Philipo Mwakibinga wa WARAMI awajibu maaskofu wa KKKT; adai wanatumiwa na CHADEMA

Philipo Mwakibinga, (sijajua anatoka taasisi gani) amewajibu Maaskofu wa KKKT juu ya waraka waliotoa huku akiwatuhumu kutumwa na CHADEMA.

Amesema waraka huo waliutoa siku moja baada ya waraka wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kutoa waraka wake na kusema ulianza kuasambazwa na Godbless Lema.

Pia waraka huo umefanana kwa mambo mengi na waraka uliotolewa na Freeman Mbowe na kusema waraka huo utakua umeandaliwa na CHADEMA ila Maaskofu walitia saini tu.

Pia amesema maaskofu hao walitakiwa kuelezea mambo wanayofanya kutokana na michango na misamaha ya kodi wanayopata na sio kutoa waraka wa kuikosoa Serikali pekee.

Huyo mangi shoo mmachame amegeuza Kkkt branch ya chadema. War aka wa maaskofu wa Kkkt umebeba umbra name uongo wrote kwenye propaganda za chadema. Kwa mfano uzushi kuhusu miilii inayookotwa coco beach. Serikali imetoa taarifa kwamba hao so watanzania name hakuna mwili wowote umehusishwa au kudaiwa no wa mtanzania. Serikali ambayo imefanya makubwa kupambana na ufisadi na uzembe na kufanya mambo makubwa kuhusu maendeleo haikosi maadui ambao mmojawapo no askofu shoo akiwa amejificha kwenye JoJo lake LA kanisa.
 
MBINU ZENU ZOTE MNAZOTUMIA TUMESHAZIJUWA MTAHANGAIKA SANA LAKINI HAMTAWEZA. AWAMU HII UJINGA WENU WOTE UMEKWAMA NA HAO MNAOWATUMA KUFARAKANISHA SERIKALI NA WANAINCHI TUTAWAKABILI KISAWASAWA
Yes hii nzuri tena kama hawa maaskofuuuuuzi ndio tutawalisha sakramenti zoteeee hadi ziishe ndio watajua kwann walitekwa kutoka kanisani hadi kwenda kuhubiri siasa za cdm makanisani
 
Mwakibinga uliisumbua sana Serikali ya Kikwete enzi zako ukiwa UDOM! Lakini maisha yamefanya ccm ukutie nyavuni kweli maisha haya jamani!!!!! Hahahahahahaaa! Kwa wanaomjua huyu jamaaa alikuwa kiboko ya utawala wa UDOM Na hadi sasa jina hilo likitajwa lazima Wakubwa wote waliohudumukwenye serikali ya Kikwete watafahamu vema
 
Je ule waraka wa baraza la maaskofu Tanzania (TEC) wametumwa na chama gani? Kwani una tofauti gani kimaudhui na huu wa maaskofu wa KKKT? Naanza kuamini kuwa JF inaanza kuvamiwa na vilaza na mashabiki wa kisiasa.
vilaza wa uvccm haswa
 
*WATETEZI WA RASILIMALI WASIO NA MIPAKA*

(WARAMI)

TAARIFA KUHUSIANA NA WARAKA WA MAASKOFU KKKT


JANA tuliona katika mitandao ya kijamii waraka wa viongozi wetu wa dini,ukizungumzia masuala mbali mbali ya nchi na mwelekeo wake huku sehemu kubwa ya waraka huo ukijikita katika kuikosoa serikali juu ya namna inavyoendeshwa.

Tunafahamu viongozi wa dini wana wajibu wa kiutumishi katika jamii huku wakilinda dhamira yao ya kuhakikisha umoja wa nchi yetu unabaki kuwa salama kwa namna yoyote ile.

Inapotokea mazingira yoyote ya viongozi wetu wa dini kushindwa kusimamia wajibu huo jamii inayoongozwa na viongozi hao inapaswa ijisimamie yenyewe na kuwakumbusha wajibu wao huo

Sisi Watetezi wa Rasiliamli wasio na mipaka (WARAMI) tunaamini kuwa moja wa wajibu wetu ni kuhakikisha Jamii inapatiwa haki hiyo pasipo upendeleo wa aina yoyote ule wa kiimani, kisiasa kanda au hata kiukabila

Kwa vyovyote vile tunaona ni sahihi kwa sasa nasi kupaza sauti yetu kwa jamii ili pamoja na viongozi wetu hawa wa dini wakiwemo maaskofu wa *KKKT* tuone ni namna gani bora ya kuishi katika jamii ambamo watu wake wamechanganyika kwa utofauti tofauti baina ya dini, kabila, jinsia, ufuasi wa kiitikadi na kadharika
Tunatumia nafasi hii kuwakumbusha viongozi wetu wa dini wajitafakari kwa umakini na kuanza kuchagua aina ya maneno ama kauli sambamba na njia wanazotumia ili kutokuleta taharuki kwa jamii hasa wakizingatia ukweli kwamba mara nyingi sio kila maoni wanayoona wao yanafaa basi kwetu sisi waumini wao pia yanafaa kwa maana tuyafuate kama yalivyo.

