Elections 2010 PICHA: Kampeni za Kikwete jimboni Karatu

hapati kitu hapo aangalie picha za mwanza,kahama na bunda! eti anawaambia wachague CCm ili wapelekewe umeme vijijini,na kwamba idara ya maji inaendeshwa km idara ya mtu binafsi so what!?
 
Kwani JK asingeenda, wakaenda Ze Komedy kukata viuno bila kiingilio, watu wasingejaa uwanja? Kuna watu watatu nimewaona nawafahamu ni wauza mitumba wa pale Monduli, hawana cheo chochote CCM, sidhani kama hata kadi ya uanachama wanayo!!
 
Hakuna kitu, watu wameenda kuwaangalia kina Joti wanavyokata mauno na si kumsikiliza Kikwete. Nashangaa CCM chama kikongwe kabisa kinatumia nguvu nyingi na pesa kibao kwenye kampeni kwa nini? hapo mtu makini lazima ajiulize mara mbili.

Habari za uhakika zinasema CCM walikodi magari toka Arusha mjini na sehemu zingine kupeleka watu Karatu. Kina Joti hiki ndiyo kipndi cha kumaliza nyumba na kujijenga ki maisha.
 
Binafsi mimi ni mkazi wa Karatu mjini na nilibahatika kuhudhuria Mkutano wa JK mambo yanayofanywa na JK na CCM ni ya aibu tupu.Watu waliofurika hapo wote asilimia kubwa wametoka Monduli,Mto wa Mbu na wengine Arusha mpaka jana saa nne usiku Magari yalikuwa yakifanya kazi ya kuwarudisha wana CCM makwao,Kwa kawaida watu wa Karatu hatujazoea Burudani kama za kina Joti na Wenzake kwetu ilikuwa ni lazima tuende kuwaona na juu ya umati wa watu hao nasikitika mpiga picha hakulenga watu wa Karatu waliokuwa pembezoni mwa uwanja hawana jezi za CCM.Halafu uwanja uliotumika ni uwanja wa CCM ni mfinyu mno watu hawa kama ingeklikuwa ni uwanja wa Helicopter wa Mbowe ambao tumezoea Chadema wanapofanyia Mikutano yao ingekuwa ni aibu kwa CCM na JK.
Kikubwa ni wape pole wana CCM kwa ujinga walionao mpaka sasa.Karatu Hatudanganyiki kwa kweli,wamegawa T Shirt na Kofia mpaka kwa vichaa barabarani sasa hii ni akili kweli?
 
wamesomba wanachama wao wa arusha mjini kwenda kuwasapoti..
Ukitaka kuamini hebu angalia video za uko karatu utaona watu ni wengi lakini wanaoshangilia ni wachache saaana, sio karatu tu pia hata mikutano mingine ni hivyo hivyo...
Yan wananchi wanaenda kuangalia na kusikiliza muziki.. Mana ni shoo ya bureeeee
 
Kwa mantiki hiyo, kama kura zingepigwa muda ambao JK anafanya mkutano basi sehemu ama majimbo mengine yanayo zunguka sehemu ulipo huo mkutano, ccm wangepata sifuri kwa sababu wana ccm wote wamehamishwa kwenda kujaza mkutano.
 
wamesomba wanachama wao wa arusha mjini kwenda kuwasapoti..
Ukitaka kuamini hebu angalia video za uko karatu utaona watu ni wengi lakini wanaoshangilia ni wachache saaana, sio karatu tu pia hata mikutano mingine ni hivyo hivyo...
Yan wananchi wanaenda kuangalia na kusikiliza muziki.. Mana ni shoo ya bureeeee
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…