Nanyi watu wa Mtwara mmetuchosha!. Gas Gas, kwani uchumi wenu huko ni gas tu? Mkiachiwa kama mnavyodai, mtaweza kuimanage hiyo gas hadi ilete matokeo sahihi? Mbona watu wenyewe maneno mengi lakini juhudi za kutafuta maarifa ya maendeleo habaaa? Waaaii! Mie nimejichokea mwaya.
Na kama kuna chama, idara ama mtu yeyote anatengeneza umaarufu kwa kubrain wash watu kama hawa, anatengeneza mazingira magumu hata kwake akipewa utawala.
Ikumbukwe kwamba umaskini wa wa Tanzania unauhusiano wa moja kwa moja na uwezo wa upper stairs. Ndiyo maana wanachagua ccm kila wakati huku wana vidonda vinavyooza katika maisha ambavyo vimesababishwa ha hao hao ccm, na wala hata bandage na dawa za kutibia hawapewi.
Tatizo ni ule uwezo wa upper stairs ndio unawafanya waichague ccm huku wakiugulia maumivu yake.
Wanasiasa wetu mnapaswa kuliona hili na mjue kwamba kutoa hamasa bila elimu inayojengwa msingi wa uelewa na kuchanganua na ku reason, mjue kwamba hawa watu watakariri hayo hayo. Na watakariri kwamba njia sahihi ya kupata haki ama maendeleo ni vurugu. Na kwamba ni lazima wapate haki hata bila kuangalia upande wa nyajibu na michakato ya maendeleo.
Watakapo wapa fursa ya uongozi, watategemea kila kitu kishuke bila mchakato, bila juhudi zao binafsi na hawataangalia suala la uwajibikaji. Na kwaa kuwa watakuwa wamekuwa wa hivyo, itakuwa ni vigumu sana kwao kufuata mipango na hatua zake ambazo mara
nyingine huhitaji subira na muda. Hivo watu hii wataanza kufanya fujo wakijua ndiyo njia ya kuspeed up upatikanaji wa matakwa yao. ccm nao kwa kuwa ni makamanda wa hila, wataanza kuweachochea. Sasa pamoja na umaskini wa
mali, ujinga na matatizo kibao ya watz, kutaongezeka ile kitu naitwa furugu.
MIMI NAOMBA WADAU WOTE WA MAENDELEO TUTOE ELIMU YA MAENDELEO KWA WATU WOTE ILI WAJUE, PAMOJA NA KUDAI HAKI, LAKINI PIA WAJUE KUNA WAJIBU WAO. PIA MAENDELEO NI MCHAKATO UNAOHITAJI USHIRIKIANO, UTASHI, UPENDO, JUHUDI NA MAARIFA.