Miongoni mwa masuala yaliyoandikwa katika waraka ule wa maaskofu wetu ni malalamiko kuhusu *Katiba Mpya, Uhuru wa kutoa maoni, Usawa katika elimu, mauaji ya watu, uchumi Demokrasi,kodi kwa wafanyabiashara na ajira kwa vijana kwa kuyataja kwa uchache.*

*WARAMI*, *Tunashangaa ni kwanini waraka huu wa salamu za PASAKA haukujikita zaidi katika kuwasisitiza waumini wake kujikita katika kuabudu, kumnyenyekea Mungu, kusoma bibilia na maandiko mengine ya dini na badala yake wakajikita katika maoni yanayong’ata na kupuliza*

Watanzania wote ni mashahidi kuwa kwa sasa nchi yetu imejitanabaisha katika kutatua changamoto zilizokuwa zinaimbwa kila siku na wanasiasa hasa wa upinzani na kwa kweli tumeanza kuyaona matunda ya serikali kujikita katika kutatua changamoto hizo

Sote ni mashahidi kuwa Kuilazimisha Serikali kuitisha mchakato upya wa katiba ni jambo ambalo haliingii akilini kwa sasa kutokana na ukweli kwamba ni wanasiasa wenyewe hususan wa vyama vya upinzani ndio waliosusia na kukwamisha mchakato wa katiba kwa kutaka kulazimisha mawazo yao yawe bila kuzingatia msingi mama wa Demokrasia kuwa wachache wanasikilizwa wengi wanashinda.

Maaskofu wetu wamekazana kulalama kuhusu katiba mpya huku waumini wake wanaotuongoza hawana ufahamu kuhusu BIBILIA

Aidha, tumeona hivi karibuni namna Rais wa nchi alivyozungumza na jumuiya ya wafanyabiashara na kuweka wazi changamoto zote zinazowakabili wafanyabiashara ikiwemo suala la kodi na kuweka mkakati wa pamoja kulitatua, sasa kuendelea kulalamika kwenye hili hakuna tofauti na nongwa kwa kuwa hata muda alioutoa Rais kwa watendaji wake haujakwisha.

maaskofu wetu wamezungumzia kuhusu utekwaji na mauaji ikiwemo utiaji wa hofu lakini hawajajikita kuelezea kwa kina hasa ni yepi?,

sisi tunafahamu kuwa wapo watu walioathirika moja kwa moja na matukio ya kutekwa na kuteswa kwa vijana kama *Mussa tesha wa Igunga, Joseph yona wa Temeke, Halidi Kagenzi wa CHADEMA* na wengineo yalipaswa kukemewa tangu siku ya kwanza ya kutokea kwake na si kuyasubiri mpaka leo.

Tunawashangaa maaskofu wetu hawa kusema kuhusu usawa wa elimu huku wakifahamu kuwa wanamiliki chuo kikuu ambacho hivi karibuni kilipandisha ada ya masomo na Askofu mkuu alipoombwa kushusha ada akamwamuru mlinzi afungue geti na anayetaka alipe asome asiyetaka mlango uko wazi atoke, nafikiri Usawa wa elimu ulipaswa kuanza katika chuo kinachomilikiwa na *KKKT* na si vinginevyo.

Maaskofu wetu wanajaribu kutuaminisha kwamba wao ni wasafi na kila wanachozungumza ni sahihi je wanadhani wapo wasafi kiasi cha kuwa tayari kuchunguzwa na kuwekwa hadharani kuhusu Uhalali wa makanisa yao?.

Je maaskofu wetu hawa ni wasafi kiasi cha kuwa tayari kuchunguzwa matumizi ya mabilioni ya sadaka wanayokusanya kila siku?.

Ama maaskofu hawa wanaweza kuueleza umma kuhusiana matumizi ya misaada, misamaha ya kodi wanayopaswa kulipa na matumizi ya kodi hizo walizosamehewa na serikali.

*MAASKOFU WETU WANATUMIKA?*

Hatutaki kuamini kwamba viongozi wetu hawa wanatumika na wanasiasa kwa maslahi yao ama ya wanasiasa lakini nafikiri tunapaswa kufikiri sawa kwenye hili kwa kujijibu maswali machache yafuatayo?

