Penzi jipya tamu khah! Sio kwa simu hizi aisee!

Mwalupale

JF-Expert Member
Apr 29, 2012
1,049
674
Jamani sikukuu ya Meimosi inaendaje huko kwenu?

Kumbe kuna watu huwa wanapagawa penzini kiasi hiki. Hizi simu ninazopokea kila mara sio za nchi hii. Na nilivyo mvivu basi najinafikisha tu. Anapiga simu kila mara sijui anachofurahia ni nini jamani?

Sasa nimeamini ile nadharia ya kwamba mwanamke akishafunuliwa huwa anatapatapa sana kilinda penzi na mwanaume akifunua huwa hana habari tena (vice versa is true).

Sasa imebaki nikipokea nabaki nasema "niambie baby" nayeye ananijibu "mi sina usemi niambie wewe" hahahahahaha uuuuuwi!

Ananiudhi sana ila namlia timing ya kumtuliza munkari bila kumuathiri kisaikolojia manake kazi haziendi ni simu tu kila muda.

Wadau kwa anaejua exit strategy nzuri anipe hapa niitumie ku exit kwenye hili penzi jipya litanitoa roho. Binti anataka tuongee kila baada ya nusu saa. Akimaliza kuongea anataka tuchat kwa sms muda wote.

Ukichelewa kujibu sms tu ataanzisha ugomvi huo duuh! Sasa hii sera ya serikali ya awamu ya tano ya hapa kazi tu nahisi itanipita kushoto kwakuwa kazi haziendi. This love is too strong nahisi huyu mtoto atarukwa na akili aisee.

Kama ulishawahi kuwa kwenye relationship ya namna hii niambie jinsi ulivyochoropoka. Msaada kwenye tuta.

Nawasilisha
 
Kwanini usimwambie tu kuwa apunguze kukupigia pigia na kutext, since unakuwa busy na kazi.... Nadhani atakuelewa

Hiyo ni better solution kuliko unavotaka kumuacha, tena kwa sababu ndogo kama hiyo

Pia kumbuka hiyo ni just a phase, most of the time as the relationship inazidi kukua, watu huwa wanapunguza huo mtindo wa ku-call na ku-text kila baada ya dakika
 
Ukitoka kwenye uvulana kufikia level ya uanaume utaujutia huu uzi.
Wala sitaujutia. Simu kila baada ya dakika kadhaa na kuchat kusikoisha. Hakuna jambo maalumu la kuongelea. Anapiga tunabaki tunaguna tu. Nakuhakikishia sitajutia. Mimi ni mvulana na pia ni mwanaume. Get real. Kwani wewe mumeo anakupigia kila mara hata kama hakuna jambo la maana la kuongea?
 
Kwa wanaume ninaowajua mimi ukimpigia mara ya kwanza atakusalimia vizuri ya pili anakuuliza 'unataka nini' kwa sauti flani hivi. Hupigi tena ukifiria hujui unachotaka na sauti wala si ya kubembeleza.
 
espy ananipigiaga simu saa saba usiku na kuendelea ole wangu nisipokee

this kind of love is new to me haupo peke yako
Mkuu mimi hazipiti dakika 20 bila kupiga. Alafu hakuna maneno ya kuongea sasa. Duh
 
Jamani sikukuu ya meimosi inaendaje huko kwenu?
Kumbe kuna watu huwa wanapagawa penzini kiasi hiki. Hizi simu ninazopokea kila mara sio za nchi hii. Na nilivyo mvivu basi najinafikisha tu. Anapiga simu kila mara sijui anachofurahia ni nini jamani?
Sasa nimeamini ile nadharia ya kwamba mwanamke akishafunuliwa huwa anatapatapa sana kilinda penzi na mwanaume akifunua huwa hana habari tena (vice versa is true).
Sasa imebaki jikipokea nabaki nasema "niambie baby" nayeye ananijibu "mi sina usemi niambie wewe" hahahahahaha uuuuuwi!
Ananiudhi sana ila namlia timing ya kumtuliza munkali bila kumuathiri kisaikolojia manake kazi haziendi ni simu tu kila muda.
Wadau kwa anaejua exit strategy nzuri anipe hapa niitumie ku exit kwenye hili penzi jipya litanitoa roho. Binti anataka tuongee kila baada ya nusu saa. Akimaliza kuongea anataka tuchat kwa sms muda wote. Ukichelewa kujibu sms tu ataanzisha ugomvi huo duuh!
Sasa hii sera ya serikali ya awamu ya tano ya hapa kazi tu nahisi itanipita kushoto kwakuwa kazi haziendi. This love is too strong nahisi huyu mtoto atarukwa na akili aisee.

Kama ulishawahi kuwa kwenye relationship ya namna hii niambie jinsi ulivyochoropoka. Msaada kwenye tuta.
Nawasilisha
Mwenye mapenzi ya thati na mwenza humuelewesha tuu kwa nia njema kbs na km ni muelewa hatopinga ulichomueleza.
Muite mueleze tuu.Haina haja ya kuexit wakati ndo kwanza penzi jipya,mueleweshe tuu bila shaka ataelewa kile unachokimaanisha
(Ila na sm za penzi jipyaunawezajikuta we ni malaika kwakweli,muda wote masimu na masms)
 
Wabongo tuna visa sana. Ukipendwa unaona kero na kuomba exit strategy

Ukiumizwa ooohhh "wanawake wanaumiza, hawana mapenzi yakweli".

Ila ujue Mungu naye ni mjuzi sana watu kama nyie huwa anawajaribu kuwaletea watu wakuwapenda kweli ila kwa akili zenu mnatafuta namna ya kuondoka unapopendwa kwenda kupenda usipopendwa.

Jitahidi utapata unachokitafuta, acha mie nibaki ninapopendwa hata ikipigwa simu saa tisa za usiku napokea tu hamna namna
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom