Pesa ndio kila kitu kweli?

Pesa ndio kila kitu kweli?

mende 2014

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2014
Posts
763
Reaction score
131
"Wapo wanaodai" "PESA NDIO KILA KITU" SI KWELI!," PESA SIO KILA KITU" 'Pesa yaweza kununua (KITANDA) wala sio (USINGIZI),
Pesa yaweza kununua (SAA) wala sio (WAKATI),
Pesa yaweza kununua (KITABU) wala sio (MAARIFA),
Pesa yaweza knunua (CHEO) wala sio (HESHIMA),
Pesa yaweza kununua (DAWA) wala sio (AFYA),
Pesa yaweza kununua (DAMU) wala sio (UHAI),
Pesa yaweza kununua (ANASA) wala sio (UPENDO),
Pesa yaweza kukupeleka (INDIA NA CHINA) wala sio (MBINGUNI) umeamini kuwa pesa sio kila kitu au unakataaa? Mheshimu Mungu yeye ndio kila kitu sio pesa
 
Mkuu hiyo ndoto ni ya asubuhi au ya mchana maana kuna wembo usemao pesa ni sabuni ya roho na ushahidi wa pesa nenda misikitini na makanisani na kwa kuna makanisa mapya haya yapo mabararani au kila kona za kariakoo na kote huko ni makilele ya pesa au sadaka ya pesa tuu vitu hawavitaki wao ni mapesa tuuuuu
 
Achana na misemo ya kujipa moyo PESA NDO KILA KITU hayo mengine yatakuja badae
 
pesa ndio kila kitu..nani anapajua mbinguni kungekuwa kunatambuliwa nauli yake ingejulikana na pesa ingetumika..kama hii dunia imetengenezwa kwa material things pesa ndio kila kitu Duniani...Upendo nani anaujua unshikika,Penzi si touchable..pesa inalileta pia amani inaletwa na pesa .
 
katika material world pesa ndio kitu, unangaaliwa una bei gani, heshima umaarufu na kuthaminiwa ikiwemo kuogopwa huanzia hapo ndo maana kuna usemi usemao MWENYE PESA SI MWENZAKO
 
Wanaosema hvyo ni wavivu na failure ishawakaa.

Wanatumia justification hyo ku-certify uvivu wao.

Ishi Tandale kwa tumbo halafu mwenzao aishi Masaki, tuone kama hela hainunui kila kitu.

Fanya kazi 24/7 na uwe happy na familia yako halafu mwenzako aende likizo Zanzibar na familia yake halafu useme pesa hainunui kila kitu.
 
"Wapo wanaodai" "PESA NDIO KILA KITU" SI KWELI!," PESA SIO KILA KITU" 'Pesa yaweza kununua (KITANDA) wala sio (USINGIZI),
Pesa yaweza kununua (SAA) wala sio (WAKATI),
Pesa yaweza kununua (KITABU) wala sio (MAARIFA),
Pesa yaweza knunua (CHEO) wala sio (HESHIMA),
Pesa yaweza kununua (DAWA) wala sio (AFYA),
Pesa yaweza kununua (DAMU) wala sio (UHAI),
Pesa yaweza kununua (ANASA) wala sio (UPENDO),
Pesa yaweza kukupeleka (INDIA NA CHINA) wala sio (MBINGUNI) umeamini kuwa pesa sio kila kitu au unakataaa? Mheshimu Mungu yeye ndio kila kitu sio pesa

Kwa mchaga pesa ni kila kitu kwao sasa unaposema sio kila kitu wanaweza kukupa hata kipondo.
 
pesa inaleta heshima na utu ndani ya jamii, pesa inanunua haki Mahakamani. nasema pesa ndo mambo yote, hutaki kaa hata siku bila kutafuta pesa uone.
 
Back
Top Bottom