1. Ikiwa waraka huu wa Maaskofu wetu umesainiwa tarehe 15-03-2018, kwanini umetoka leo na si kipindi ulipoandaliwa ama siku ya ibada kama inavyokuwa kawaida ya siku nyingine?


2. Kwanini waraka huu umetolewa siku moja baada ya waraka wa *Mwenyekiti wa CHADEMA Mheshimiwa Freeman Mbowe* ambao kimsingi maudhui yanafanana kiasi cha kutia shaka kuwa umeandaliwa na mtu mmoja na maaskofu kushirikishwa kuweka majina yao tu?

3.Kwanini waraka huu wa Maaskofu umesambazwa kwa mara ya kwanza na kiongozi wa CHADEMA ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu wa chama hicho mheshimiwa LEMA ambaye ndiye aliusambaza Waraka wa Mbowe katika muda unaofanana na njia zinazofanana?.

Ukijijibu maswali hayo hapo juu unaweza kupata picha halisi

*WITO*

1.Tunatoa wito kwa Maaskofu wetu kujikita katika masuala mahsusi yanayohusu Dini, watuelimishe kwenye dini, wamuachie Kaisari yaliyo yake nay a Mungu yaliyo yake

2.Tunawaomba maaskofu wetu wachague njia sahihi ya kupita kama walivyofanya wenzao waliowatangulia. Wapo viongozi wa dini walipoona wana wito wa kushiriki Siasa waliamua kuachana Upadri na Uaskofu na kujikita kwenye siasa

MWISHO.
Tunaamini kuwa kila jamii ina utaratibu wake wa kujiongoza (DEMOKRASIA), ndio maana Demokrasia ya Waislam inawataka wawe na Mufti ambaye wala hachguliwi na waislam wote lakini hueshimiwa na kila muislam, Wakatoriki wao wanaongozwa na PAPA ambaye wala hachaguliwi na wakatoliki wote lakini kila mkatoriki anamuheshimu na kumuamini. Mifano ya hivyo ni mingi nasi hatuna budi *kuiheshimu demokrasia yetu tunayoiishi*.

Wasalaam

*Philipo Mwakibinga* *Mkurugenzi wa Utafiti WARAMI*
0758910403
mwakibingapj@gmail.com
 
Philipo Mwakibinga, (sijajua anatoka taasisi gani) amewajibu Maaskofu wa KKKT juu ya waraka waliotoa huku akiwatuhumu kutumwa na CHADEMA.

Amesema waraka huo waliutoa siku moja baada ya waraka wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kutoa waraka wake na kusema ulianza kuasambazwa na Godbless Lema.

Pia waraka huo umefanana kwa mambo mengi na waraka uliotolewa na Freeman Mbowe na kusema waraka huo utakua umeandaliwa na CHADEMA ila Maaskofu walitia saini tu.

Pia amesema maaskofu hao walitakiwa kuelezea mambo wanayofanya kutokana na michango na misamaha ya kodi wanayopata na sio kutoa waraka wa kuikosoa Serikali pekee.


Hoja dhaifu mno ya kusema wanatumika, kama sio hoja ya kijinga!!! Kuna ya kuchukua na ya kuacha kama yapo!!!
 
Hakuna anaekatazwa kutoa maoni lakini kwann ni maaskofu wenye asili ya kaskazini tu?? Ndio wengi?? Tena dhehebu flan tu?? Na maoni yao ni ya kichonganishi ila Rais magufuli mpole sana ndio maana hawa watumikaji hawaachi kujitoa ufahamu.

..cha msingi ni uzito wa madai yao.

..hatupaswi kuangalia wanatokea wapi hapa Tz.
 
Hoja dhaifu mno ya kusema wanatumika, kama sio hoja ya kijinga!!! Kuna ya kuchukua na ya kuacha kama yapo!!!

Kwenye ishu ya "matumizi ya sadaka", mimi nimemshangaa kidogo kwani si ajabu hata yeye huenda kanisani na kutoa "sadaka" yake... Nadhani hata kwenye ibada za waislamu kuna sadaka pia.... Hata kama anaabudu Ng'ombe ama mti ama mizimu yake lazima huitolea sadaka !!

Sasa swali la kujiuliza ni, yeye huyu Mwakimbinga huwa anatoa sadaka yake kumpa nani na kwa lengo gani? Na kwanini asiulize matumizi ya sadaka yake hukohuko kanisani kwake anakoitolea ??
 
