Picha hizi hatuwatendei haki Polisi


Huyu nae kashamwagiwa unga. Safi sana. Waendelee kupigwa picha hadi wakome. Polisi ni waonezi wakubwa sana. Asilimia kubwa yao!!

Ikiwa inawauma polisi wa chini kama mleta mada Mgirik, na wao wawapige picha bosi zao na kuwarekodi wanapowatuma kutushughulikia au kupeleka hesabu kila jioni. Nyambaaaaf....
 
Last edited by a moderator:

Hao watu walikupeje mkopo? Yani huwezi rudisha kabisa! Dah elimu ya hela inahitajika sana TZ. Sasa hio 5 ya kiwanja unampango wa kurudisha na 5 uliyo invest kwenye duka la jumla ambalo hujawahi hata kuanza!
Halafu mbona unaharibu thread?
 
huyo mwizI tu ana tingisha kiberiti humu na utapeli wake
 

Ni kweli polisi mmoja akifanya kosa haimaanishi ni wote na ndio maana hata waliofukuzwa kazi ni hao tu waliofanya kosa sio polisi wote,lakini jambo kuangalia ni wapi walipojikwaa sio walipoangukia na hii ndio nafasi ya kujirudi na wakae kwenye mstari vinginevyo katika hiki kipindi cha utandawazi wataumbuliwa mpaka wakose pa kupita. Hivi kama ushahidi wa picha kwenye mitandao umetosha kuwafukuzisha kazi hao wa chini vipi kuhusu zile picha za mauaji ya Mwangosi kule Nyololo na yule kamanda alipelekwa wapi?
 



Kamuhanda yuko Wizarani kwenye ofisi za makao makuu ya polisi anakula bata mzinga.
Na ameshiriki kutoa maamuzi ya kuwafukuza kazi wale madogo waliokua wanakulana ndimi kama njiwa.
 
Mimi na declare siwapendi polisi, ktk maisha yangu sijaona msaada wao zaidi ya kero kwangu na jamii. Sitegemei kuwa na rafiki polisi

Si bure utakuwa umetokea kwenye familia ya vibaka..huwezi kuwapenda polisi wakati una damu ya kihalifu.
 
Si bure utakuwa umetokea kwenye familia ya vibaka..huwezi kuwapenda polisi wakati una damu ya kihalifu.

Duuh! Thank you, nadhani wewe unanufaika na uozo wa mapolisi, Niwe mhalifu au sio siwezi badilisha msimamo wangu. Na popote wakiniletea za kuleta nawanyoosha. Nawajua hao watu kuliko unavyonidhania
 
Hao watu walikupeje mkopo? Yani huwezi rudisha kabisa! Dah elimu ya hela inahitajika sana TZ. Sasa hio 5 ya kiwanja unampango wa kurudisha na 5 uliyo invest kwenye duka la jumla ambalo hujawahi hata kuanza!
Halafu mbona unaharibu thread?

Achana naye huyo kule fb ametapeli sana ameliza watu..utaangukia pua.
 
ndugu zangu kama tumeweza kushirikiana hivi kwenye suala hili sasa kwa nini tusionyeshe msimamo huu kwenye rushwa?hapo tutakuwa tumefanikiwa.
 

Ktk social network nyingi hivi karibun kumetokea na hili jambo la kuwarusha askari wetu wakiwa kwenye matukio mbalimbali ambayo hayaendani na maadili ya kazi au maadili ya jamii.
KWA HIYO WALICHOFANYA HAO POLISI NI MAADILI??

Binafsi kama raia sijapendezewa na mambo wanayoyafanya askari wetu, ni mambo ya kulidhalilisha jeshi letu la polisi na kuidhalilisha sare ya jeshi ambayo ni moja ya nembo ya taifa hili.
KWANI ALIEDHALILISHA MAVAZI YA POLISI WALIKUWA NI RAIA AU NI POLISI WENYEWE?? HAO POLISI NDIO VINARA WA KUDHALILISHA RAIA..UMEZIONA PICHA ZA POLISI WA KIUME AKIWADHALILISHA WANAWAKE?? WEWE UNAFURAHIA HILO??

