Picha: Mkutano Wa ACT-Wazalendo, Shinyanga (Tarehe 19 Aprili, 2015 )

Mimi nilikuwepo hapo viwanja vya mahakama!
Kiukweli zitto hajazomewa, mtu pekee aliopigiwa kelele ni mama mwenyekiti(kama sijakosea cheo chake).
Lakini zitto, afande sele hawakuzomewa kabisa!!
Hizo ni chuki binafsi kuwadanganya watu.
 
ACT ni chama pekee kimeanzishwa na Vijana,Vijana wote ACT inawahusu,vingine vimeanzishwa na wazee
 
Tatizo wabongo tumekariri siasa za kupakana matope lakini sio za kujenga hoja ndio maana kwa hili wanasiasa wanaona na njia mpya ya siasa ambayo ACT wanatumia.
Wananchi walio wengi hasa wanachama wa vyama vya siasa wanatarajia kuona ZZK anawachambua na kuwaanika au kuyaanika mapungufu ya vyama vingine kama njia ya kujisafisha na kujitakasa lakini kinachomtofautisha huyu ZZK ni namna yake ya kujibu hoja na si majibizano sasa unakuta anaongelea mambo ambayo yanawafanya hata wapinzani wenzake kukosa pointi na kukalia kumuita msaliti bila kudadavua kiunagaubaga.
Siasa za ushabiki ndizo zinazoliangamiza taifa letu.
Pima hoja na si ushabiki
 
Enzi za Rwatonga Murema hadi wananchi walikuwa wanasukuma gari lake nowdays Murema hatumutambui tena kisiasa so wait zit
 
Wajiharishie marabili kaka?MPARE MNYIKA alikuwa na mkutano leo MWANZA watu waliohudhuria hata kwenye NOWA hawajai.

Kabila la Mnyika limekujaje hapo? Wewe kabila lako lina nini zaidi ya makabila ya wengine? Bull..hit
 
Yaani nimeshangazwa sana na baadhi ya wanachama wa vyama vya upinzani badala ya kupambana na chama tawala sasa hivi wanapambana na ACT hivi kweli inaingia akilini ndugu zangu GTs
Hapa ndo napata uhakika kuwa kama CDM haitajizatiti pamoja na huo UKAWA kura zitagawanyika kwani badala ya UKAWA kuwa na mpinzani mmoja CCM wana wapinzani wawili yaani CCM NA ACT hii ni mbaya sana kwa vyama vinavyounda huo umoja kwani kupambana na adui wawili inahitaji xtra skills and ability sasa je itawezekana kupambana na ACT NA CCM naona loop hole ileeeee kwa CCM kuwavunja miguu UKAWA
 
Mwisho lets observe this trend:
1995 Hakuna kama NCCR kwa upinzani
2000 Hakuna kama CUF kwa upinzani enzi za Ngangari na Ngunguri

2005 Hapa CUF inapoa inachipukia CDM UPINZANI
2010 Hapa CDM ilitisha
2015 Naona ni zamu ya ACT kung'aaa Upinzani nyie subirini
Na mwisho
2020 ni zamu ya Peter Kuga Mziray Kung'aa
 
Kijana unakataaa nafsi yako na kusaliti umma kisa umepewa hela au ahadi ya madaraka ambayo hujui utaipata ni ujinga mtupu yaani ukilaza unakuja unagombana na watu wanaotaka uje ujitambue kijana Wa aina hii ni LAANA kwa jamii yetu na nimpuuzi sana
 
acha ujinga mbona ndani ya chadema kuna padre, je unataka tuamini kuwa chadema ni chama cha kidini? unataka tuamini chadema ni chama cha kikanda? kipimo unachompimia mwenzio hicho hicho kitakupima na wewe
 
Mrema aliwahi kulalamika kwamba watu walisukuma gari take, walimbeba lakini kura hakupata.

Tanzania siasa ya vyama bado ni stronger kuliko individuals
 
Yaani nimeshangazwa sana na baadhi ya wanachama wa vyama vya upinzani badala ya kupambana na chama tawala sasa hivi wanapambana na ACT hivi kweli inaingia akilini ndugu zangu GTs
Hapa ndo napata uhakika kuwa kama CDM haitajizatiti pamoja na huo UKAWA kura zitagawanyika kwani badala ya UKAWA kuwa na mpinzani mmoja CCM wana wapinzani wawili yaani CCM NA ACT hii ni mbaya sana kwa vyama vinavyounda huo umoja kwani kupambana na adui wawili inahitaji xtra skills and ability sasa je itawezekana kupambana na ACT NA CCM naona loop hole ileeeee kwa CCM kuwavunja miguu UKAWA

ukitaja Act ndo ccm na ccm ndo actkwa hiyo chadema na ukawa tunapambana na ccm pamoja na matawi yake ambayo Ni act,tlp,udp chausita,ppt maendeleo n.k
kumbuka ukitaka kumfukuza chizi maeneo ya nyumbani kwako hakikisha unamtimua na makopo yake.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom