Peter Msechu asema hajawahi kuona Watu ' Wanafiki ' na ' Wabinafsi ' duniani kama Watanzania

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,548
108,882
Akizungumza muda mfupi tu uliopita katika mahojiano na Kituo kimoja cha Television Msanii Peter Msechu amesema kwamba kama kuna kitu ambacho amejifunza kwa Watanzania basi ni tabia zao kubwa mbili ' pacha ' za Unafiki na Ubinafsi.

Alitolea mfano hai kwamba kuna siku moja aliwahi ' Kuposti ' Mtandaoni kuwaomba Watanzania wapakue Nyimbo zake na wampigie Kura lakini cha Kushangaza ndani ya Siku tatu alipata ' mrejesho ' wa Watu wasiozidi 25 tu lakini Kesho yake ' akaposti ' kuwa ameachana na Mkewe Mama Lolo cha kushangaza ndani ya dakika 10 alipokea sms zaidi ya 3200 za Watu huku wengine hata hawajui na wakijifanya kumpa ushauri na kumpoza na akashangaa mno kwamba iweje alipowataka wampe ' sapoti ' katika Kazi yake hawakumpa ' ushirikiano ' ila kwa mambo ya ' Kimbea ' ndipo wengi walijotokeza?

Nami nimuambie tu Peter Msechu kwamba nampa pole kubwa kwa kuchelewa Kwake kujua kwamba hakuna Watu ' Wanafiki ' na ' Wabinafsi ' duniani kama Watanzania na nadhani hicho ' Kipaji / Kipawa / Talanta ' pekee tuliyojaaliwa nayo Watanzania na kwakweli tunatendea haki kabisa.

Nawasilisha.
 
Yeye ndo mnafiki wa kwanza kisha wanafuata watanzania alafu mimi ndo wa mwisho.

Si aliiimbia CCM mbele kwa mbele mwaka 2015 acha sasa imlalie mbele. Leo bungeni nimeshangaa naibu spika kuizima hoja ya kuzifungia nyimbo zao sasa wapate akili sio 2020 wawatungie nyimbo mawe na kiranja wao wa kuzimu
 
Hivi watanzania waliopo mitandaoni wanawakilisha asilimia ngapi ya watanzania wote mpaka uwatukane na wale wa kwetu Ng'walugulu ?Mimi binafsi sijui hata wimbo mmoja wa huyo mtu na bado ananiita mnafiki, asitake kuwaweka watu katika kundi moja.
 
Akizungumza muda mfupi tu uliopita katika mahojiano na Kituo kimoja cha Television Msanii Peter Msechu amesema kwamba kama kuna kitu ambacho amejifunza kwa Watanzania basi ni tabia zao kubwa mbili ' pacha ' za Unafiki na Ubinafsi.

Alitolea mfano hai kwamba kuna siku moja aliwahi ' Kuposti ' Mtandaoni kuwaomba Watanzania wapakue Nyimbo zake na wampigie Kura lakini cha Kushangaza ndani ya Siku tatu alipata ' mrejesho ' wa Watu wasiozidi 25 tu lakini Kesho yake ' akaposti ' kuwa ameachana na Mkewe Mama Lolo cha kushangaza ndani ya dakika 10 alipokea sms zaidi ya 3200 za Watu huku wengine hata hawajui na wakijifanya kumpa ushauri na kumpoza na akashangaa mno kwamba iweje alipowataka wampe ' sapoti ' katika Kazi yake hawakumpa ' ushirikiano ' ila kwa mambo ya ' Kimbea ' ndipo wengi walijotokeza?

Nami nimuambie tu Peter Msechu kwamba nampa pole kubwa kwa kuchelewa Kwake kujua kwamba hakuna Watu ' Wanafiki ' na ' Wabinafsi ' duniani kama Watanzania na nadhani hicho ' Kipaji / Kipawa / Talanta ' pekee tuliyojaaliwa nayo Watanzania na kwakweli tunatendea haki kabisa.

Nawasilisha.

Mnafiki namba moja hapa Tz ni wewe mwenye 2&3 Dick Uchwara na Bashite 4 CCM yako wanafiki na kigeugeu
 
Back
Top Bottom