Penzi kitovu cha uzembe

snail

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2012
Posts
462
Reaction score
142
Habarini woteee!

Natambua hili swali linahusika sana JF doctor venue. Lakini naomba niulize hapa MMU kwakua nahitaji kumtoa mtu kwenye mawazo mabaya haraka mno na katika hali ya kawaida jf doctor majibu yanachelewa coz wadau wake wako busy sana! Ila badae nitalipeleka jf doctor ili wachambuzi wenye uwezo walione;

Swala ni hili: Dogo wangu ametembea na binti wa jirani mwenye umri wa miaka 18 bila kinga mara kadhaa. ila uhalisia ni kwamba mama wa huyu binti alikufa kwa ukimwi miaka mitano iliyopita na waliokua rafiki wa huyu mama mimi ni rafiki zangu na walishaniambia kua binti ambaye katembea na dogo wangu alisha athirika toka kwa mama yake. Dogo wangu anapata hofu kwakua nae ameambiwa na rafiki zake kama nilivyo ambiwa mimi hadi imemlazimu kuweka wazi habari hizi kwangu kaka yake, binafsi sina ufahamu sana na nimemwambia anipe muda kidogo!

Sasa naomba msaada wa jibu, je yawezekana kwa binti kuadhirika toka kwa mama na akaweza kuendelea na maisha hadi kufika umri wa miaka 18? Izingatiwe kua sasa hivi yuko vizuri sana hana muonekano wa afya mgogoro hata kidogoi.

Ahsanteni,
Naomba kuwakilisha hoja.
 
Mimi sioni haja ya kujua afya ya binti, lisemwalo lipo kama halipo....Mwambie mdogo wako akapime kujua afya yake baasi.
 
Binamu yangu ameishi navyo toka akiwa 1 year old haadi leo mwaka wa 17 huu nae alipewa na wazazi wake
 
Mimi sioni haja ya kujua afya ya binti, lisemwalo lipo kama halipo....Mwambie mdogo wako akapime kujua afya yake baasi.

kupima itakua lazima sema kwa sasa haina haja coz ana wiki moja na nusu tu tangu aanze kutembea nae kwa mara ya kwanza
 
duh...huyo ilishakula kwake aanze tuu kuchimba kabiri mapemaaaa
 
Kuweni makini na ukimwi eti ivo vitu sio vya kufanyia pupa ilo shimo lime zika wengi sana.
 
kupima itakua lazima sema kwa sasa haina haja coz ana wiki moja na nusu tu tangu aanze kutembea nae kwa mara ya kwanza
kama ni kweli ni wiki moja na nusu imepita basi ana bahati. Nenda Muhimbili University wanapofanya utafiti wa dawa ya ukimwi, wana vipimo vya hali ya juu lakini pia wanaweza kumuanzishia dawa mapema na kuendelea kumfuatilia kuona matokeo yanakuwaje. Ukweli ni kwamba kuanza dawa mapema uwezekano wa kuua virusi kabla havijajificha sehemu ambayo dawa haiwezi fika ni mkubwa sana.Ni PM for further information
 
snail, kwa kuwa wewe halijakugusa moja kwa moja ila kwa kupitia mdogo wako... Unapaswa uwe imara kwa ajili yake. Sasa hivi UKIMWI upo kila mahala, hivyo bila kujalisha kuwa kalala na huyo binti ambaye inasemekana kaathirika; kama mdogo wako anafanya ngono zembe na anapenda kujua afya yake, yapaswa afanye vipimo.

Kujua status ya huyo binti jirani haitasaidia kitu... Kikubwa hapa ni wewe kumshawishi mdogo wako kama yupo tayari akapime afya yake kama kweli yupo tayari na ana wasi wasi.

Naomba niongeze kuwa kupima HIV/AIDs inahitaji utayari na si kukurupuka, hivyo ni vema mkatumia vituo ambavyo vimejikita kwa kutoa huduma hiyo... Kwa misingi kuwa huwa wana maandalizi mazuri zaidi ya kukujenga psychologically kabla na baada ya kuchukua vipimo.

Pole sana na wasi uliyo nao na nawatakieni kila la kheri suala hili.
 
