PETITION: Tanzanians deserve WHOLE truth about Standard Bank

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
David Green QC
Director
Serious Fraud Office
2-4 Cockspur Street
London SW1Y 5BS


Dear David Green
We are writing to urge you to reopen the investigation into Standard Bank and its role in alleged bribery relating to a $600 million bond for our country, Tanzania. Corruption has caused enormous problems for our citizens in Tanzania, and we need to know that the perpetrators of corruption are going to be brought to justice. We deserve to know the full truth about corruption that affects our country.

The $600 million bond that Standard Bank raised for the government of Tanzania has saddled our country with a significant debt. There have been suggestions that the bond, the mandate for which was given to Standard Bank without any competitive bidding, was not a good deal for Tanzania and that we are paying a significantly higher interest rate than we might otherwise have done with a more competitive bond. There has been little transparency over what the money raised by the bond was used for and whether it was used for the public good or for the private gain of government officials.

We are deeply concerned at recent claims made by one of Standard Bank’s employees in Tanzania who is alleged by Standard Bank and your office to have committed bribery, that Standard Bank misrepresented the truth and suppressed material facts about its involvement in order to get the Deferred Prosecution Agreement that your office offered it and that was approved by a Judge in December 2015.

We would like to see all those involved in this corruption scandal that has tainted our country brought to justice. We are pleased that the SFO has said it will assist the Tanzanian authorities to bring those involved in Tanzania to justice. But we are concerned that the full truth of whether individuals in the UK were complicit in the corruption has not been established because the SFO did not complete its investigation into the allegations.

In particular, the SFO did not seek to establish independently from the company, for instance by interviewing those alleged to have paid the bribes, whether the UK employees’ version of events was correct. By relying on the company’s version of events, and by forestalling its investigation, the SFO has denied the public of Tanzania the full story of how this corruption was committed.
This is not the first time that the SFO has entered into an agreement with a company in relation to corruption in Tanzania that has left us with a bitter taste in our mouth.

In 2010, the settlement with BAE Systems over alleged corruption in a radar deal left many Tanzanians feeling that the war on corruption is merely words. Those in the UK who commit or are complicit in corruption appear to us untouchable.

We are also concerned in this case that the compensation offered does not reflect the harm caused by the alleged corruption. It doesn’t appear that the SFO put any expert evidence to the court about the opportunity cost that was lost by our country by not pursuing other more favourable options for instance through competitive bidding. The bribes allegedly paid by Standard Bank’s subsidiary were paid in order to close off other options on the table.

We urge you to place this letter and the court documents from Tanzania that allege that Standard Bank suppressed material facts in order to get a Deferred Prosecution Agreement before Justice Leveson.

Yours sincerely

SIGN HERE
 
Charity begins at home. What about Escow money lol

Standard Bank wachunguzwe Kwa rushwa Hati Fungani ya USD 600m Kwa Tanzania
Deni la Taifa la Tanzania sasa ni USD 15 bilioni ( tshs 30 trilioni).

Kutokana na ukubwa wa deni hilo, Tanzania hulipa Huduma ya Deni la Taifa takribani tshs 2.2 trilioni kila mwaka. Bajeti ya kuhudumia Deni la Taifa ni kubwa zaidi kuliko bajeti ya Wizara yeyote nchini Tanzania.

Hata hivyo katika Madeni hayo kuna ambayo yamepatikana Kwa rushwa na mengine yamechukuliwa Kwa matumizi ya anasa tu. Kitaalam Madeni haya yanaitwa ' odious debts '. Moja ya Deni la hovyo ni USD 600m ambalo Tanzania ilikopa kutoka Benki ya Standard ya Uingereza kupitia Hati Fungani.

Taasisi ya SFO ya Uingereza inayoshughulika na rushwa kubwa imeonyesha kuwa mkopo huu ulipatikana Kwa rushwa.

Taasisi ya Corruption Watch ya UK imeonyesha kuwa Tanzania imepata hasara ya takribani USD 80 milioni ( tshs 160 bilioni ) Kwa kuchukua mkopo huu. Hata hivyo uchunguzi wa SFO haukuhusisha maofisa wa juu wa Standard Bank makao makuu na hivyo kufunika kombe mwanaharamu apite.

Iwapo uchunguzi ungegundua kuwa Standard Bank walihusika moja Kwa moja na Hongo hii, Tanzania ingefutiwa deni lote na kuokoa fedha nyingi sana ambazo zingewekezwa kwenye sekta za elimu, afya na Maji.

