frontline7
Member
- Sep 26, 2013
- 31
- 25
Wadau mimi nahoji hili...
Kama "pesa za dili" ziliwawezesha wazazi kuwapeleka watoto wao shule, kulipia pango la nyumba, kulisha familia, kupata huduma za afya, kulipa kodi za serikali, kujenga pamoja na mengine mengi; kwanini basi serikali imeamua kuwanyang'anya watu wake "pesa za dili" na ninavyojua mimi moja kati ya majukumu ya msingi ya serikali kwa watu wake ni kuhakikisha ustawi bora katika nyanja zote za maisha,
kwanini basi "pesa za dili" zisiachiwe tu ili watu wapate nguvu ya kupata mahitaji haya ya msingi?
Au serikali ina lengo tofauti kwa watu wake? Maana kama "pesa za dili" ndizo zilikua zinaendesha nchi, sasa hapa serikali inataka kutuambia nini?
au ina mpango wa kukuza umasikini na kuondoa maisha bora?
Nahoji tu, au mimi ndo sielewi? Hizi "pesa za dili" si kama hizi noti za Tshs 500,1000, 2000, 5000 na 10, 000 tu? Mbona sasa hazionekani?
Wala mimi si mchochezi. Nauliza tu..