Picha hizi hatuwatendei haki Polisi

Uko sawa mkuu, watu ni wanafiki sana wanakaa kutafuta udhaifu wa wengine ilihali nao ni wanadamu na hawajakamilika sio tabia nzur unapomfanyia mtu kitu vuta picha ndo wewe. Mwenye tabia za kinafkii dzain aache use......
 
Hao polisi baadhi yao si watu ndiyo maana wakikutana JWTZ lazima moto uwake kwa njia hii au nyingine tabia yao ya kubambikizia watu kesi kupiga watu kuua watu kwa visingizio mbalimbali,sasa hivi hili jeshi limekuwa si kulinda raia na mali zao bali ni la Kupiga watu tu.mimi hata siwaonei huruma maana wao hawana huruma wakikuamlia.
Hebu angalia hii wanaua nyoka!
 
Hao unaowatetea walishafuzu pale CCP wanajua kila kitu tatizo lao walishabweteka wanajifanyia wanavyotaka wenyewe hata kama sheria inawakataza kufanya hivyo,Mwangosi walimuua kwa uzembe kama huu na aliyefanya analindwa sasa wamezoea mpaka wanajifanyia vitendo ambavyo havisitahili,walichopata ni haki yao ili iwe fundisho kwa wengine.
 

Hali hiyo imejitokeza kuwa hivyo na itaendelea kukua kwa sababu polisi wameonekana kuwanyanyasa wananchi. Sijui kama ni kwa ubabe wao au kwa kuogopa viongozi wa serikali, lakini wamekuwa hawatumii busara katika mambo wanayowafanyia wananchi. Katika mazingira ya namna hiyo huwezi kutegemea kuwa mwananchi atakuwa na mapenzi mema na polisi. Ni jukumu la polisi kuangalia upya mahusiano yao na wananchi siyo kudandia tu amri za kisiasa za kulinda maamuzi ya chama kinachoshikilia dola. Sihitaji kutoa mifano, wewe mwenyewe unaifahamu.

Kuhusu picha napo sitetei, maana wamefanya uzembe wenyewe. na kama wale waliokuwa wanafanya mahaba nahisi kama tutawatetea kuwa kwa sababu wanatumia muda mwingi kazini kwa hiyo hawapati muda wa kufanya starehe! Upuuzi. Kila mtu anajua kazi inataka nini kabla ya kuiianza na hata akishaanza kazi. kama mziki wake huuwezi tafuta nyingine. Kufukuzwa kazi hawajafukuzwa na watu kwenye mitandao, wamefukuzwa na viongozi wao kwa mujibu wa sheria zao za kazi. Wabunge wanaosinzia bungeni kila mtu anajua nani mwajiri wao, ni wananchi waliowachagua. Kwa kuwa na wao picha zinarushwa mitandaoni, ni jukumu la wananchi kuwawajibisha baada ya miaka mitano, (maana katiba ya Chenge kwa kufuata mapendekezo ya JK imeondoa uwezekano wa kuwawajibiisha mara moja). Kama wananchi wakiwachagua tena kwa sababu ni wa chama chetu, basii wanastahili mabaya yote yatakayotokana na uzembe wao, na hapa hakuna wa kumlaumu zaidi yao wenyewe...

Kifupi mtoa mada na waliokuunga mkono wote mmedandia mantiki ya suala hili.
 

Mkuu hapo wa kulaumiwa ni wenyewe kwa wenyewe mf ile ya vichakani ni mwenzao ndio amefanya hivyo naye pia kachukuliwa hatua kali ifike mahali viongozi wao wakae na askari wao kuwasisitiza kuishi kwa upendo..
 
Umehack akaunti za watu kule facebook na huu uzushi wako umeona hujafanikiwa ukaamua kuhamia JF. Ila kumbuka huku ni kwa great thinkers sidhani kama utapata mtu wa kumtapeli..
Note:wakuu kaeni chonjo na matangazo ya hivi

Tapeli tapeli tapeli iii huyo...umekosea njia huku jf watu wanajitambua vizuri.
 
Polisi wenyewe hawawatendei haki wananchi na ndicho kiini cha wananchi kuwa na chuki nao. UKuta wameujenga wenyewe. Na kama viongozi wa jeshi hili wataendelea kuwa vibaraka wa ccm, mumiani wa wananchi, watakaoathirika na askari wadogo wadogo wanaotumwa kutelekeza maazimio ovu ya wkaubwa wao. Na bahati mbaya wengi wanaishi uraiani ambako maisha yao yote yamezingirwa na hao raia wanaoonewa.

