Pepo za mabadiliko zaja tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pepo za mabadiliko zaja tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PMNBuko, Jan 11, 2011.

 1. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu Tanzania wa Oktoba 2010, tumeshuhudia pepo kubwa sana zikivuma kwa kasi kutoka pande zote za nchi yetu. Ni pepo za mabadiliko. Wananchi wanataka madadiliko ya kweli. Watawala walioko kwenye ngazi kubwa za nchi hii ama wamezisikia au kuziona hizo pepo lakini bado hawajaonesha jitihada za kuzizuia. Ni mwanzo wa miti mikubwa yenye nguvu kubwa (Key Politicians) kuangushwa chini na pepo hizo. Ni wakati ambapo watawala hawataamini kilichofanyika.

  Mabadiliko haya yamenikumbusha Hotuba makini na ya kihistoria ya Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Mr Hrold Macmillan alipotembelea Afrika na tarehe 3 Februari 1960 na akahutubia maelfu ya watu huko Afrika ya Kusini, na kusema:

  "The wind of change is blowing through this continent (Africa), and whether we like it or not, this growth of national consciousness is a political fact. We must all accept it as a fact, and our national policies must take account of it." - Harold Macmillan.


  Kinachotokea leo hii Tanzania kisiasa ni kama hiki akisemacho Harold. Basi, ni wapi tunahitaji kufanya mabadiliko ili pepo hizi zisituangushe chini? CCM wako wapi katika hili? Wamejiandaa vipi kukabiliana na Pepo hizi? Je kuendelea kukwepa "political facts" zitasaidia siku chache za usoni?
   
Loading...