Serikali iliyopo madarakani imekuwa ikijinasibu kuwa pamoja na mambo mengine imefanikiwa kutumbua majipu na hivyo kudhibiti mianya iliyokuwa ikipelekea upotevu wa mapato hasa mapato ya bandarini.
Lakini tangu serikali ijinasibu kwa maneno mengi bado maeneo mengi ya utoaji wa huduma za jamii yamekosa vitendea kazi mfano dawa mahospitalini na hata watoto kuendelea kukaa chini au kusomea chini ya mti kwa kukosa madawati na vyumba vya madarasa.
Mfano mzuri juzi nilikuwa naumwa nikaenda hospitali ya Benjamin Mkapa iliyoko ndani ya chuo kikuu cha Dodoma - UDM ambayo ni hospital kubwa mpya pengine kuliko zote hapa nchini lakini cha kushangaza dawa za kawaida tu niliambiwa hazipo.
Nikaamua kwenda hospital ya mkoa napo majibu yakawa hayohayo, badala yake wakanielekeza maduka ya dawa ya watu binafisi yaliyoko jirani na hospitali (blue, providence na chamwino pharmacy) ndipo nilifanikiwa kupata dawa hizo.
Sasa nauliza hayo makusanyo ya kodi pamoja na mapato kutoka vyanzo vingine mnayojinasibu kuwa mnayapata, nani anakula au nyie watumbuaji nao mmegeuka viwavi jeshi?