Peter Kibatala: Rasimu ya Warioba ni Sheria

Peter Kibatala: Rasimu ya Warioba ni Sheria

Wana-UKAWA kama majibu yenu ndio ninayoyaona hapa afadhali mlitoka Bungeni!
 
Wakuu,
Huwezi kuamini lakini ndivyo ilivyotokea Mahakama Kuu ambapo Wakili Peter Kibatala alipoiambia Mahakama hiyo kwamba eti Rasimu ya Warioba ni Sheria. Watu tulikuwa tunajiuliza kwa nini UKAWA walikuwa wanakomalia sana Rasimu ya Warioba kumbe wenzetu waliamini kwamba hiyo ni Sheria.

Hayo yako kwenye kesi ya Saed Kubenea v. Attorney General, Misc. Civil Cause No. 28 of 2014 katika ukurasa wa 9 tunapata haya yafuatayo:

It was Mr. Masaju’s further argument that the Draft Constitution has no legal force, that it is “a mere annex” to the Commission’s Report [relying on section 20 (1)] and can only serve as a “working document”. He wondered how could a document that is not part of the law be binding on the Constituent Assembly. Submitting on this point, Mr. Kibatala stated that the Draft Constitution was “law” and therefore binding.

Lakini Mahakama Kuu ilijibu katika ukurasa huo huo wa 9 kwa ujasiri kama ifuatavyo:

We would respectfully differ from both counsel on this point, though we differ more markedly from counsel for the petitioner’s position. We do not think that the Draft Constitution is law, as it has not been enacted into one.

Tunawashauri wana-UKAWA wakubali tu Hukumu ya Mahakama Kuu kwamba Rasimu ya Warioba ilikuwa sio Sheria bali ni "WORKING DOCUMENT" ili kutengeneza Katiba Mpya!

Pia Kibatala na usomi wake wote kuamini kwamba RASIMU YA WARIOBA ni SHERIA nalo linatupa mashaka sana na weledi wake!

Ni hayo tu kwa leo, karibuni kwa mjadala!

ndiyo ilikuwa sheria kwa sababu ilibeba maoni ya watz namna gani waongozwe na kuwadhibiti mafisadi. Lakn fisadi likakabidhiwa kuandika katiba na mafisadi menzie likatupilia mbali
 
Kwangu mimi naunga mkono hoja kwamba, katiba ya warioba ni sheria kuliko katiba pendekezwa. Sababu ni kwamba katiba pendekezwa imeandikwa na kina chenge mafisadi waliokubuhu. Wakati rasimu imeunganisha maoni ya watanzania juu ya katiba waitakayo!
 
Mkuu usitoe majibu mepesi kwa swali zito - Tiririka hapa thibitisha kwa vipi rasimu haina uhusiano na sheria au si sheria kabisa!
Unga hauwezi kuwa ugali mpaka hatua zote za kusonga ugali ziwe zimepitiwa!
 
Kwangu mimi naunga mkono hoja kwamba, katiba ya warioba ni sheria kuliko katiba pendekezwa. Sababu ni kwamba katiba pendekezwa imeandikwa na kina chenge mafisadi waliokubuhu. Wakati rasimu imeunganisha maoni ya watanzania juu ya katiba waitakayo!

Kwa hiyo Warioba kwa kukusanya maoni ndio alitunga Sheria tayari?
 
Unga hauwezi kuwa ugali mpaka hatua zote za kusonga ugali ziwe zimepitiwa!

Umeandika meengi mazuri
Lakini kwa mfano kama huu umejidhalilisha!
Nadhani ulimaanisha ugali hauwi ugali hadi hatua zote za kusaga unga na kusonga zikamilike!
Ukishasonga ugali hupati tena unga-labda kwenu!
Mie naendelea kuamini kwamba kwa BMK, Rasimu ya TUME ilikuwa ni sheria kuu
 
Hiyo "Sheria" ilitungwa na Warioba?
 
Umeandika meengi mazuri
Lakini kwa mfano kama huu umejidhalilisha!
Nadhani ulimaanisha ugali hauwi ugali hadi hatua zote za kusaga unga na kusonga zikamilike!
Ukishasonga ugali hupati tena unga-labda kwenu!
Mie naendelea kuamini kwamba kwa BMK, Rasimu ya TUME ilikuwa ni sheria kuu
Kwa hiyo kila unaposonga ugali lazima ukasage unga kwanza? Makubwa haya; anyway. Mzee Waryoba na team yake walikuwa wanaandaa tu rasimu ya katiba mpya. Kwa hivyo basi hii katiba (sheria mama) inayopendekezwa ni matokeo tu ya kazi akina Waryoba na mwisho wa siku baada ya wananchi kuikubali, ifikapo 2016 Tanzania itakuwa imepata katiba (sheria mama). Hata hivyo ni matumsini yangu kuwa wananchi wataikataa rasimu hii maana imeondoa mambo mengi ya msingi, muundo wa serikali.

Mungu ibariki Africa, Mungu ibariki Tanganyika.
 
Tanzania kila mwenye uwezo wa kutumia mtandao anakuwa msomi! Lahasha kutafsiri sheria ni zaid ya kuwa msomi.
Hiv tunaopiga upatu kuwa rasimu ya 3 ni nzur tumeangalia nin?,uzur wa katiba si uwingi wa mambo na si kusa kila jambo tu bali namna gani inawaelekeza viongoz miiko na maadili namna ya kufikia mambo hayo machache au mengi.katiba pendekez imekosa hofu ya viongozi kutoka kwa wananchi kwa maana hiyo tutegemee mabadiliko chanya kidogo au yasiwepo kabisa.
 
Unajua watanzania atuna uwezo wa kuongea yanayo tuuma nandio mahana tunaishia kurumba f nipese ngapi zimetumika kupata rasimu ya wananchi wakati hiliwezekana kabisa kuandikia bungeni hinamahanisha watanzani awana akiri turikuwa tunapimwa tuna nn kichwani lakini tayar tanzania himepata hufa kwajir ya masirai ya wachache katiba ni maliziano si malumbano ataww uliyeleta kamada haka hunaona unaweza lakini ujui niatari sana kuzarau wananchi watanzania mungu atusaidie,
 
Back
Top Bottom