Physics: Ugunduzi wa gravitation waves, je italeta mapinduzi gani zaidi katika sayansi

The hammer

JF-Expert Member
May 17, 2011
2,396
1,784
Habari wakuu,

Jana kama sikosei,wanasayansi walitangaza mapinduzi makubwa ya kugundua alichokisema Albert Einstein miaka mia moja iliyopita kuhusu kupata/kuwa na uwezo wa kuipima gravitation waves hasa zinazotokana na black holes au nyota zinazokaribia kufa kama sijakosea.

Kama tunavyojua ugunduzi wa gravitation force ilivyolete mapinduzi hasa katika flying object kama ndege n.k

Sasa je,hii gravitation waves inaweza kuja na lipi maana naona hili limepokewa kwa furaha sana kwa wanasayansi wengi duniani kwa kusoma comments zao.

Wanafizikia faida yake itakuwa ni nini hasa?
 
Uelewa wa gravitation force labda useme umesaidia katika kulaunch rockets na kuweka satellites angani, lakini sio ndege. Ndege ni maswala ya aerodynamics
 
Huu uvumbuzi wa hizi waves unathibitisha theory ya Einstein kuhusu spacetime ambayo inakinzana na theory ya gravitation ya Newton.
 
  • Thanks
Reactions: Lee
So maybe phyisics ya gravitation iwe modified ianze kufundishwa accoring to theory hii
 
Huu uvumbuzi wa hizi waves unathibitisha theory ya Einstein kuhusu spacetime ambayo inakinzana na theory ya gravitation ya Newton.
Sasa hapa ndo itakuwa kazi kweli kweli,yaani yale ma-pendullum bob nimeyafanya kuitafuta 9.8g inakuja kuwa uongo.

Hiyo spacetime ni nini na inaweza kukinzana vip na ya Newton
 
The hammer, space-time maana yake ni dimensions 4. Space ina 3: length,width na depth. Einstein aliongezea time kama dimension, so there are 4 known dimensions as of now. This is quite popular. Sasa Einstein alitheorize space as something wakati sisi tunadhani space ni nothingness. Kwa hiyo akasema space can be twisted and the extent of twisting depends on the mass of the body in that space. Google or youtube spacetime fabric if you are really interested
 
Kwa hiyo kwenye hii spacetime fabric, kwa mfano jua letu limeitwist sana kuliko sayari zake kwa hiyo sayari zinakua zinazunguka around as if to fall towards the sun... same case to our moon.
 
Newton alitheorize kwamba kuna nguvu ya uvutano kati ya vitu viwili na formula ndo ile unayoifaham. Lakini nini kinabeba hii force, wadau wakaja na theory kwamba kutakua na particles zinazobeba hii hii gravitation force, wakaziita gravitons, lakini mpaka leo hawajazigindua
 
Hii kitu ni ndefu sana, jaribu kusoma/kufuatilia astrophysics,quantum mechanics na particle physics. Pia hapa utagundua elimu tuliyosoma ni very outdated
 
mimi naona hii itakua ni pure physics, yaani ile physics ambayo haina application bali ni kuongeza knowledge tuu
 
Hua narudia mara kwa mara kwamba elimu yetu ni ya kuamini kile tunachoambiwa na wataalamu.
Kikibadilika leo tunabadili kile tunachojifunza na tunachokifahamu, au tulichowahi kujifunza.

Kwa mfano leo hii kunawezatokea mtaalam mmoja akasema maji yanachemka katika nyuzi 150 badala ya nyuzi 100. Itabidi tukubali tu. Hivyo basi uelewa na elimu yetu vinategemea sana kuamini vile tunavyoambiwa kadri ya maendeleo ya ugunduzi wa wataalam.
 
Huu ugunduzi utazidi kuiweka universe wazi, kwa kuistadi dark matter kwa urahisi. Maana katika hizi giants light or electromagnetic waves haziwezi kuescape kutokana na kuwa na g kubwa mno. mwanga husaidia optical telescopes katika uchunguzi wa distant objects, hata kama kama mwanga ungekuwa unaescape usingeweza kutuletea taarifa sahihi kutokana na multiple gravitational lensing effects pale utakapopita jirani na heavy masses. Matumizi ya radio telescopes yalishindikana for the same effects. Kwa hiyo kwa kugundua hizi g_waves kutakuza understanding of nature na kugundulika kwa technolojia mbalimbali in our spacetime. Labda wanasayansi wataweza kutengeneza time machine, na kuilezea kwa ufasaha wormholes za Sir Einstein (RIP), ambazo ni milango ya kusafiri kutoka universe moja kwenda nyingine. Time machine ni interesting, hutumiwa sana kwenye science fiction movies za holywood....ambayo ikitengezwa kama alivyo suggest Einstein itaongeza ugunduzi...Kwa time machine unaweza utembelea past yako au future yako....ni kama vile hadithi lakini Einstein aliona they are real things....the power of imagination is the source of knowledge and discovery.....
 
A very great innovation,sasa mipaka yao ya uchunguzi katika black holes imekuwa midogo kwani black holes was invisible by any kind of EMW,aisee hii elimu ya space ni pana sana,black holes zinatokea when heavy objects as stars zikiwa mwisho wa maisha yake kugongana na kutokea black holes at which kuna uvutano mkubwa sana kana kwamba hata mwanga hufyonzwa,ila kupitia gravitational waves as stated mr Einstein sasa nadhani watachunguza mambo mengi katika space time.
 
Habari wakuu,

Jana kama sikosei,wanasayansi walitangaza mapinduzi makubwa ya kugundua alichokisema Albert Einstein miaka mia moja iliyopita kuhusu kupata/kuwa na uwezo wa kuipima gravitation waves hasa zinazotokana na black holes au nyota zinazokaribia kufa kama sijakosea.

Kama tunavyojua ugunduzi wa gravitation force ilivyolete mapinduzi hasa katika flying object kama ndege n.k

Sasa je,hii gravitation waves inaweza kuja na lipi maana naona hili limepokewa kwa furaha sana kwa wanasayansi wengi duniani kwa kusoma comments zao.

Wanafizikia faida yake itakuwa ni nini hasa?
Mapinduzi yatakuwa makubwa kwa maana hata huu ugunduzi wa tar 11 mwezi huu inasemekana black holes hizo mbili ambazo zilikuwa zikizungukana kwa kasi sana kabla ya kugongana zilikuwa umbali ambapo ukisafiri kwa kasi ya mwanga ni miaka bilioni 1.3 ila wao walitumia 20 millisecond kupitia gravitational wave,JE HUO SI UGUNDUZI MKUBWA,Einstein aliongelea hili mnamo 1916,jamaa alikuwa Think Tanker.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom