Hapo maskini karunguyeye, ameonewa sana, sijui itakuwaje? Nyani anashangilia mtihani ulivo rahisi, Kipepeo daa! kamependelewa sana, kwake kama kumsukuma mlevi huo mtihani atapita kirahisi mno, Nyoka anamsanifu mwlm kimoyoymoyo, kitu ubua tu huo.
Ngoma iko kwa Simba anatamani but mpaka roho inamuuma, atafanyaje?, Mamba wa watu ndo kabisaaa msindikizaji atajirudia zake majini. tembo anajiuliza kwa ukubwa wake huo atazarauliwa sana akishindwa hapo kuna mawili auvuruge mti, na kukatakatamajani au ajiue.
Kuna makundi ya watu wa aina hizi Duniani wengine ni kina karunguyeye na wenzake, wengine kipepeo na wenzake mwalimu ametoa kitu (Mtihani) bila kujali hali zao. wazi nyani na wenzake wamependelewa! nauliza sasa Elimu yetu kwani ni ya upendeleo?