Philipo Mwakibinga, (sijajua anatoka taasisi gani) amewajibu Maaskofu wa KKKT juu ya waraka waliotoa huku akiwatuhumu kutumwa na CHADEMA.

Amesema waraka huo waliutoa siku moja baada ya waraka wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kutoa waraka wake na kusema ulianza kuasambazwa na Godbless Lema.

Pia waraka huo umefanana kwa mambo mengi na waraka uliotolewa na Freeman Mbowe na kusema waraka huo utakua umeandaliwa na CHADEMA ila Maaskofu walitia saini tu.

Pia amesema maaskofu hao walitakiwa kuelezea mambo wanayofanya kutokana na michango na misamaha ya kodi wanayopata na sio kutoa waraka wa kuikosoa Serikali pekee.

Si vizuri Mkuu kulikashifu kanisa na Maaskofu. Hicho ni kiburi cha uzima;

Ninyi ndio ambao mkiwa wazima huwa mnapinga uwepo wa Mungu kwa kusema Mungu hayupo.

Ila pale mnapougua na kukaribia kufa,haraka hukimbilia kanisa na kutubu,huku mkiomba kwamba nikifa naomba nizikwe na kanisa.

Nakushauri mkuu;usitukane kanisa na Maaskofu kwani hao mtu akifa ndio wanaoongoza ibaada za kuwaombea na kuwazika!!!!!
 
NAONA MSEMAJI MPYA WA SERIKALI BAADA YA JERRY MURO NA MUSIBA... HUYU AKISHALIPWA BUKU SABA ATALETWA MWINGINE AJIBU WARAKA MWINGINE...........................
 
..cha msingi ni uzito wa madai yao.

..hatupaswi kuangalia wanatokea wapi hapa Tz.

Kwanza KKKT na makanisa mengine hususani RC ni kawaida kutoa waraka maalumu kwa waumini wote kila mwaka kila majira ya sikukuu za Pasaka na Noel (Christmas)

Mimi ni m KKKT, tayari ulishafika huku (Shinyanga) kwetu kitambo na unasomwa kama matangazo ya kawaida mfululizo kuanzia jumapili ya leo 25/3/2018 na ile ya pasaka yenyewe 30/3/2018 na kwa kifupi ndiyo ujumbe wa pasaka kwa maumini wote mwaka huu !!

Sasa sijui watasambaza maaskari ktk kila kanisa siku hiyo kuanzia vijijini hadi mijini ili kuzuiwa kutosomwa ama "kamati za ulinzi na usalama" za maeneo husika zitaagizwa kukusanya makaratasi yote ?
 
Kimsingi, ujumbe huu wa wa Maaskofu mimi naona hauna jipya na kwa mtu yeyote mwenye akili timamu kabisa hawezi kudhani kuwa ni ujumbe muhimu kwa sasa.
Maaskofu waache kutumiwa na WANASIASA. Nyaraka kama hizi ni kujaribu kuwafitinisha wabanchi na serikali yao.
Huu ni UBOVU kuliko UBOVU wenyewe.
Takribani 90% ya ujumbe huu wameongelea mambo ya SIASA.
Kuna mazuri mangapi yaliyofanywa na serikali ya awamu hii ya tano?
Kama hawa wanaojiita Maaskofu ni wapenda haki, kwa nini basi wasingetaja angalau hata MAZURI mache tu yaliyofanywa na serikali ya awamu hii ya tano?
Huu ni UBOVU kuliko UBOVU wenyewe.
Magufuli piga kazi, usitishike na matamko yanayokuja dhidi ya serikali yako.
Hawa hawa kwenye mgao wa fedha za KIFISADI za ESCROW walikuwemo na waligawiwa.

Mkuu hebu taja hayo mazuri ya serekali mpaka hao maaskofu wasithubutu kuongelea madhaifu yaliyopo.
 
Nadhani tuwe tunajadili mambo ya maana yanayotolewa na watu ambao tjlunajua wapo.sawasawa. Sasa ukimsikiliza mtu kama huyu unaona kabisa, hata kuongea tu anatumia nguvu nyingi sana lakini ni dhahiri ndani ya kichwa hakuna nguvu inayofanana na nguvu ya mwili.
He is out of point completely ajibu hoja mojamoja
 
MBINU ZENU ZOTE MNAZOTUMIA TUMESHAZIJUWA MTAHANGAIKA SANA LAKINI HAMTAWEZA. AWAMU HII UJINGA WENU WOTE UMEKWAMA NA HAO MNAOWATUMA KUFARAKANISHA SERIKALI NA WANAINCHI TUTAWAKABILI KISAWASAWA

Kwa SMG au kwa kuwateka?
 
Back
Top Bottom