Picha: CHADEMA yavuna mamia ya wanachama Nzega, Dr. Slaa aitikisa Nzega

Picha: CHADEMA yavuna mamia ya wanachama Nzega, Dr. Slaa aitikisa Nzega

Crashwise

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
22,227
Reaction score
8,760
Wakati chama cha demokrasia na maendeleo kikizidi kunadi sera zake jana kilifanikiwa kuvuna mamia ya wanachama kama picha zinavyoonyesha hapo chini..Peoplesssssssssssssssssssss
Kansa Mbarouk akitoa kadi.JPG
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mkoa wa Tabora, Kansa Mbarouk, akimkabidhi kadi ya uawanachama wa chama hicho mmoja wa wakazi wa kijiji cha Ngw'aluzwilo, baada ya mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa chama hDk. Willibrod Slaa jana.
Slaa akikumbatiana na mbunge wa zamani.JPG
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa akikumbatiana na mbunge wa zamani wa jimbo la Bukene mkoani Tabora, Steven Kahumba, baada ya mkutano wa hadhra wa kujenga chama uliofanyika katika mji wa Bukene juzi.
View attachment 128145
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, akikabidhi kadi ya chama hicho kwa mmoja wa wakazi wa kijiji cha Ngw'aluzwilo katika Kata ya Lusu jimbo la Nzega, baada ya mkutani wa hadhara kijiji ni hapo jana, akiwa katika ziara yake ya kujenga chama.
Slaa kuhutubia Nzega 1..JPG
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa akiwahutubia wananchi wa mji wa Nzega, katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Setendi jana, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kujenga chama.
Slaa kuhutubia Nzega 3..JPG
CHADEMA MWENDO MDUNDO MAPA WANAFIKI WAKAAE....
​
 
Waje hapa wale wagonjwa waakili wa kule Lumumba tuwasikie,

Dr Slaa ni rais wa mioyo ya watanzania
 
Hakika kwa umati huu ni wazi ukombozi umefika.Inatia moyo sana kuona mamia ya kina mama wanachukua kadi za Ukombozi.
 
AHAAA ndio maana inamuumiza sana Zitto na magamba waliomtuma! Kweli hakuna zaidi ya Chadema
 
Kweli kuiaua chadema ni kazi ngumu jamani kumbe tabora inakubalika hivi ccm kwishney 2015
 
Kama Tabora nako wananchi wameamka hivi,bas ccm kwisha habari yake na 2015 watajibeba!
 
wala wala..watu wameunga foleni kuchukua kadi....?CCM wanapata huu ujumbe?
 
Naona pro-Chadema wameamua kujifariji na kujiliwaza.
 
peoplesssssssssssssssssss poweeeeeeeeeeeeeeeeeer. Maccm watakiona cha moto badala wafanye mambo ya maendeleo wao wanaacha ucngiz kwa ajili ya kuhonga watu wakichafue CDM
 
Matumaini ambayo yapo kati ya Wananchi na Chadema ni ya Kipekee, Mioyoni mwao pamejawa majonzi ya furaha kwa chama hiki, Wakinamama wakiwa mstari wa Mbele katikA mchakato huu, Ni furaha ambayo haina tafsiri kwa jinsi Chadema, Inaingia katik fikra za Watanzania kinamama wakiwa ni wahusika wakuu, Chadema kupitia Organization zake ni mgawanyo wa Majukumu ndio huwa na changamoto hususani kuwapa elimu ya Uraia watz.
Chadema kupitia Viongozi wa Kanda.
wangeamua jambo moja zuri na lenye Mantiki zaidi.
(1)Kila mwenyekiti wa Kanda husika awe na Ukaguzi w ChAma kila baada ya siku(21)Katika majimbo husika, Ili kuepusha ulazima wa Mtendaji Mkuu kufanya ziara Mwenyewe ktoka makao Makuu.
Mtendaji Mkuu atahitajika tu pindi kuna Dharura ya Kanda Husika, Mtendaji Mkuu akae Makao Makuu apokee kero zinazowasilishwa kwake.
 
Picha zile zile za uchaguzi mkuu 2010, zimetumika kwenye matukio yote ya ziara ya slaa mkoa wa tabora
 
peoplesssssssssssssssssss poweeeeeeeeeeeeeeeeeer. Maccm watakiona cha moto badala wafanye mambo ya maendeleo wao wanaacha ucngiz kwa ajili ya kuhonga watu wakichafue CDM
Amesemaje kuhusu gongo
 
Kuna haja ya kuwa na presentation zitakazo ainisha kila asset ya nchi hii na mchango wake kwa Taifa na jinsi ambavyo CCM wanavyovurunda kwenye Mali za Watanzania! Takwimu ni muhimu sana, kwa kuanzia napendekeza wakati wa ziara za kwenye majimbo wananchi wapigwe darasa kuhusiana na utajiri unaowazunguka na jinsi ambavyo CCM kwa kushirikiana na wageni wanavyowaibia! Mfano pale Nzega kulikuwa na mgodi wa Resolute, katka kipindi cha uhai wa mgodi iliingiza dolla kadhaa, wageni walikula kadhaa, halimashauri na serikali walilipwa kadhaa, gharama za kufunga mgodi ni 25% ya mapato yote ya mgodi! Kwanini wameondoka na kuwaachia mashimo? hiyo 25% ya mapato ya mgodi wamekula nani?... vivyo hivyo wakitembelea maeneo yenye Uranium, Almasi, vivutio vya utalii na hata kilimo... kunahata ya kujadili in terms of monetary values ... wananchi watawaelewa kwa haraka zaidi...
 
Back
Top Bottom