La kufanya, ccm ibadilishe sheria ili makosa wanayofanya yasiwe makosa kama vile ilivyo halali sasa kwa ufusika uliokithiri, rushwa, ufisadi, uzandiki, uvunjaji wa katiba na haki za binadamu kwa ccm na serikali yake. Hii itakuwa ni njia pekee ya ccm kuwatetea, kuwalinda na kulipa fadhira kwa askari.
 

kafungue bar ili polisi waje kulewa tuwapige picha kisha tuipost humu
 
Mtoa mada umeongea ukweli sana ila cdhani kama kauli yako wahusika wataifanyia kazi. Mfumo umeharibika sn. Pole
 

Kula like utetezi Maneno meeeengi! Halafu pumba tupu...
 
Ndio polisi wetu hao hao anaowatetea mtoa mada!

mkuu KUNGUNI wa majuu umeuelewa uzi wangu lakn?
Picha kama hii hyo ndiyo ilistahili kuishikia bango kwasababu huo ni ukiukwaji wa haki za binadamu na hcho kitendo kinamadhara kwa jamii.

Lakin picha kama za kusinzia na kula denda unapozishikia bango zile zna madhara gani kwetu wananchi? Au znaathiri vp uchumi wa nchi mpaka tuzikomalie vile?

Tubadilike jaman tuwe na mawazo na matendo ya kimapinduzi
 
Last edited by a moderator:
mleta mada anachojaribu kusema ana manisha kiongozi na mtu wa chini wakifanya makosa wote waadabishwe sawa... kunguni wa ulaya

bila shaka ndug yangu mrangi tena tuangalie na yale mambo mazito ambayo yanaweza kudhoofisha uchumi,haki za binadam au kudhoofisha aman ya nchi hayo ndio mambo ya kuyakomalia lakn tunapokaa watu na vipara na vitambi vyetu tunakomalia kitendo cha askar kulana denda na kusinzia huo ni wepesi wa akili
 
Last edited by a moderator:
Soldier mbona wayafukuzwa wengi km picha zao zikiwekwa hapa?

Huyu naye afukuzwe kwa kunywa bia na kuichezea kofia ya geshi ra PORISI
cc Mgirik
 

Nakubaliana kabisa kwamba maadili yameporomoka sana. Ikumbukwe kuwa jeshi la Polisi pamoja na mabaya yote , ni mali ya wananchi.
Tabia inayoendelea siku hizi ya kupa-publish maswala ya kipolisi kwenye mitandao ni kosa kubwa kwani ikumbukwe kwamba polisi mmoja ama wawili wanapofanya kosa hawaliwakilishi jeshi la Polisi. Ni matendo ya watu binafsi kama binadamu wengine.
Lakini kwa upande mwingine jeshi la polisi nao wajiangalie na kujichuja wenyewe. Hivi, kwa mfano karatasi ya simu ambayo hivi karibuni imezagaa kwenye mitandao ikiwa ni amri ya Trafic hq kubadilisha kazi kwa ma-Wp wawili waliofanya kazi kizembe ilitokaje kwenye mafaili ya Polisi hadi mitandaoni? Je,huko siyo kufanya kitendo kibaya kinyume na sheria za polisi?
Hii maana yake kuna watu waliopewa dhamana za utunzaji wa nyaraka hawajatimiza wajibu wao.
Polisi na nyie safisheni nyumba yenu kwanza. Mu hodari wa kupeleleza makosa ya wengine, munashindwaje kupeleleza kwenu?
Jamii ielewe kwamba pamoja na makosa wanayoyafanya polisi, pamoja na kutowapenda kote , pamoja na kuwaita majina yote ya kifedhuli kama vile policcm na mengineyo, bado tunalihitaji jeshi la polisi kwa kiasi kikubwa.
Fikiria jeshi la polisi lisimame kufanya kazi kwa saa moja tu, madhara yatakuwaje!
 

hata mm naelewa hilo lakin sasa kwann tusiwakomalie hasa pale wanapofanya ubaya kama huo?
Kama kuwabambika watu kesi, kuwapiga raia pasina kosa hapo ndio mahala pake pa kuwabana.

Vile vile hayo uliyoyasema hayaamuliwi na askari wa chini hayo yote ni uongozi wa juu ndio unatakiwa kuubana
 
Mimi na declare siwapendi polisi, ktk maisha yangu sijaona msaada wao zaidi ya kero kwangu na jamii. Sitegemei kuwa na rafiki polisi
 
wameyataka wenyewe! na watarushwa sana mitandaoni mpaka wanyooke. Wananyanyasa sana raia hawa watu.
 
Umehack akaunti za watu kule facebook na huu uzushi wako umeona hujafanikiwa ukaamua kuhamia JF. Ila kumbuka huku ni kwa great thinkers sidhani kama utapata mtu wa kumtapeli..
Note:wakuu kaeni chonjo na matangazo ya hivi

hahahaa huyu kama kashindwa kutapeli kule facebook ataweza huku, ameruka majivu atakanyaga moto!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…