Lakin pamoja na udhaifu huo uliopo kwa hawa wenzetu, hatukupaswa kufanya kama hivi tulivyofanya. Kitendo cha kurusha picha hizi kwenye social network ni udhalilishaji mkubwa sana dhidi ya jeshi letu.

CHADEMA WALIPOSEMA KUWA MWANDISHI WA HABARI KAUAWA NA POLISI, CCM NA POLISI SI WALITOKA MAPOVU KWA KUKANUSHA NA WALITAKA UTHIBITISHO…SASA BAADA YA KUPEWA ZILE PICHA SI WALIKAA KIMYA NA AIBU ZAO…NDIO KUSEMA POLISI WANATAKA UTHIBITISHO NA PICHA HAZIDANGANYI..



Nikweli yawezekana ikawa njia moja wapo ya kuwaamsha kuwa wawe makin ktk utendaji wao na hhasa wawapo maeneo ya kazi lakn kuna picha zingne zmevuka mpaka.

TULETEE HIZO PICHA UNAZOZIONA HAZIJAPITA MIPAKA..TUNATAKA JEMBE LIITWE JEMBE NA SIO KIJIKO..HATUWEZI KUENDELEE KAMA TUTAKUWA WANAFIKI NA WAOONGO

Tutambue kuwa askari naye ni binadam kama tulivyo mm na ww nayeye anamapungufu kama binadam kwahyo ni bora tukatumia busara zaidi kuliko hivi tunavyofanya.

Inafikia hatua unampiga picha akiwa amesinzia bila kuangalia kuwa huyo askari na yeye anachoka kama ambavyo tunachoka mm na ww.

MKUU SASA ASKARI KABLA YA KUJIUNGA NA HIYO KAZI SI ALIJUA UGUMU WA KAZI HIYO?? SI ALIAAPA KUWA HATA FANYA UZEMBE KAZINI…KWA HIYO HUYO ASKARI AKISINZIA AKIWA MLINZI WA BENKI TUMWACHE TU MKUU ETI AMECHOKA??

Tukumbuke kuwa kabla mm na ww hatujaamka kwenda kazn hawa jamaa wanakuwa wapo barabaran mpaka mda tunapokuwa kazn wao bado wanakuwa barabaran kwaajili ya usalama wetu sasa kwann tufikie hatua ya kuwadhalilisha kias hcho?
KAKA MBONA SISI WALIPAKODI WENGI TUNAFANYA KAZI HUO USIKU!!! MKUU SIO SIRI WENGI WA HAO ASKARI BARABARANI WAMEKISIRI KTK KUPOKEA RUSHWA…MKUU KAMA UNAENDESHA GARI HUJAWAHI KUSIMAMISHWA NA HAO POLISI BILA KUWA NA KOSA…NA WAKATI MWINGINE WAKIKOSA KOSA WANAKUDAI ETI UWAPE TU HELA..


Ni bora kama umemuona amekaa mahali kasinzia nenda kamwamshe hata yeye atakuona unamaana zaidi kuliko kumrusha kwenye mitandao.

UKAMWAMSHE???!!! UNATAKA AKUTUKANE..POLISI TANZANIA HII WANAJIFANYA KAMA MUNGU MTU


Hebu fikiria angekuwa babayako,mama yako au dadayako au kaka yako ndio anarushwa vile na baadae anafukuzwa kaz kwa kosa dogo ambalo hata ww unauwezo wa kumsaidia.

KOSA DOGO KUPIGA PICHA ZA UZEMBE KAMA HUO..YAANI MKUU KAMA ANGEKUWA NI MKE WAKO KAPIGA PICHA ILE UNGEFURAIA???SI UNGETANGAZA TARAKA CHAPCHAPU!!!!

