Petro je wanipenda? Lisha kondoo wangu

Petro je wanipenda? Lisha kondoo wangu

Joseph Gadiel

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2022
Posts
448
Reaction score
765
Yohana 21 : 15
Walipokwisha kula, Yesu akamuuliza Simoni Petro, “Je, Simoni mwana wa Yohana, unanipenda kweli kuliko hawa?” Yeye akamjibu, “Ndiyo Bwana, wewe unajua ya kuwa ninakupenda.” Yesu akamwambia, “Lisha wana-kondoo wangu.” Yesu akamuuliza tena, “Simoni, mwana wa Yohana, wanipenda?” Petro akamjibu, “Ndiyo Bwana, wewe unajua ya kuwa ninakupenda.” Yesu akamwambia, “Chunga kondoo wangu.” Kwa mara ya tatu Yesu akamuuliza Petro, “Simoni mwana wa Yohana, unanipenda?” Petro akahuzunika sana kwa kuwa Yesu alimuuliza mara ya tatu, “Unanipenda?” Akamjibu, “Bwana, wewe unajua yote, unajua ya kuwa ninakupenda.” Yesu akamwambia, “Lisha kondoo wangu.
 
Ndio Papa wa kwanza.

Yesu Kristo aliyembadilishia jina akamuita Kefa (kwa Kiaramu "mwamba", jina ambalo lilitafsiriwa kwa Kigiriki Petros na kwa Kilatini Petrus).

Ndio maana hapo unaona anaulizwa Simon. Alaf Biblia inasema Petro akajibu.

Najua KOBAZ hawachelewi kuja kusema Biblia inakinzana. Kumbe wenyewe ndio hawaelewi.
 
Wapi waliandika kuwa ni papa wa kwanza??

Wakati petro hakuwahi kajanga italy
 
Wewe ndiye Petro, Na juu ya Jiwe hili nitalijenga Kanisa langu.
Juu ya mwamba huu.
Perro sie mwamba aliekuwa anazungumzia yesu.
Maana petro alimkana yesu mara tatu, yesu hawezi jenga kanisa lake juu ya mtuu.

Mwamba ulikuwa ninnini??

Juu ya ufunuo, mungu kukufunulia jambo usilolifahamu. Hakika mwili na nyama hazijakufunulia haya ila baba yangu alieko mbinguni,na juu ya mwamba huu.

Hakuwa anaongelea habari za petro,ila mungu kufunua jambo ndani yako. Kukupa jibu ndani yako.
Kukuongoza
 
Hakika nimefunuliwa na YESU kupitia ww
 
Back
Top Bottom