Tunataka Benki ya Standard ya Uingereza ichunguzwe upya na SFO kuhusu tuhuma za rushwa ili kupata biashara Tanzania ( Hati Fungani USD 600m ).

Unataka kujua ukweli wote kuhusu ufisadi wa Hati Fungani ulioliingizia Taifa deni la USD 600 milioni ( tshs 1.2 trilioni )?

Saini petition hii ili taasisi ya Rushwa kubwa ( FSO ) ya Uingereza ifungue upya uchunguzi kwa kuzingatia ushahidi mpya kuwa mabosi wa Benki ya Standard ya Uingereza walihusika na mipango ya kutoa hongo ili kupata biashara Tanzania.

Ikigundulika kuwa mabosi hawa walishiriki maana yake Tanzania itafutiwa deni lote kwa sababu benki hiyo itawajibika kurudisha fedha za watu kwani Hati fungani itaonekana ni batili.

Tanzania inaanza kulipa deni hilo kuanzia mwezi Aprili, 2016 kama tusipohakikisha tunazuia Kwa kupitia petition hii. Iwapo deni hili litalipwa juhudi za Rais John Magufuli kupata mapato zitaathiriwa na sekta nyeti kama elimu, afya na Maji zitakosa bajeti ya kutosha.

Mkopo uliopatikana Kwa rushwa sio halali.
Ewe Mtanzania ungana na Watanzania wenzako duniani kutaka SFO ifungue uchunguzi kwa kuzingatia ushahidi mpya dhidi ya Benki ya Standard ambayo sasa inaitwa ICBC plc
Petition hii imeletwa kwenu na Jumuiya ya Watanzania wanaoishi ughaibuni.
 
Vipi kuhusu taasisi zetu :pccb,
Standard Bank wachunguzwe Kwa rushwa Hati Fungani ya USD 600m Kwa Tanzania
Deni la Taifa la Tanzania sasa ni USD 15 bilioni ( tshs 30 trilioni). Kutokana na ukubwa wa deni hilo, Tanzania hulipa Huduma ya Deni la Taifa takribani tshs 2.2 trilioni kila mwaka. Bajeti ya kuhudumia Deni la Taifa ni kubwa zaidi kuliko bajeti ya Wizara yeyote nchini Tanzania.
Hata hivyo katika Madeni hayo kuna ambayo yamepatikana Kwa rushwa na mengine yamechukuliwa Kwa matumizi ya anasa tu. Kitaalam Madeni haya yanaitwa ' odious debts '. Moja ya Deni la hovyo ni USD 600m ambalo Tanzania ilikopa kutoka Benki ya Standard ya Uingereza kupitia Hati Fungani. Taasisi ya SFO ya Uingereza inayoshughulika na rushwa kubwa imeonyesha kuwa mkopo huu ulipatikana Kwa rushwa. Taasisi ya Corruption Watch ya UK imeonyesha kuwa Tanzania imepata hasara ya takribani USD 80 milioni ( tshs 160 bilioni ) Kwa kuchukua mkopo huu. Hata hivyo uchunguzi wa SFO haukuhusisha maofisa wa juu wa Standard Bank makao makuu na hivyo kufunika kombe mwanaharamu apite. Iwapo uchunguzi ungegundua kuwa Standard Bank walihusika moja Kwa moja na Hongo hii, Tanzania ingefutiwa deni lote na kuokoa fedha nyingi sana ambazo zingewekezwa kwenye sekta za elimu, afya na Maji.
Tunataka Benki ya Standard ya Uingereza ichunguzwe upya na SFO kuhusu tuhuma za rushwa ili kupata biashara Tanzania ( Hati Fungani USD 600m ).
Unataka kujua ukweli wote kuhusu ufisadi wa Hati Fungani ulioliingizia Taifa deni la USD 600 milioni ( tshs 1.2 trilioni )?
Saini petition hii ili taasisi ya Rushwa kubwa ( FSO ) ya Uingereza ifungue upya uchunguzi kwa kuzingatia ushahidi mpya kuwa mabosi wa Benki ya Standard ya Uingereza walihusika na mipango ya kutoa hongo ili kupata biashara Tanzania. Ikigundulika kuwa mabosi hawa walishiriki maana yake Tanzania itafutiwa deni lote kwa sababu benki hiyo itawajibika kurudisha fedha za watu kwani Hati fungani itaonekana ni batili. Tanzania inaanza kulipa deni hilo kuanzia mwezi Aprili, 2016 kama tusipohakikisha tunazuia Kwa kupitia petition hii. Iwapo deni hili litalipwa juhudi za Rais John Magufuli kupata mapato zitaathiriwa na sekta nyeti kama elimu, afya na Maji zitakosa bajeti ya kutosha.
Mkopo uliopatikana Kwa rushwa sio halali.
Ewe Mtanzania ungana na Watanzania wenzako duniani kutaka SFO ifungue uchunguzi kwa kuzingatia ushahidi mpya dhidi ya Benki ya Standard ambayo sasa inaitwa ICBC plc
Petition hii imeletwa kwenu na Jumuiya ya Watanzania wanaoishi ughaibuni.
Bofya hapo chini kuweka saini yako. Tetea Tanzania yako. Uzalendo wako ndio uhai wa Tanzania yako.
David Green Director Serious Fraud Office UK: Petithttps://www.change.org/p/david-green-director-serious-fraud-office-uk-petition-to-reopen-investigation-into-standard-bank-s-alleged-bribery-in-tanzania?recruiter=80046040&utm_source=share_petition&utm_medium=copylinkion to reopen investigation into standard bank's...
Cag, ag, et cetera, wao wamekaa tu kusubiri posho na mishahara ninono, hawana la kufanya?
 
