Pesa na shida zinakwenda pamoja

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,561
44,753
Nashindwa kuelewa kwanini ukipata pesa ndo shida zinaanza..kwa mfano Mimi kipindi nimebumbwa kitaa Sina kazi nilikuwa natumia chini ya laki mbili kwa Mwezi kwa mahitaji yangu nikiunga unga katika vibarua.ila nashangaa nikapata kazi napata Zaidi ya laki sita kwa Mwezi ila ndo shida zinajitokeza zinazofanya nisolve.

Kwa mfano kulipa fine au fidia baada ya kuharibu Mali ya mtu Mara police kila kukicha kusolve misala ya hapa na pale.yaani shida shida zinajitokeza mpaka hio laki sita Tena naiona ndogo haitoshi mambo Ni mengi muda nashindwa kufahamu kwanini siwezi Tena kwenda na Yale matumizi ya laki mbili kwa Mwezi Kama mwanzo halafu hata kujenga sijengi Wala siweki akiba yaani zote zinapotelea kwa binadamu wenzangu.
 
Umetunza zako hela kwa miezi sita Unataka ufanyie Jambo ile siku unavunja kibubu tu ndo siku hiyohiyo inapigwa simu toka kijijini unaambiwa bibi yako kameza chemli!..

Mkuu pesa inasaikolojia yake,ukipata na saikolojia inabadilika so ni ama ikubadili au uibadili inategemea na unajiweza kisaikolojia kiasi gani!. Kwa matajiri pesa huleta pesa hatunzi pesa ikae tu!. Kibongobongo matatizo ndo yanamaliza pesa taratibu naanza kuwaelewa wale wanaopata fedha halafu wanajificha wanaizalisha ikiwa nyingi ndo anajitokeza.😀
 
Back
Top Bottom