Pensheni ya February kutoka Hazina

koryo

JF-Expert Member
Jun 21, 2010
639
278
Mimi ni mmojawapo wa Wastaafu anayepokea pensheni kutoka sehemu mbili tofauti kila mwezi. Pensheni zote huwa ninazipata kati ya tarehe 28 mpaka tarehe 1 ya mwezi unaofuata.

Tayari nimepata pensheni yangu kutoka LAPF lakini pensheni yangu toka HAZINA sijaipata hadi leo tarehe 7.2.2016.

Ikumbukwe sisi wastaafu tunaishi maisha magumu sana na tunategemea pensheni katika maisha yetu ya kila siku.

Ninawaomba HAZINA inieleze sababu ya kuchelewesha pensheni yangu.
 
Mstaaf uko vzur mpaka jf unaenda nayo sawa... Natumai wMekuskia mzee wangu
 
Mnapata pension mbili kwa mwezi?, hapa kuna ufisadi hebu tuelezee vizuri kabla hatujakuchulia hatua kali
 
Hawa wastaafu wanateseka sana,hasa hawa wa PSPF.mpaka mkurugenzi aamke vizuri sikuhiyo ndo anakumbuka kuwaingizia pesa zao
 
Mimi ni mstaafu mwenzako pia. Kama ni Mfuko wa PSPF, mimi nimepata pensheni yangu ya Feb., tarehe 3/3/2016 kupitia CRDB.
 
Back
Top Bottom