Physics na IS zipewe kipaumbele

Equitable

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2021
Posts
2,124
Reaction score
5,698
Tanzania ya sasa inaitwa ya viwanda. Somo la physics limeachwa na serikali hailiangalii kwa jicho kali.

Wakati nasoma mimi somo hili halikuwa na walimu wa kutosha. Advance mwalimu mmoja alizunguka shule zaidi ya tatu kufundisha.

Nimesikitika leo kijana wangu ananipigia simu akinijulisha kuwa shuleni hakuna mwalimu wa somo hili.

Somo hili halikuwekwa hata kwenye BRN ya Kikwete sijui ni makusudi au kusahau.

Bila physics na computer science(IS) Viwanda vitaendeshwaje?
Naiomba sana serikali

1. Itilie mkazo masomo ya sayansi kwa maendeleo ya taifa.

2. Ada ya chuo kikuu kwa sayansi ni x2 ya masomo ya art. Serikali iangalie namna ya kulevel. Kutoa 100% ya mikopo hakusaidii watu hawa maana wakija kitaa wanakatwa na bodi mpaka wanastaafu.

Serikali sikivu itasikiliza.
 
Tanzania ya viwanda iliisha kabla ya mendazake kurudisha namba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…