Hawa SFO wamehalalisha rrushwa kwa nchi masikini kama Tanzania. Wao wanafanya uchunguzi just for the interest of UK tuu ambaye ndie mhongaji kwa kuyakubalia makampuni haya ya kibeberu, kuihonga SFO hongo nyingine halali kwa jina la faini, ambayo italipwa na makampuni haya ili yaruhusiwe kufanya non disclosure zile fedha za hongo (kick backs) zimelipwa kwenye accont za kina nani, kwa lengo la just to save the faces of African top leaders ili hivi masikini viendelee kuzipa biashara kampuni hizi za kibeberu, lakini sio yule aliyenyonywa kwa hongo hiyo ambayo ni nchi masikini kama Tanzania.

Ajenti wa ile Radar ya BAE ndio huyo huyo ajenti wa ndege ya rais ile Gulf Stream, baada ya Tanzania kuletewa infaleted rates za more than two times ya original price ya ile ndege, Mzee John Cheyo, alipiga kelele na kuonyesha real price kwenye wmba masikioni na kuelezwa kuwa ikibidi watu kulaebsite ya BAE, lakini watu walitia pamba masikioni na kuambiwa ikibidi watu kula nyasi, na wale nyasi lakini ndege lazima inunuliwe!, hizo fedha za ziada zilielezwa ni agents commissions na retainer for after sales service, sasa kitu kama hiki kweli utaamini kuwa wakuu wetu kule top hawahusiki?!.

Tena agent huyo akaelezwa kuwa ni good family friend wa yule mpangaji wetu wa ile nyumba nyeupe, na kweli siku za sherry party ndie pekee huuhusiwa kuingiza gari yake, a red Ferrari ndani ya geti za nyumba ile na kuipaki pembeni ya garden ili kila mgeni aione na labda aulize ni gari ya nani, wakati mawaziri na mabalozi wanashushwa tuu na magari yao ndani kisha magari kutoka kwenda kupaki nje!.

Kama kule top hawahusiki, kweli baada ya uchunguzi wa SFO kufungwa kwa hongo ya halali iliyobatizwa jina la faini na change ya radar, nchi masikini tungeridhika na kukaa kimya tuu kwa kukubali kuwa yamekwisha, huku tukielewa wazi waliopokea hizo kickbacks ni watu wetu?!.

Hili la Stan Chart nalo litapita hivi hivi!, kama na wewe ni mwenzangu na mimi ambaye unaunga mkono Tanzania kuendelea kufanywa shamba la Bibi, ungana nasi kutia saini tamko hili, tukimaliza tutie saini ule uchunguzi wa radar ili kuwabaini ni kina nani ambao ndio mchwa wetu wanaolitafuna taifa letu, usikute ni kweli kikulacho kii nguoni mwako!.

Tusikubali!.

Pasco
 
Mimi hata kusaini sitosahini ,kuna hela walibeba kwenye sandarusi Stanbic na raisi wa nchi anakataa sio hela za wananchi wake ,Mabilioni ya uswiss yameishia wapi ?waendelee kula tu
 
from deepest part in my heart i swear to god ya kwamba nawachukia mafisadi wanaodidimiza uchumi wetu ila mungu atalipa tu siku moja wataomba ardhi ipasuke waingie.
 
Mkombozi Bank na Body yake imeshachukuliwa hatua gani mpaka sasa?
Kama inaruhusiwa hapa basi naomba kueleweshwa kwa wale wanaofuatilia.
 
Back
Top Bottom