Regia Mtema
R I P
- Nov 21, 2009
- 2,970
- 873
Wakuu, Salaam!
Jana nilikuwa kwenye maandamano katika Wilaya ya Chato nyumbani kwa Maghufuli ambako kulikuwa na umati mkubwa wa watu. Maandamano yalikuwa ni ya Kilometa nane yaliyoshirikisha magari,pikipiki na waendao kwa miguu. Baada ya maandamano kama kawaida ulifanyika mkutano mkubwa wa hadhara. Leo wakati tunarudi Mwanza tukafanya maandamano madogo na mkutano wa hadhara katika Kata ya Katoro jimboni Busanda ambako nako watu walijitokeza kwa wingi. Hakika watanzania wameamua kuunga mkono mabadiliko. Kama tungeanza mapema vuguvugu hili nadhani saa hizi tungekuwa tunazungmza mengine kabisa.
Maandamano Kanda ya Ziwa ndio yamehitimishwa na baadhi ya Viongozi wamesharejea kwenye Makazi Yao. Wengine bado tupo hapa jijini Mwanza tunakula Sato. Tumehitimisha kwaajili ya kufanya tathmini na kujipanga upya kwaajili ya Kanda zingine.
Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke.
Kutoka Jijiji Mwanza
Regia E Mtema
Waziri Kivuli- Kazi na Ajira.
============================
Nimependa sana hii picha...Kazi nzuri sana Mh...Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke.
wanawewesuka tu sasa hivikwahakika hakuna atakaye kimbia mabadiliko haya.
Ukifanya analytical analysis inakuwa vigumu sana kuelewa CCM walishinda vipi Urais na idadi kubwa ya wabunge only 4months back??? The only conclusion ni Uchakachuaji wa hali ya juu, na kama uchaguzi huru ukifanyika TZ hata kesho CHadema ni RULING PARTY.
Kila la heri Dada Regia, lakini nadhani sasa uongozi mzima wa chadema ukae chini na wanasheria ili kucover all the bases, ili kila matamshi yawe ndani ya sheria, maana JK na serikali wamepigwa na hofu na kitakachofuata ni mabavu ya dola. Ni muhimu sana kwa sasa hivi kuwaelimisha wananchi matumizi mabaya ya serikali, upotevu wa pesa za umma na mambo mengine bila kusogea hata kidogo kwenye gray area yoyote kisheria, sababu hamna haja MAPENZI YA WANANCHI KWA CHADEMA YANAKUWA NATURALLY sababu ya upuuzi wa serikali.
May God Bless Tanzania.
Mkuu analysis gani tena hapo wakati picha zinajionyesha. Watoto kibao hawapigi kura. Pia vijana kibao ambao kelele nyingi lakini hawapigi kura. Unawaona wazee wangapi kwenye hizo picha? Wazee wengine ndio huwa wanapiga kura, ila wapo wachache sana kwenye picha ambazo nimeziona so far.