Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,209
- 4,406
PESA NA ELIMU.
1) Tangu jua kuchomoza,nimetanga kwenye njia,
Kwamba tumbo kuijaza,ndilo hasa langu nia,
Niwe sako na ruwaza,na riziki kujipatia,
Jihatada hata ingawa,haiondowi kudura.
2)vipi umekosa mwanga,kwenye kiza chenye nuru.
Laiti ungejipanga,ungelikwepa tanuru.
Jipange toka upanga,arusha dar na hedaru.
Pesa wananita nuru,fahari ya ulimwengu..
3) Afadhali umekuja,mjalaana wa mauko,
Asili wa vyote vioja,metufanya maeko,
Nakuvisha langu koja,bila wewe mimi siko,
Dunia imepotoka,tangu pesa kutumika
4) Wadamu ni asili,pesa walishaumbiwa
Bilayo ujahili,dunia utakimbiwa.
Kwanza mimi ujabali,ulimwengu navutiwa.
Pesa sabuni ya roho,na furaha duniani.
5) Una hila za ujanja,ufanyayo kwenye nyanja,
Watuweka paruwanja,tukosapo kubinginja,
Pindi tunapokuonja,twajitosa kwa uwanja,
Nafikiri una baya,tulisali kubla kuja.
6) Pesa bwana ni silaha,bunduki zito mzigo
Kusomasoma wahaha,darasa wapata pigo.
Pesa ni chanzo cha raha,iweje kwako kipigo
Pesa chakula kitamu,ladhaye huishi hamu.
7) Siwe mtazamo chanya,meshamiri pia hasi,
Mapwaguzi unamanya,pamoja nao waasi,
Ufisadi nchini Kenya,kweli wewe ibilisi,
Kupe kwao viongozi,tamaa kabla mauti.
8) Miye ndie mtawala,weye ni makaratasi
Mwenyewe ni nayo nywila,ya maisha marahisi.
Elimu mbona ni hila,maisha kuhisihisi.
Pesa siyo ufisadi,tafuta acha elimu.
9) Hino kisengere nyuma,kabla kukupa shutuma,
Vipi enzi za mama,halal hapakuwepo lalama,
Hata mosi kwenye uma,kisa chumo walichuma,
Malipo yakawa bidhaa,ujio kavunja staha.
10)Kumbe watamani pesa,mbona waogopa sema
Mfuko waupapasa,ungelinena mapema.
Mihela upewe sasa,ununue japo sima.
Pesa ni shibe ya kweli,elimu njaa legea.
11)Sio kama nakupenda,ila hapa sina budi,
Nipo kwenye njia panda,kukusaka inabidi,
Najituma kwa kibanda,nikipigwa na baridi,
Ningepata kibadala,kunikinaisha nafsi.
shairiESA NA ELIMU.
Mtunzi:Briyan Makungah wa Nakuru Kenya.
+255724845351.
Idd ninga wa Arusha Tanzania.
+255624010160