Picha: Mkesha wa Mwenge wa uhuru kijiji cha Nkinga Igunga

Hayo ndio matumizi machafu ya kodi zetu kugharamia mbio za mwenge na baada ya mda kuagiza dawa kwa waathirika wa ukimwi ambao wameambukizwa kupitia hii mikesha. Tutegemee ni nini kinafanyika kwenye hii mkesha zaidi ya kubadilishana maradhi.Kwanini mwenge usihifadhiwe kukikucha ndio kufanyike huo mkusanyiko je kuna shughuli yeyote inafanyika usiku huo.Sipati jibu kama kwenye msafara wa mbio za mwenge kukawa na mwathirika wa ukimwi nae akapanga kuusamba atausamba kwa watu wangapi kwenye hii nchi kupitia hii mikesha tunavyopenda kuwapapatikia wageni bila kujali madhara yao.
 

tusidanganyanye sasa hivi ni wakati wa utandawazi kama
ni mshikama kuna media kibao zinaweza kutumika
utamdanganya nani sasa hivi hata watoto wadogo wanajua?
kwa taarifa yako kama sio shinikizo kutoka kwa mkuu wa wilaya
waajiriwa wa serikali na wanafunzi kuudhuria hakika wangebaki hao wakimbiza huo moshi....period!
 
Gharama zinalipwa na wananchi waliochangia. kulikuwa na haja gani ya kuweka picha 3 zinazofanana??? ungeweka moja tu.
 
Gharama si ndio kodi zenu?? Alaf picha zako ni kama vile ulipiga ukiwa unavizia au??
 
Kesho tunaomba utupatie picha ya kuzagaa kwa taka za Kondom zilizotumika hapo nkinga maana mwenge huwa haulali sehemu hivi hivi bila hiyo shughuli

Nitafarijika sana condom zikionekana zimetumika manake mke wa rafiki yangu yupo huko anakimbiza mwenge
 

Usinikere na mifano yako mkuu. Mwenge wa Olympic una maana na TIJA usilinganishe na hizi shughuli za CCM
 
Gharama si ndio kodi zenu?? Alaf picha zako ni kama vile ulipiga ukiwa unavizia au??

Ni kweli mkuu,nimeshawahi kuzuiliwa kwenye mkutano wa Nchemba hapa Nkinga nisipige picha.ukizingatia wale mabaunsa waliokuwepo kipindi cha Nchemba ndiyo waliokuwepo kwenye mwenge.
 
Mbio za mwenge hazina tija nowadayz...zinawamulikia mafisadi sehemu nono..zinachochea ngono pia ni sehemu ya ufisadi.
 
ufujaji wa hela za umma...mwenge hauna maana kabisa zaidi ya kuenzi maneno ya mwalimu ''tutawasha mwenge na kuuweka juu ya mlima Kilimanjaro''......huku kuzunguka na kufuja pesa ndiyo nini sasa.....nchi yenye viongozi wavivu wa kufikiri....naililia Tanzania aaaah tanganyika yangu.
 
MWENYE KUJUA FAIDA ZA MWENGE KWENYE KARNE HII YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA ANIFAHAMISHE,Je ni busara mtu mzima kukesha unaangalia moto?je mwenge sio ushirikina fulani?
 
Mbio za Mwenge zimepitwa na wakati. Madhara yake ni mengi kuliko mazuri yake. 1. Unawafanya watu waache shughuli zao na kwenda kwenye Mwenge. 2. Mafisadi wa maofisini wanatumia mwanya huo kuiba/kufuja pesa za umma. 3. Watu vijijini wanachangishwa pesa zisizo na sitakabadhi eti ni kwa ajili ya Mwenge. 4. Na ni kweli kuwa katika mikesha ya Mwenge kunafanyika ngono - salama na zisizo salama. 5. Fedha nyingi zinatumika kugharimia magari, posho na gharama zingine za wakimbiza Mwenge. 6. Halafu kuna usanii kuwa Mwenge unazindua au kukagua miradi. Hivi bila Mwenge hiyo miradi haiwezi kufanyika? Mchango wake katika mradi kufanikiwa au kutofanikiwa ni upi? Pendekezo langu ni kuwa Mwenge uwe unawashwa mara moja kwa mwaka, tena katika Mkoa wa Kilimanjaro (Mjini Moshi) halafu upandishwe juu ya Mlima Kilimanjaro. Baada ya hapo ushushwe na kuzimwa na maisha yaendelee. Capt. Nyirenda aliupandisha Mwenge juu ya Mlima Kilimanjaro hakuzunguka nao nchi nzima. Mwenge kwa sasa ni ufisadi. Mwenye kujua faida za Mwenge (kwa sasa) naomba hatujuze hapa.
 
Usinikere na mifano yako mkuu. Mwenge wa Olympic una maana na TIJA usilinganishe na hizi shughuli za CCM

haaa kumbe tatizo hapa ni ccm na siyo mwenge,watz tunakaugonjwa fulani cha kutokikubali kitu chetu hata siku moja nini tija ya mwenge wa Olympic ?
 

Kujenga mshikamano wa kitaifa ambao hivi sasa umeanza kupotea kutokana na kutokuwepo kwa shughuli ambazo zinatuunganisha watanzania bila ya kujali rangi,dini wala kipato lakini pia kinawaamasisha wana jamii kuwa na moyo wa kuchangia miradi ya kijamii mfano shule,zahanati maji nk
 
Sijawahi kujua maana ya hii makitu! Ni wastage of money, time, resources etc! Yaani ni ujinga wa hali ya juu!
 
labda ni kweli tupu lakini kuna virahisishi na mwenge ni kimojawapo.
 
Wengi walikuwa wanafunzi wa Ulaya secondary.na pia kulikuwa na sare za tishet nyeupe za mwenge.Cha kushangaza makarani wa sensa walikosa hata sare za sensa lakini za mwenge zimepatikana.
na nyie nao!!yaani mlikosa majina ya kuita sekondari yenu hadi mkaita ulaya!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…