo waulete mwili wa mtoto kanisani tukaupoakea na tukaupeleka madhabahuni. Baada ya dk 48 Mtoto akafufuka. Na tayari wazazi wakawa wamefika wakampeleka hosptali kumtibu jeraha LA kalamu. Na mpaka sasa mzazi wa mtoto na walimu 3 wamempokea Yesu Jana baada ya muujiza huo. NI SAA YA UFUFUO NA UZIMA DUNIANI.