Imekuwa ni kawaida kwa WanaCDM wakiongozwa na Katibu wao Mkuu kutoa matamko yasiyo na tija hasa katika swala la maendeleo ya Taifa letu, matamko ambayo mengi yamejaa kejeli na uhuni unaopaswa kupuuziwa kuliko upuuzi wenyewe.
Katika kudhihirisha kuwa hawajui wayanenayo leo Mwenyekiti wa CDM Taifa amesikika akitoa tamko ambalo kimsingi litakuwa kama funzo kwa Katibu wake Mkuu na baadhi ya WanaCDM.
Mbowe kasema yeye amezunguka sana hapa Nchini kwa anga na barabara na amejionea maendeleo ambayo Serikali ya CCM imefikia na kwa hilo anampongeza Rais pamoja na Serikali yake. Hapa Mbowe hakutaka kumumunya maneno hata kidogo.
Hili ni fundisho kwa Slaa na wenzie ambao wamezoea kutamka kuwa miaka 50 CCM haijafanya kitu. Lakini nimekuja kugundua kuwa Samaki akianza kuzeeka huanzia kwenye Ubongo.
Mh. Freeman hongera sana kwa hayo uliyoyaona na kuyasema na tunaamini kuwa utaendelea kuwaeleza na hao wengine na wataelewa tu taratibu