Gravitational waves from black holes detected

mxyo16

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
1,243
758
Miaka karibu 100 iliyopita Albert Einstein, pamoja na theory yake ya General Relativity, alitabiri inapotokea nyota kufa (neutrons stars), au nyota mbili kuungana, (mfano jua letu linazeeka hapo baadae litakufa na kupasuka nakubaki kipande kidogo kigumu hivi ukubwa wa dunia yetu, sasa inaweza kuvamiwa na kajua kengine kalikokufa pia na ndio hapo dhoruba hutokea), au black holes mbili kuungana (black holes binary system) ile dhoruba husababisha gravitational waves, na akasema sio rahisi kuzi detect sababu ni very weak....

Wanasayansi miaka zaidi ya kumi iliyopita wametengeneza facilities kusaka hizo waves, sasa wamefanikiwa....wamezipata na wanaweza hata kuzawadiwa nobel prize.

Wanasema ugunduzi huu utawasaidia kuweza kuona na kugundua mengi yasioweza kuonekana kwa macho...... kama yaliyopo kwenye black holes, dark unverse etc na hata kuvumbua mpaka mwanzo wa unverse "the big bang" kutokana na hizo gravitational waves...
Wenyewe wanaziita ...ripples in the fabric of space and time

_88168345_gravitacijski-valovi.jpg

........ugunduzi wake ni kama wa DNA.
 
Walitumia satellite inayoitwa Gravity Probe B
nasa_gpb_news1.jpg

Gravity Probe B: Testing Einstein's Universe
Ni uvumbuzi mkubwa sana.
No sir, detection hii waliyoitangaza wametumia facilitities zilizopo hapa ground duniani.... process inaitwa LIGO yani Laser Interferometer Gravitational-wave Observatories...na hii chini ni moja kati ya lab zao zinazoshiriliana kufanya kazi kwa pamoja. na hujengwa kwa mfano wa herufi L
_83113973_83113972.jpg


picha uliyoweka inaelezea jinsi space warp inavyo happen as per Einstein.....pale dunia ilipo imesababisha curve kwenye space na kwahiyo chochote kitachopita hapo hakitapitiliza, bali kitavutwa na dunia na either kuizunguka dunia (orbiting)
 
No sir, detection hii waliyoitangaza wametumia facilitities zilizopo hapa ground duniani.... process inaitwa LIGO yani Laser Interferometer Gravitational-wave Observatories...na hii chini ni moja kati ya lab zao zinazoshiriliana kufanya kazi kwa pamoja. na hujengwa kwa mfano wa herufi L
_83113973_83113972.jpg


picha uliyoweka inaelezea jinsi gravitation wave inavyo happen as per Einstein.....pale dunia ilipo imesababisha curve kwenye space na kwahiyo chochote kitachopita hapo hakitapitiliza, bali kitavutwa na dunia na either kuizunguka dunia (orbiting)
LIGO ni muendelezo wa tafiti za gravitational waves as per Einstein .Nafikiri article hii ya Space.com inaelezea vizuri
Detecting Ripples in Space-Time, with a Little Help from Einstein
 
Field za watu hizi... Napenda kuyajua sema
Sio ngumu kuelewa. Ni kwamba miaka bilioni moja ilyopita (one bilion years ago) nyota mfu mbili (black holes) ziligongana na kutengeneza mawimbi (gravitational waves). Haya mawimbi yamesafiri kwa miaka mingi angani na kuwasili duniani miezi mitano iliyopita,na mawimbi haya yamegundulika duniani kwa kutumia vifaa vinavyoitwa Laser Interferometers. Utafiti huu wa aina hii ya mawimbi ulianza muda mrefu,takribani miaka 11 iliyopita..na ni utafiti wa kuthibitisha ugunduzi aliofanya Albert Einstein miaka 100 iliyopita.Albert Einstein aligundua mawimbi haya bila vifaa..kwa kutumia mahesabu tu. Watafiti wa sasa wanatumia vifaa na wamethibitisha kuwa Einstein ..licha ya kuwa hakuwa na vifaa ugunduzi wake ni sahihi na alikuwa anasema ukweli.
Triumph for gravitational wave hunt | Science
 