Tukumbuke kuwa maisha yetu watanzania huwa walio wengi tunategemeana, unapomfukuzisha kazi mwenzako tayari unakuwa umewarudisha nyuma watu wengi sana wanao mtegemea.

ANAPOFUKUZWA POLISI MMOJA SIO KUWA NAFASI HAIZIBWI…KUNA WAZALENDO KIBAO WATAZIBA HILO PENGO…HAPO ANAYEAJILIWA ATATEGEMEWA NA FAMILIA MPYA

Kama wabunge wenyew pamoja na kuwa na viyoyozi ukumbin lakn bado wanasinzia sasa sembuse askari anayepigwa na jua masaa12?
WAPINZANI WANAPOTAKA KUFANYA MAANDAMANO YA KUPIGANIA MAISHA DHIDI YA HAO WABUNGE SI HAO POLISI NDIO WANAWANYANYASA WAPINZANI, WAKATI WABUNGE WAKIPATA KIYOYOZI NA KUSINZIA BUNGENI…NA HATA WABUNGE WENGINE WAKIDIRIKI KUINGIA MSITUNI(KOMBA) NA MPAKA LEO HAJASHIKWA


Lakn haya tunayoyafanya huku ni kuwaonea tu hawa wenzetu.

MKUU WATU WANAFANYA UFUSKA NA WANALALA NA KUWAPIGA RAIA NA KUWABAMBIKIA KESI RAIA WAKAWAIDA UNASEMA TUNAWAONEA!!!

Kumbuka hata polis wao sio wote ni wadhalim bali wanashindwa kufanya maamuzi sahihi ya haki kwasababu ya kusaka tonge, wanaogopa wakienda tofauti na maelekezo watapoteza kazi zao kitu ambacho kitakuwa janga kwa familia zao na wategemezi wao..
MKUU KAMA KWELI DHAMIRA YAKO INAMWOGOPA MUNGU SI DHANI UTASHIRIKI UOVU ETI SABABU YA KUTAFUTA TONGE..MKUU UKO TAYALI KWENDA KUMBAMBIKIZIA MTU KESI YA KUUA ETI SABABU UNATAFUTA TONGE??

KIIFUPI MKUU HAPA TANZANIA HAKUNA MAHUSIANO MAZURI KATI YA POLISI NA RAIA….POLISI WANAJIONA KAMA MIUNGU MIDOGO NA WANATAKA WAOGOPWE WAKATI UWEPO WAO PALE NI TOKANA NA KODI YAKO…WANANCHI WAKAWAIDA WANACHUKIA KUWA IWAJE KODI YANGU ITUMIKE KUNUNUA RISASI YA KUMUA RAIA BILA KOSA?? AU KUMBAMBIKIZIA MTU MAKOSA YA AMBAYO HAKUSTAIRI?? WANGAPI WANASOTA MIAKA KIBAO JELA KWA KUONEWA??.
 
Duuh! Thank you, nadhani wewe unanufaika na uozo wa mapolisi, Niwe mhalifu au sio siwezi badilisha msimamo wangu. Na popote wakiniletea za kuleta nawanyoosha. Nawajua hao watu kuliko unavyonidhania

huku mitandaoni nnajua sana kuongea ila mtaani kimya na mnanyooshwa vilivyo na watu kama wewe ndo wale wamenyong'onyea kama kuku aliyenyeshewa
 
Siku hawa jamaa ukiingia anga zao vibaya ndio utajua kuwa hawa jamaa ubinadamu hawaujui, hata kama una haki na huna kosa utaisoma.
 
huku mitandaoni nnajua sana kuongea ila mtaani kimya na mnanyooshwa vilivyo na watu kama wewe ndo wale wamenyong'onyea kama kuku aliyenyeshewa

Bahati mbaya hatujuani, na wewe kuwa na hisia hizo upo sahihi coz zinawakilisha jinsi ulivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…