Pentagon yaja na Teknolojia ya 'Laser' yenye uwezo wa kutambua watu kutokana na mapigo ya moyo

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
May 27, 2016
5,416
7,828
Jetson: Teknolojia ya 'Laser' yenye uwezo wa kutambua watu kutokana na mapigo ya mioyo yao

1148146


Teknolojia iliyoandaliwa na Idara ya Ulinzi ya Marekani (DOD) imefungua uwezekano wa kutambua watu kutokana na mapigo ya mioyo yao. Teknolojia hiyo inajulikana kama Jetson, ambayo hutumia laser (Laser Vibrometry) kusoma mapigo ya moyo wa mtu (Cardiac Signatures).

Teknolojia hii ni ya kipekee kama ilivyo ile ya alama za vidole, yenye madhumuni ya kufanya utambuzi. Teknolojia hii ya utambuzi ni ngumu zaidi kuepukika tofauti na zingine ambazo kwa namna moja ama nyingine zinaweza kuepukika mfano, 'Face Recognition' ambayo unaweza kuiepuka kwa kuvalia kifunika uso (Mask) ama ndevu bandia.

Teknolojia hii imepewa uwezo wa kutambua mtu kutoka hadi umbali wa mita 200 kwa kuchunguza harakati za dakika juu ya uso wa ngozi dhidi ya mapigo yake ya moyo. Hi ni njia bora zaidi ya utambuzi sababu inaweza kutambua mtu akiwa umbali mrefu zaidi kuliko kuchunguza sura yake ama kuvikaribia vidole vyake kwa ajili ya 'Finger Prints' ambapo itahitajika mlengwa awe karibu.

Teknolojia hii imeundwa kutokana na maombi mbalimbali kutoka katika vitengo maalumu vya kijeshi nchini Marekani kuja na mbinu bora zaidi zenye kufanya utambuzi kwa usahihi zaidi na kwa umbali mrefu zaidi.

1148148

Makao makuu ya Idara ya Ulinzi nchini Marekani, Pentagon.

Meneja wa Programu ya Ofisi ya Usaidizi wa Kiufundi ya Kupambana na Ugaidi ya Pentagon, Stewart Remaly akitolea ufafanuzi kuhusiana na Teknolojia hii, alisema kuwa Teknolojia hii ina usahihi wa asilimia 95 na kwa nadharia inaweza kutumika kwa umbali mrefu zaidi.

Remaly alisema "siwezi kusema kwamba unaweza kutambua mapigo ya moyo kutokea anga za mbali lakini kwa umbali mrefu na wa kawaida hilo linawezekana kabisa".

1148144


Utambuzi kwa kutumia Teknolojia hii unaweza kutumia hadi sekunde thelathini (30) huku mlegwa husika akiwa mahali pamoja. Mara baada ya taarifa kukusanywa zinaweza kutumika kufuatilia magaidi wanaofikiriwa au watu wengine wenye maslahi binafsi.

Pamoja na kwamba Teknolojia hii ina usahihi kwa kiwango kikubwa lakini kutokana na upya wake na pia baadhi ya changamoto itahitajika zaidi kuhakiki majibu yake kwa kutumia teknolojia nyinginezo zilizo thibitishwa zaidi kama vile, Teknolojia ya utambuzi wa sura (Face Recognition).

Changamoto nyingine pia ni kutokana na upungufu wa taarifa za kutosha (Database) za za saini za mioyo (Cardiac Signatures) ambapo itahitajika kuandaliwa na kuendelezwa ili kuweza kuendana na mapigo ya moyo husika ama kinyume chake.

1148147


Licha ya hivyo, Teknolojia hii inaweza pia kutambua watu kutokana na matendo yao. Mfano, rekodi za mapigo ya moyo zinaweza kutumika kumtambua mhusika aliyetoka kufanya jambo fulani la kihalifu kama vile, kupandikiza bomu, ujambazi n.k. baada ya kukamatwa.

Unaweza kujibadili sura kwa kufanya 'Plastic Surgery' ama unaweza kuunguza 'Finger Prints' zako ila itakuwa ngumu sana kuiepuka aina hii ya Teknolojia ya utambuzi wa mapigo ya moyo pale itakapoanza kutumika hususan na vyombo vya ulinzi na usalama nchini Marekani.


Prepared by: FRANC THE GREAT
Sources: Forbes | Extreme Tech | Army-Technology | IFL Science | Getty Images
 
ufanisi wake ni kwa 95%,,hizo tano zilizobaki ndo wanapopitia akina hayatollah,
Hahaha! Si rahisi hivyo kutengeneza kitu chenye Accuracy ya 100%. Licha ya hivyo ufanisi wa hii Teknolojia ni mkubwa zaidi ukilinganisha na nyingine zilizopita ingawa bado ipo Under Development.
 
Hatuwezi kufika huko, sema tutafikiwa tu na hizo technologia. Tungesema tutafika ikiwa tunafanya kitu kutafuta technologia hiyo, sisi ni watumiaji sio wagunduzi. wakiisha itumia ikaonekana kwao imepitwa na wakati ,sasa wata I-cormercialize na wachina wataanza ku duplicate na sisi ndio tutaanza kutumia.
Nilishangaa eti kuna Tanzania ya viwanda bila technologia, hahaha vichekesho.
 
Hatuwezi kufika huko, sema tutafikiwa tu na hizo technologia. Tungesema tutafika ikiwa tunafanya kitu kutafuta technologia hiyo, sisi ni watumiaji sio wagunduzi. wakiisha itumia ikaonekana kwao imepitwa na wakati ,sasa wata I-cormercialize na wachina wataanza ku duplicate na sisi ndio tutaanza kutumia.
Nilishangaa eti kuna Tanzania ya viwanda bila technologia, hahaha vichekesho.
Wakati wengine wakifanya Innovations mbalimbali huku wengine wakifanya Reverse Engineering, nchi za Dunia ya tatu hasa Afrika bado zina safari ndefu sana.
 
Wakati wengine wakifanya Innovations mbalimbali huku wengine wakifanya Reverse Engineering, nchi za Dunia ya tatu hasa Afrika bado zina safari ndefu sana.
Sisi hatuna safari yoyote, tupo tu tumeng'aa macho tunasubiri wataleta na tuta nunua. Hatuna uwezo wa kuanza hata safari, wale COSTECH kelele nyiingi sijawahi hata kufahamu wanasimamia nini pale. PhD kibao lakini ugunduzi zero, Hata Phd za lugha wameshindwa kutafuta maumbo ya kutengeneza maandishi ya lugha zetu za asili, sijui hilo nalo wanasubiria Anthropologist waje wachimbe wagundue au inakuwaje. Sisi watuachie siasa na kupigana kwa hila za kisiasa ;lakini siyo tafiti na technologia.
 
Back
Top Bottom