Pesa ya mkopo sio yako

ItsMi

Member
Sep 13, 2021
66
31
Habari yako ewe mdau wangu wa nguvu.

Mara kadhaa tumekuwa tukiona watu wanachukua mikopo kwenye benki tofauti tofauti au taasisi za kifedha huku wimbi kubwa la wanaochukua mikopo hiyo ikiwa ni wafanyabiashara pamoja na watumishi wa serikali.
Wengi wamekuwa wakichukua pesa hizo kwa ajili ya mambo mbalimbali huku wengi wao wamekua wakiandamwa na madeni yanayopelekea kuuzwa kwa mali au dhamana zilizokuwa zimewekwa ili kuweza kukopa pesa hizo na kumekuwa na watu wachache sana ambao wanafanikiwa kurejesha pesa hizo.

Hivyo leo nimeona kuja na mada hii kwa kuwa wengi wamekuwa wakifika mahali pabaya kwenye maisha yao kwa sababu walikosa washauri, hivyo hii ni njia ambayo inaweza kutahadharisha maamuzi yako kabla haujachukua mkopo kwa haya ni majibu kwamba kwanini haupaswi kukopa fedha.

1.kukopa kwa ajili ya harusi au sherehe unayotaka ifanyike kwa kutaka kufurahisha watu wengi ambapo kulia utalia peke yako kwa kuwa inawezekana ukazipoteza mali zako kwa kuuzwa kwasababu umeshindwa kulipa deni ulilokopeshwa.

2.Kukopa kwa sababu kuna uwezekano mkubwa wa kukopeshwa pesa hizo, hii sio nzuri kwa sababu kama ikatokea umepewa pesa hizo itapelekea kuzitumia pasipo bajeti au malengo maalum hivyo inaweza ikapelekea ukashindwa kuzizalisha pesa hizo na kuingia matatizoni na hatimaye mali zako kuuzwa kwa mujibu wa mkataba wenu mlivyokubaliana na kusaini.

3.kopa kwa malengo usiige mkumbo kwa kuwa kila mtu anayo akili yake katika kuhangaika na kulipa madeni ya mkopo aliochukua

4.usichukue mkopo kama hujui faida na hasara kwenye biashara unayotaka ufanye au kuanzisha, kwasababu unaweza kujikuta umekopa pesa na hakuna ulichokipata sasa nadhani tunajua kitachotokea.

5.Usichukue mkopo kwa sababu umefirisika, na kama tunavyo fahamu kwamba hakuna kitu kibaya kama madeni ambayo hujui utayalipa vipi. Sasa imetokea umefirisika umeenda kuchukua mkopo kuanzisha biashara kwa dhamana mara gafla nayo biashara chali.

SIJASEMA KWAMBA USIKOPE AU USIINGIE KWENYE MADENI HAPANA, ISIPOKUWA TUWE NA MITAZAMO CHANYA KATIKA KUKOPA PESA HIZO ILI KUWEZA KUZIZALISHA ZAIDI ZILETE FAIDA KWA PANDE ZOTE MBILI.

Hivyo usichukue pesa endapo huna matumizi madhubuti yanayolenga uzalishaji wa bidhaa au huduma flani unayoitoa, pia unaweza ukayazingatia haya yatakusaidia.

1.tunakopa pesa ili kuanzisha biadhara au kutanua wigo wa biashara zetu ili tufikie malengo yenye tija kwa maisha yetu.

2.Pesa ya mkopo siyo ya kwako na haitakiwi uifanyie mchezo kwa maana waliokukopesha pia wanaithamini hata kama wewe unaiona ni ndogo lakini wao huitazamia makubwa.

3.Pesa ya mkopo inahitaji mpangilio mzuri wa bajeti katika kuizalisha zaidi ili ikuletee faida kwako na yule aliyekukopesha kwa kumlipa riba Stahiki.

4.Pia unapokopeshwa hakikisha unalipa deni ili kuimarisha imani yako kama mteja kwa aliyekukopesha ili ikitokea siku nyingine umepata shida iwe rahisi kukopesheka.

5.Pesa zinahitaji nidhamu ya hali ya juu sana kwa sababu wengi wamekuwa wakifikia pabaya kiuchumi hii ni kutokana na matumizi ya pupa kwa pesa walizozipata na hatimaye wakazitumia bila ya kufanya uwekezaji na pengine waliziona nyingi kiasi kwamba wakaamini hazitokwisha kamwe, Kwa hiyo wakachezea bahati na kufika mahali hivi sasa hawana kitu. Wakihisi kama ulikuwa upepo tu ukawapitia na kwenda zake.
Na hiyo yote imetokana na matumizi mabaya na usimamizi mbovu wa pesa au kukosa nidhamu ya pesa,

ninachotaka naomba tuelewe kwamba mahali popote penye mafanikio ipo bajeti, uvumilivu na kujinyima ili kuhakikisha kwamba unaifikia ndoto uliyojiwekea
Kwa kuwa kama ukikopa pesa na hatimaye ukashindwa kuzilipa Kinachokuwa kimebaki ni kufirisiwa kwa mali zako zote ulizokuwa umeziwekea dhamana ya kupata mkopo huo.

Kwa hiyo hili litakusaidia wewe kuweza kuisimamia vizuri pesa ili ikuletee mabadiliko kwenye maisha yako

SASA MAAMUZI NI YAKO PAMBANA USIRUDI NYUMA.
ASANTE.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom