Traxtion
JF-Expert Member
- Dec 10, 2021
- 5,896
- 11,792
Peugeot ni kampuni ya Kifaransa inayodili na utengenezaji wa magari ya umeme. Kwenye picha ni gari aina ya Peugeot e 3008 New Model (2024)
SPECIFICATIONS ZAKE 👇👇
Dimensions: 4,542 mm x 1,895 mm x 1,641 mm, 2,739 mm wheelbase.
Drivetrain tested: 73 kWh FWD - FWD 157 kW (210 hp), 343 Nm, 73 kWh total battery capacity, 71 kWh usable battery capacity
Other drivetrains: Dual-motor AWD - AWD 240 kW (320 hp), 509 Nm, 73 kWh total battery capacity, 71 kWh usable battery capacity
Charging: 160 kW CCS
Range: 524 km WLTP
Weight: 2,108 kg unladen, 2,640 kg gross
Other features: Heated, ventilated and massaging seats, OTA updates.
Gari hili lina muundo mzuri sana, mfano kwenye picha angalia shape ya taa zake zipo kama alama za mikwaruzo ya kucha za tiger au simba.
Kwa mbele hapa utaona logo ya kampuni hiyo ya Peugeot
Ukiliangalia kwa pembeni lina mwonekano kama magari mengi ya umeme sasahivi, isipokuwa nyuma lina mwonekano wa kitofauti kidogo
Kwa nyuma gari lina mwonekano kama limedidimia hivi, hii inatokana na car top kushuka chini sana huku kwenye upande wa buti, maana yake ni kwamba hata space ya kuwekea mizigo itakuwa imepunguzwa ukubwa.
Lakini binafsi nimependa mwonekano wake
Design ya tairi ni ya kipekee pia, ni tofauti kidogo na magari mengi tuliyozoea kuyaona
Kwa ndani usukani wa gari ni mdogo kuliko magari mengi, lakini kuna mengi mazuri.
Kilichofanya niandike kuhusu gari hili ni design yake. Hili gari lina mwonekano mzuri na ukitaka kulijua vizuri ndani nje sima review yake hapa
Peugeot e-3008 GT Electric review
We review the Peugeot e-3008 GT Electric in the real world!
m.arenaev.com
Gari hili kwa Ulaya bei inarange TSh 130 millions hadi TSh 160 millions
Je ni gari gani umewahi kukubali design yake? Ikiwezekana weka na picha yake tuone
Mimi yapo mengi ila hilo ni moja wapo