Picha 5: Muonekano wa Flyover 5 kali zaidi duniani

Sexer

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
8,216
7,907
1: Judge Harry, Marekani

Flyover hii imejengwa jijini Los Angeles, Marekani ambapo unaambiwa ina urefu wa zaidi ya futi 130 kutoka ardhini. Ilijengwa mwaka 1993 na ina uwezo wa kupitisha magari mazito ya mizigo.
IMG_9282.JPG


2: Spaghetti Junction, Uingereza

Ilijengwa mwaka 1965 na kujipatia umaarufu mkubwa duniani kwa namna ilivyojengwa. Ilipewa jina la Spaghetti kutokana na namna barabara zilivyojinyonga.
IMG_9283.JPG


3: Binhai, China

Flyover hii ilijengwa mwaka 2001 ikiwa na urefu wa kilometa 53 ambapo inaunganisha miji mbalimbali nchini humo.
IMG_9284.JPG


4: High Five, Marekani

High Five ilijengwa mwaka 2001 na inapatikana katika mji wa Dallas, Marekani ambapo inayaunganisha zaidi ya madaraja matano. Iligharimu zaidi ya Dollar 261 million.
IMG_9285.JPG


5: The Circle, Marekani

Ujenzi wake ulikamilika December 2016 na inapatikana katika mji wa Chicago, Marekani. The Circle ina uwezo wa kupitisha magari yenye uzito mkubwa na iligharimu zaidi ya Dollar 250 million.
IMG_9286.JPG
 
Duh! Kwa cc tuliozoea Morogoro road na Ally HassanMwinyi road unaweza kwenda kwa Trump ukajikuta umepita kwenye mafly over umetokea Mexico kwa wahuni. Ikimalizika bongo inabidi elimu itolewe kidogo or else kila siku itakua ni mwendo wa ajali na mpoteano
 
Wakati sisi tunashangilia uhuru waingereza walikuwa wana Flyover, baada ya miaka 50 tangu uhuru tunaanza mchakato wa Flyover sijui waingereza watakuwa wamejenga nini kwa hiyo miongo mitano.

Ukitaka kuwa na barabara za hivyo huku Afrika ni lazima uwe na mikakati ya muda mrefu na watu makini watakaojua dhana yako
 
Duh! Kwa cc tuliozoea Morogoro road na Ally HassanMwinyi road unaweza kwenda kwa Trump ukajikuta umepita kwenye mafly over umetokea Mexico kwa wahuni. Ikimalizika bongo inabidi elimu itolewe kidogo or else kila siku itakua ni mwendo wa ajali na mpoteano

IMG_9282.JPG

usiogope kiongozi, ukicheki hiyo picha upande wa juu kushoto utaona kabarabara kamepita, sasa hiyo ndo flyover yetu itakavyokuwa
 
Hahaha eti tuta!!! Unamaanisha lile la tazara mkuu?? Daaah bora hata ubungo interchange..
Mkuu ndio. Hata Ubungo kwa mwaka 2017 ni Flyover ya kizee sn. Inazidiwa na ya UK ya 1965.

Zote kwa picha za Aerial ziko kamw tuta.
 
Back
Top Bottom