Ukichepukia kwangu na lipete lako la ndoa, nakuvua kisha sikurudishii. Nikiona vinang'aa nawahi kwa sonara
inategemea na mtu aliyeivaa,kama ni mtu ambaye hawezi kufikiria mara mbili mbili kuhusiana na matendo yake na matokeo yake kwa mke/mume wake pete wala haiwezi kusaidia,ila kama ni mtu ambaye anakaa na kutafakari na kufikiria matendo yake yatakuwa na matokeo gani kwa mume/mke/familia yake wake yaweza kusidia sana kama ikitokea mtu kajisahau sana.
ulipotea ana mkuu ulikuwaga wapi?karibu tena Amavubi.
Amavubi pete ni kiashiria tuu cha ndoa (kwa mawazo yangu) uaminifu wa mtu hauko kwenye kuvaa pete unaweza ukavaa pete na ukawa mfagizi balaa pamoja na pete yako kidoleni
Uaminifu ni wamtu mwenyewe na sio kuvaa pete kunakoweza kukufanya uwe muaminifu
Na isitoshe pete inavulika unaivua unaweka mfukoni unaendelea na mambo yako au unatoka unaiacha ofcn unaenda kufanya yako na unairudia baadae. Wengine wakiwa wanajua wanaenda kufanya mambo yao wanazivua kabisa wala hazionekani
Ndo maana nasema uaminifu umo kwa mtu mwenyewe na sio pete
Ukichepukia kwangu na lipete lako la ndoa, nakuvua kisha sikurudishii. Nikiona vinang'aa nawahi kwa sonara
BLUE G nashukuru kunikumbuka nipo, nadhani pete mujarab ya ndoa inavaliwa moyoni na si kidoleni
Sana as wanawake wengi single wezi, wenye tamaa, wivu na mengineyo mengi. wanajua kuwa wamepata mtu aliye na majukumu sio wakuranda randa na watakaomchuma vizuri. so ni mume wa mtu kujiheshimu haswa akiivaa na asipoivaa pia.
pete n pambo sikuhz thaman yake imeisha
Ukichepukia kwangu na lipete lako la ndoa, nakuvua kisha sikurudishii. Nikiona vinang'aa nawahi kwa sonara
Haina mchango wowote, Uhaminifu, Kuheshimiana, Upendo, Kujali na nk, hayo ndo yenye mchango mkubwa kwa ndoa, siku hizi kutokana na mfumo wa kisasa na unaoleta mitafaruku kwa ndoa nyingi wamama/wababa baadhi walio kwa ndoa wanakosa furaha, upendo nk hivo wanatafakali wafanye nn kupata hivo vitu hata furaha ya unyumba, ndiposa baadhi ya manyang'au kugundua kuna wanandoa wanaotaabika na kutaka utulivu nayo uwasaka kwa lengo la kutaka kuwapoza.
Wezi wa ndoa (michepuko) ufuatilia sn vidole, na wengine baada ya kujua ni deal nao wanavaa pete hata kama hawajaolewa.
"Kaa chonjo"