Sio ngumu kuelewa. Ni kwamba miaka bilioni moja ilyopita (one bilion years ago) nyota mfu mbili (black holes) ziligongana na kutengeneza mawimbi (gravitational waves). Haya mawimbi yamesafiri kwa miaka mingi angani na kuwasili duniani miezi mitano iliyopita,na mawimbi haya yamegundulika duniani kwa kutumia vifaa vinavyoitwa Laser Interferometers.Utafiti huu wa aina hii ya mawimbi ulianza muda mrefu,takribani miaka 11 iliyopita..na ni utafiti wa kuthibitisha ugunduzi aliofanya Albert Einstern miaka 100 iliyopita.Albert Einstein aligundua mawimbi haya bila vifaa..kwa kutumia mahesabu tu. Watafiti wa sasa wanatumia vifaa na wamethibitisha kuwa Einstein ..licha ya kuwa hakuwa na vifaa ugunduzi wake ni sahihi na alikuwa anasema ukweli.
Triumph for gravitational wave hunt | Science
Wenzetu hawakati tamaa na wanaamua na wanaweza na hawana muda na porojo.Sio sisi,tafiti kibao zinawekwa mezani.
 
Mh huyu Albert Einstein alikua si mtu wa kawaida.
Kama huyu jamaa miaka mia iliyopita aliwaza yote haya, nikweli kwamba waafrika hatukuwa na ma genius?

Iwapo historia na michoro kwenye mapango vinaonyesha zana za kale zilizo tengenezwa kwa mawe na baadae chuma na utumiaji wa moto kwa kupekecha vijiti, ambavyo vimeonekana duniani kote na kutumika na jamii zote,.....mie najiuliza tulikwama wapi mpaka wenzetu leo hii wametuacha kiasi hicho katika maendeleo ya sayansi na teknolojia...

Ila nahisi kwa watu weupe, majeshi ndio yaliyoleta chachu ya maendeleo katika teknolojia, kutaka kushinda vita na kutwaa maadui mali na ardhi zao kirahisi, labda uteketezwaji wa majeshi yetu uliua kabisa sayansi..

Mie naamini kama kabla ya tv kuingia kwa watu weusi, ile kwamba unaenda kwa mganga anakuonyesha kwenye chombo adui yako! Kitendo cha kuiongelea tu kama wasemavyo lisemwalo lipo.....nahisi hii teknolojia tulikua nayo sema tu iliiangamizwa....ila watu weusi ingetutoa sana kama...kina sony, apple, samsung...etc hili ni swala la "waves" na wote tuna lishuhudia sasa hivi kwenye tv zetu na simu....tunavyoona picha, video na kusikia sauti...
 
Wenzetu hawakati tamaa na wanaamua na wanaweza na hawana muda na porojo.Sio sisi,tafiti kibao zinawekwa mezani.
Nadhani sababu ni ukosefu wa viongozi wanaopenda maendeleo, wale wenye nia ya kuongeza ufanisi katika uzalishaji na kutoa huduma kwa wepesi katika jamii...
kama bosi wa shirika la nyumba alivyoweza kukopa bank za kimataifa kuliwezesha shirika, tupate wasomi wa kilimo nao wafanye hivyo, ma engineer wa UDSM, DIT, MBEYA TECH etc... nao pia wananafasi kufanya uwekezaji kwenye vitengo vyao.
 
Sasa hakuna madhara kwa dunia na vilivyopo kwa mawimbi hayo kupita karibu na sisi

Hakuna madhara, ila ni ufunguo kwa jamii ya wanasayansi kujua mengi kuhusu universe.....nifaida kwao....kubwa hasa ni kujua origin, kujua character zake, factors, na nini kifanyike au kujilinda na majanga mbalimabali yanayoweza kumkumba mwanadamu hapa Duniani......
nikama walivyoweza kugundua mawimbi yaliyo tuwezesha kuwa na mawasiliano ya redio, simu, setelite, gps, tv, ultra sound, x-rays, gamma rays etc...naamini unazijua faida zake.....
..ila mawimbi haya ya sasa ni level ya juu kabisa....yanaelezea phenomena ya muungano kati ya stars, black holes na mwanzo wa kitu kipya baada ya muungano huo. Hii teknologia wanataka wa improve kujua au ku prove mwanzo wa yote haya yaliyopo ulimwenguni....the big bang theory.
 
mxyo 16
Nimesoma mahali ugunduzi huu utawezesha kuona mwanzo ulimwengu ulivyokuwa (big bang) kwa kufuatia ripples za edge ya universe
 
Back
Top Bottom