PESA YA NCHI INAPOKUWA SOUVENIR.

jembe2015

Senior Member
Sep 21, 2014
118
71
Mfano mzuri ni kwa nchi ya ZImbabwe ambapo noti zote hizi ambazo jumla yake ni trilioni 50,bilioni 30 na milioni 260. 50,030,260,000,000.

Zinanunuliwa mitaani Harare kwa USD 20 na watalii.

Hapo ndipo mhe.Rais Mugabe alipo ifikisha nchi yake baada ya kuwa madarakani kwa miaka 35.

Utaratibu wa kubeba magunia ya fedha hatimaye ulishindikana,wananchi wakaamua kuachana na pesa yao wakaanza kutumia USD na Rand za Afrika kusini.

Watanzania tukazane na tumuunge mkono Rais Magufuli kuwabana wahujumu uchumi wote katika sekta zote hasa bandarini ili uchumi wetu usiyumbishwe na wahujumu uchumi kwani hata Zimbabwe yalianza hivyo hivyo kwa wakubwa kujichukulia mashamba ya wazungu na kushindwa kuyaendeleza.

Wakakataa kuyagawa kwa wakulima wadogo wadogo waliokuwa hawana ardhi.Hatimaye vijana asio kuwa na ardhi wakakimbilia mijini.

Kutokana na kukosa ajira wakaanza kujenga kiholela,Rais Mugabe akawavunjia nyumba zao.

Tuwe macho na tuombe sana mhe.Rais atumie busara zaidi ili yasije kutukuta haya.


Naomba kuwasilisha.
 

Attachments

  • 20160105_215352[1].jpg
    20160105_215352[1].jpg
    124.6 KB · Views: 40
Basi salamu hizo zimfikie JP kwamba Bomoa Bomoa bila Mpango wa ardhi mbadala yenye huduma za jamii kama shule ,hospitali,umeme,barabara,maji -ni kuongeza tatizo! Sijui ni kwa kiasi gani mpaka leo wale waliopelekwa Mwambe pande kama wameweza kumudu maisha na kiasi gani hudumua hizo muhimu zipo!

Hakuna anayetaka kuja mjini bila sababu-shida za pembezoni na vijijini ndiyo inayowaleta watu mjini.
Serikali ielekeze nguvu huko.
Maji
Shule.
Hospitali
Barabara
Umeme
na mwisho miradi ya Maendeleo-ufugaji wa Kisasa(Ngome,Kuku)-Kilimo bora na ya Kisasa.
 
Back
Top Bottom