Ushauri kwa Wapenzi na Wanachama wa Chama cha Deokrasia na Maendeleo CHADEMA nimefurahi sana kuona vingozi wetu wanafanya juhudi kubwa kukitangaza chama Tanzania nzima ushauri wangu wa bure kwa muda huu Tanzania ni kubwa ssana Kijiografia kuifikia hadi uchaguzi mkuu 2015 ambapo watazania tuliokata tamaa tunategemea CHADEMA kuchukua Dola na kuwakomboa wanyonge ambao kwa miaka 50 tunaishi maisha ya kubahatisha,Viongozi wangu wa chama muda huu tufanye yafuatayo
1.Tujaribu kuitembelea Tanzania kuna maeneo makubwa sana wakati huu wanahitaji kuwaona viongozi wao wakuu ambao wamejiandaa kuwakomboa.
2.Mikoa kama Arusha,Kilimanjaro, Mwanza, Mbeya, Morogoro, Mara, Kigoma, tupunguze safari za huko na mikutano ya hadhara kwavile huko tayari tumeisha pata Uungwaji mkono tujaribu kuitembelea mikoa mingine ambapo watu wanashauku ya kuwaona viongozi wao ambao wanaweza kuwaondoa kwenye minyororo ya CCM viongozi mnapopenda kila siku kufanya mikutano ambapo tayari chama kina mtaji basi tutambue ya kwamba hasimu wetu atawkumbatia hao ambao hatuwafikii na kujitambulisha kwao. Nawaomba chonde chonde Dr, Slaa,Mbowe na timu yako zingatia ushuri huu.