Last edited by a moderator:
mimi namshukuru Mungu nilipata ujasiri wa kupima sio kwamba nilikuwa nimekukuruka au nikikanyaga mahali wala kipindi nimeamua tu kuanza kuishi upya na kuachana na mambo ya wanaume... ila kiukweli mimi nilipima kwa mara ya kwanza kituo kikubwa tu sikupewa ushauri wala nini ..sijui ningekutwa nao ingekuwaje.mara ya pili ni hospal kwetu ofsini ila hapa nilimwambia dokta wetu anipime tu kishkaji mwaka ulikuwa umepita nayo bila ushauri.mara ya tatu hapa nilienda kituo kikubwa tu haa nchini na my new mpenzi hatukupewa ushauri wala nini? so naona kupima ni wewe mwenyewe uamue .
 
kuna dogo mmoja yupo mtaani yupo 20 now wala huwezi jua yupo form six
 

Hongera sana Smile... Unastahili pongezi. Kwa kweli si wengi wana guts za kwenda kupima afya upande wa HIV/AIDs kama ulivyosema hapa. Na ikitokea upo willing kupima bila kushinikizwa kwa sababu yoyote ama mtu yeyote... Mara nyingi inakuwa rahisi kupokea majibu yoyote (yawe -ve or +ve); ingawa bado ukikuta majibu ni +ve roho inauma.

Kwa ambae anapima sababu tu kahisi mwenzie anaumwa/amekufa/kasikia tetesi or maybe anaumwa mara kwa mara si wote wanakuwa psychologically stable kuweza kupokea majibu tofauti na matarajio.

Hongera... Nimependa msimamo wako. Kila la kheri.
 
Ujue dunia ya sasa imebadilika na sioni haja ya mtu kuweka maisha yake rehani kwa ajili ya raha ya dkk kadhaa! Nilikuja kugundua the more mtu anakataa kupima the more unajiweka kwenye risk ya kuambukizwa.maana unakuwa ujiamini so ukiambiwa twende kavu unaona sawa tu ila ukiwa unajua afya yako si rahisi mu akakudanganya....mi sasa hivi mwanaume akionitaka lazima athibitishwe na tbs mwenzangu.
Tuache hayo turudi kwenye topic sasa inabidi huyu dogo kakae aombe kabisa wape ushauri nasaha kwanza naona wafanyakazi wa hivi vituo sijui wamechoka au vipi wao wanapima tu kama malaria
 

WOW...JUST WOW!!!!:yo:
 

sure siku hizi hakuna ushauri wala na saha! sijui ndo wameona ukimwi umesha zoeleka? wanasahau kua ukimwi ni sawa ma hukumu ya kunyongwa tofauti yake ni kwamba unapewa muda usio julikana kabla ya kufa
 

Smile... Mie ni moja ya wanawake ambao hilo tendo hufurahia... Tena sana. Hivyo huwa naliangalia hili suala huku nikijeweka katika nafasi za wahanga iwapo kuna story yoyote ambayo inahusisha hivyo.

Suala la ngono kwa kushirikisha ugonjwa wa HIV/AIDs siyo rahisi ki hivyo... Mara nyingine ni hata vigumu kuweza eleza nje ya what is right and what is proper. Kuna suala la uaminifu... Hilo ndilo hutuchinja sana. Inapokuwa kuwa mimi ni muaminifu to the maximum BUT mpenzi wangu siyo muaminifu - unadhani atakapo athirika, hiyo ngoma haitanifikia sababu tu kuwa mimi ni mwaminifu?

Swali linabaki ufanye nini? Ujikabe kutofanya mapenzi na uishie masturbation? (Ambayo haiwezi kukufikisha kama vile upo ma mtu wako); Umfuate mpenzi wako kama kupe kuwa naye kila dakika kwa woga wa kuwa atasaliti? Ama ujifanye mjinga na kuishi maisha ambayo unaamini kuwa wewe Mungu alikuumba so special kiasi kwamba virusi haviwezi kukunyavua?

Suala la HIV/AIDs ni mtihani mkubwa sana. Hivyo wewe umepima na kuamua kuishi kwaku abstain nakupa hongera sana na naona kuwa umeshinda kwani ni wachache wanaweza hiyo njia kuitumia kama kinga.

Nakubaliana na ulilosema kuhusu dogo. Upo sawa kabisa...
 
Ukiwa kwenye ndoa swala linabadilika.ila kama mimi sina haja ya kutembea na mtu ambae sijui afya yake kwanza kesho na kesho kutwa anaweza kuniacha.ni bora nisifanye kabisa. Ukiwa kwenye ndoa hapo ni kumuomba mungu tu kwa kweli maana hapo usalama wenu upo mikononi mwenu wawili.sasa hapo ni mtihani mzito
 
sure siku hizi hakuna ushauri wala na saha! Sijui ndo wameona ukimwi umesha zoeleka? Wanasahau kua ukimwi ni sawa ma hukumu ya kunyongwa tofauti yake ni kwamba unapewa muda usio julikana kabla ya kufa
labda wameona wanajichosha watu wenyewe hawaelewi mkuu.HAWAREMBI WALA KUBEMBELEZA UNAPEWA MAJIBU YAKO LIVE LIVE KABLA HUJAKIMBIA
 

umeongea kwa hisia hadi kaka mtu napata woga! nisije shindwa kumuelekeza dogo. daaah, kiukweli hata tunaowaamini waweza leta ngoma nyumbani!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…