Pesa za jipu lijalo uwape walimu wetu

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,072
Mh. Raisi kila ukitumbua jipu unamwaga pesa, mara kadhaa umeonesha nia ya kutaka kutoa percentage ya kamato la jipu kwa watendaji kama vile ulivyomuelekeza pilato mkuu.
shida ipo kwa walimu wetu, hawa jipu kuu la kulikamata hawana ila wanafunzi wao wanafanya hayo ila sifa zinaenda kwa taasisi wanazozitumikia sasa!
Ombi langu kwako, hawa walimu wetu kwanini basi hata wasipatiwe motisha yeyote kazini kwao. hawana vitendea kazi na gharama za kulipia utumishi house hawana. President wajingeeni nyumba karibu na shule angalau wachache wabaki muda mwingi na watoto wetu.
NHC, PPF, NSSF na PSPF wasaidiane kukamilisha hili.
walimu hawana makuu wao hata 2 bedroom house bila ya dinning wala choo ndani wanaishi!
 
Aisee very touching...............mwalimu mwenzangu ila mwenzio yalinishinda nikahamia kwingine...nafundisha ila sio wanafunzi.
 
Watumishi wa umma wengi wana changamoto za kimaslahi. Akiamua kurekebisha, basi arekebishe kote. Habari za watu wazima kuanza kusema, "tumepata first lady na waziri mkuu walimu" si za kimantiki.

Muda ukifika, arekebishe maslahi ya watumishi wote wa umma.
 
Hawezi na haji kuthubutu kumuinua mwalimu. Ualimu kazi iliyodharauliwa na hata wasiosoma! Japo wote yaani mkulu, mkewe na waziri mkuu ni walimu hawatawakumbuka walimu we zao kwani ni utamaduni uliozoeleka kwa viongozi waliotokea kwenye ualimu kuwakandamiza walimu wenzao. Rejea awamu za marais waliopita kwani baadhi walikuwa walimu. Yaani wataendelea kuwadharau na kuwatumia kwenye chaguzi na sensa tu basi. Walimu wahesabu maumivu na waendelee kukaa kwenye nyumba zisizokidhi na kufanana nao. Yangu macho na muda utaamua.
 
Kama malimbikizo ya madai yao inakuwa ngumu kulipwa ndio waje kukumbukwa vitendea kazi na makazi?
Sasa hivi tuu wameshaambiwa mtoto akifika darasa la tatu hajui kusoma na kuandika watawajibishwa wakati ndio wamerundikiwa watoto 200 darasa moja na vitabu hakuna.
 
Watumishi wa umma wengi wana changamoto za kimaslahi. Akiamua kurekebisha, basi arekebishe kote. Habari za watu wazima kuanza kusema, "tumepata first lady na waziri mkuu walimu" si za kimantiki.

Muda ukifika, arekebishe maslahi ya watumishi wote wa umma.
Watumishi wa umma ni kweli wana maslahi duni, lkn shuleni kuna shida zaidi!
Just imagine Mwl ambaye kila mtu hadi mwanafunzi anaona anavyohangaika unajua inamshusha na kumfanya asiwe mwenye kujiamini!
Sasa Mwl aliyekata tamaa atamfundisha nini mwanao?
Tunahitaji brain ili taifa lisonge mbele! Sasa hiki kiwanda cha brain! Kwanini kisiboreshwe?
Pia kamà unaona kuna taasisi nyingine anastahili just say so lkn sio kutengeneza dhanà zako za kuwa wakuu ni walimu ndio maana ya Uzi huu!
Kwa. Taarifa sina uhakikà nà awamu ya mkàpa lkn àwàmu nyingine zote pàlikuwa na àngalau Mwl mmoja analala ikulu!
 
Kama malimbikizo ya madai yao inakuwa ngumu kulipwa ndio waje kukumbukwa vitendea kazi na makazi?
Sasa hivi tuu wameshaambiwa mtoto akifika darasa la tatu hajui kusoma na kuandika watawajibishwa wakati ndio wamerundikiwa watoto 200 darasa moja na vitabu hakuna.
Tunamkumbusha tu Mkuu!
Jipu la elimu ni gumu sana!
Gharama za ujinga ni za milele!
We anza kupata picha ya watendaji wa sasa wengi wanavyokuwa hawana tija!
Kama hatutoi motisha tutaendelea kulalamika lkn hatutofanikiwa!
 
Nyumba,hasa maeneo ya vijijini,halafu salary inayokidhi mahitaji muhimu.
Walimu hawakuwahi kulipwa pesa nyingi wakati wowote wa historia ya nchi hii, lkn waliheshimika ktk jamii!
Respect ilijengwa kwa kuwatengezea mazingira yenye heshima!
Mwl kijijini alikaa ktk nyumba ya bati na katika maeneo maalum karibu na shule, udhaifu wake alibaki nao ndani kwake na ktk kota zao! Leo wanapanga na wanadaiwa kodi, wanadandia daladala na wanagombana na konda, Mwl akija shule kachelewa maana hana pesa ya kuzunguka na daladala na anatoroka ili awahi kabla ya usafiri haujawa wa shida! Masomo ya ziada atakupa nani? Nani atabaki hadi jioni kusahihisha madaftari?
Lazima walimu wachakachue kukimbizana na wakati!
Jenga Magufuli nyumba za gharama nafuu kwa walimu wetu labda tutawanusuru na kulinusuru taifa letu!
 
Back
Top Bottom