Pesa zilizoachwa kwenye mifuko ya hifadhi na watumishi wenye vyeti feki ungependa zitumike kufanya?

Kiberiti Kidogo

JF-Expert Member
Jan 14, 2017
575
917
Naimani kabisa pesa zilizoachwa kwenye mifuko ya hifdhi ya jamii na watumishi wa umma ni nyingi sana. Je wewe binafsi kutokana na agizo la rais la watumishi kutopewa fedha hizo ungependa zifanye nini ili kulisaidia taifa warau kurudisha hasara iliyokula kutoka kwa watumishi hao?
 
Watu wamefundisha màprofesa na madaktari ambao wanakariri wana vyeti original afu unasema wametia hasara serikali!? Kweli!?

Kwani zile pesa za kagera wamefanyia kazi gani? Cha MTU mavi hakiliwagi! Kauli ya wengi ni kauli ya mungu...nung'uniko lao ni nung'uniko la mungu hii laana sharti imtafune mtu siku moja.

Escrow, Richmond n.k wanapeta tu mtaani.
 
MLETA MADA KATIKA MAISHA YAKO MOJA KUNA KITU UNATAKIWA KUJIFUNZA KINASEMA

"KNOWLEGE IS POWER "

HAPA NINA MAANA HAO HAO WATUMISHI MNAWAPONDA WANA VYETI KUMBUKA HUO SIO MWISHO WA MAISHA NA AJIRA.

HAPA NINA MAANA "KUTOKANA NA UZOEFU WA KAZI WALIOUPATA WAKIWA NDANI YA SERIKALI "WANA UWEZO WA KUOMBA KAZI PRIVATE NA WAKAAJIRIWA KWENYE MAKAMPUNI YA WATU BINAFSI.

NA MAISHA YAKAENDELEA
 
YAANI WEWE NDO KWELI UNAFIKIRIA NA KUSIKILIZIA KWA KUTUMIA MA☆☆..LIO(a.k.a.)Masaburi.NI WAPI RAIS AMESEMA WATUHUMIWA WA VYETI FAKE WASILIPWE MAFAO YAO.NA UNAPOSEMA WAFANYAKAZI WALIOKUWA NA VYETI WALITUIBIA SIO SAHIHI.WALIIBA KIVIPI WAKATI WALIKUWA WANAFANYA KAZI.KAMA MTU ALIAJIRIWA KAMA DRIVER NA ALIKUWA ANAMPELEKA BOSI WAKE KAZINI NA KUMRUDISHA SALAMA HOME KWA MIAKA 30, SASA HUYU ALIIBA KIVIPI ! KWA NINI UMNYIME MAFAO YAKE ? KUNA WAFANYAKAZI WENGINE WALIKUWA WAZURI SANA KWENYE NAFASI ZAO NA WALIKUWA WAKIPEWA MPAKA CREDIT YA KUWA WAFANYAKAZI BORA(INA MAANA WALIKUWA WANA-PERFORM VIZURI) KWA NINI HUYU UMNYIME MAFAO YAKE.MNYONGE MNYONGENIADHABU YAKE KESHAFUKUZWA KAZI)LAKINI HAKI YAKE MPENI(APEWE MAFAO YAKE YOTE).
 
Asiye na dhambi na awe wa kwanza kumpiga jiwe mwanamke huyu( maneno haya sio yangu nanyi mwajua).
Hoja yangu ni hii, hivi hawa wafanya maamuzi wana usafi kiasi gani kwenye maisha yao hata kuamua hivi.....
Pamoja na kughushi kwao vyeti ni lini mwajiri alilalamika kwamba utendaji wao wa kazi hauridhishi?
»»»si semi waendelee kuwa kazini LAKINI NIONAVYO WALISTAHILI KUPEWA HIZO PESA....kiukweli jasho lao lipo kwenye hizo pesa.
 
hivi tukisema tunavyovipenda vitakuwa kweli maana si alishasema huwa hapangiwi
 
Zikalipe madeni yao waliyokopa huko kwenye mabenki...zinazobakia rudisha hazina
 
Majibu yapo mengi. Ili kukupa jibu muafaka, inabidi ujuze wewe unauliza swali hili kama nani? DG kwenye mashirika ya pensheni, waziri wa fedha na mipango, Mh Dr Mkuu wa kaya au Bashite?
 
