my name is my name
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 2,016
- 2,402
Perfect strangers ni muvi ambayo inazungumzia hasara za simu katika maisha ya mahusiano na maisha ya kawaida.
Hii muvi inahusu marafiki wanne na wake zao ambao wenyewe wanaamini wanafahamiana vizuri hawafichani kitu kila tukio baya zuri wanashare hamna siri kati yao. Wamekuwa wakifahamiana tangia utotoni wamekuwa pamoja.
Sasa siku moja wameamua kukutana pamoja. Walivyokutana wanaamua kucheza mchezo ambao kila mmoja anaweka simu mezani. Simu ikiita unaweka loud speaker kila mtu anasikia unachoongea. Mesej ikiingia unasoma kwa sauti kila mtu anasikia na anaona.
Ila kilichokuja kutokea yani yule mtu unaona unamfahamu vizuri hamfichani kitu kumbe Kiukweli humfahamu kabisa ni mtu mgeni kwako. Hata mke na mume ni wageni hawafahamiami 😂 maana kila mtu ana mambo yake mabaya au mazuri anayaficha na hakuna mtu anajuwa zaidi ya yeye mwenyewe tu. Hata mmoja wao katika kundi lao kumbe anatembea na mke wa mmoja wa rafiki yake 😂
Hii muvi imetolewa kwa mara ya kwanza nchini Italy 2016 kwa Jina la perfetti sconosciuti. Ilifanya vizuri katika box office nchini humo. Baadae kuna nchi zika remake hii movie na kila nchi iliyoremake mauzo yake pia yalikuwa mazuri ktk box office.
Nchi zilizo remake ni ugiriki kwa Jina la (Teleioi xenoi), Spain kwa Jina la (perfectos desconocidos), Turkey kwa Jina la (Cebimdeki Yabanci) na France kwa Jina la (Le jeu)
Hii muvi inaonesha uhusiano wa technology na mahusiano. Ni muvi nzuri sana na version zote nzuri. Nani yuko tayari kucheza huo mchezo na yule mtu unayemuamini sana na hamfichani kitu?