MLETA MADA KATIKA MAISHA YAKO MOJA KUNA KITU UNATAKIWA KUJIFUNZA KINASEMA

"KNOWLEGE IS POWER "

HAPA NINA MAANA HAO HAO WATUMISHI MNAWAPONDA WANA VYETI KUMBUKA HUO SIO MWISHO WA MAISHA NA AJIRA.

HAPA NINA MAANA "KUTOKANA NA UZOEFU WA KAZI WALIOUPATA WAKIWA NDANI YA SERIKALI "WANA UWEZO WA KUOMBA KAZI PRIVATE NA WAKAAJIRIWA KWENYE MAKAMPUNI YA WATU BINAFSI.

NA MAISHA YAKAENDELEA
Ni kweli wanaweza ila kikubwa na kinachouma ni mafao yao. Hawa wat pamoja na vyeti feki wametumikia serikali. Wamezalisha, mfano walimu, manesi, waganga, wahudumu maofisni nk. Hawa wote wamehudumu na tija imeonekana. Walizipa pengo na kubwa akiba yao imetumika serikalini kutengeneza shughuli mbalimbali . Akiba yao imekopwa na serikali na ktumika kujenga madaraja,vyuo vikuu , ofisi za serikali nk. Sasa serikali inapowatangazia kihama mie hapo sielewi.
 
Naimani kabisa pesa zilizoachwa kwenye mifuko ya hifdhi ya jamii na watumishi wa umma ni nyingi sana. Je wewe binafsi kutokana na agizo la rais la watumishi kutopewa fedha hizo ungependa zifanye nini ili kulisaidia taifa warau kurudisha hasara iliyokula kutoka kwa watumishi hao?
Hasara gani wewe. Hao wameleta maendeleo makubwa mno. Mbona mlikuwa mnajigamba kila mwaka eti nchi imepiga hatua kwenye sekta ya elimu na Afya.
 
Watu wamefundisha màprofesa na madaktari ambao wanakariri wana vyeti original afu unasema wametia hasara serikali!? Kweli!?

Kwani zile pesa za kagera wamefanyia kazi gani? Cha MTU mavi hakiliwagi! Kauli ya wengi ni kauli ya mungu...nung'uniko lao ni nung'uniko la mungu hii laana sharti imtafune mtu siku moja.

Escrow, Richmond n.k wanapeta tu mtaani.

Mwenye laana ni yupi...kati ya aliyemrubuni mwajiri wake kwa kumpa taarifa za uongo ili ajipatie ajira ambayo hana sifa nayo huku maelfu ya wenye sifa wakizurura mitaani....!??

Au mwajiri aliyegundua uongo wa mwajiriwa wake kwa kumpa sifa za uongo kuhusu elimu yake...hivyo kumkatishia ajira yake tena kwa huruma bila ya kumpeleka kwenye vyombo vya dola kwa kujipatia kazi kwa njia ya ulaghai....!!??

Ina maana siku hizi matapeli wanaweza wakawapa laana watu waliowatapeli baada ya kugundulika utapeli wao kwa kuwa kutapelj ni sehemu ya haki zao...!!??
 
Ni kweli wanaweza ila kikubwa na kinachouma ni mafao yao. Hawa wat pamoja na vyeti feki wametumikia serikali. Wamezalisha, mfano walimu, manesi, waganga, wahudumu maofisni nk. Hawa wote wamehudumu na tija imeonekana. Walizipa pengo na kubwa akiba yao imetumika serikalini kutengeneza shughuli mbalimbali . Akiba yao imekopwa na serikali na ktumika kujenga madaraja,vyuo vikuu , ofisi za serikali nk. Sasa serikali inapowatangazia kihama mie hapo sielewi.

Kwa mfano wewe siku ukigundua kuwa kijana wako uliyemuajiri amekuibia je utamuacha aendelee na ajira kwako kwa kuwa utendaji wake ulikuwa na tija kwako....!??
 
Nyie mnaowatetea waliofoji vyeti hamna maana kabisa. Unakuta MTU mmemaliza nae sec kafeli but mtu umekomaa na kusoma then after 1 year unakutana nae maisha mazur na vicheko juu wewe bado tu unahangaika na vitabu et nimuonee huruma??? Hapana aisee atumbuliwe tu na asipate chochote
 
Back
Top Bottom