mkuu mimi hii serikali siipendi na naipinga kwa mengi mno....
na hapa utaona sitetei serikali bali napinga kiongozi wa dini
kutumia taasisi yake kuchochea vurugu....
siku zote tunapaswa kutetea sheria
ni bora siku zote sheria iheshimiwe..
hata kama ina mapungufu...
Dini zetu kuu ni uzao wa Ibrahim, kupitia watoto wake Isaka na ishmael, ishmael alikuwa mtoto wa mama mdogo, na kwa desturi watoto wa mama mdogo haweshi kulalamika, hata wapewe vyote.
Bwana masaburi unanitukana bure mi siko upande wowote ila sipendi kuona mtu akijaribu kutaka kuwauzuia polisi kufanya kazi zao ambazo sisi tax payer tunawalipa kuzifanya...tungependa kuona kodi zetu zinatumika vizuri,polisi wakikamilisha kazi zao huwa hawatoi hukumu,mzee pengo ikithibitika ataburuzwa mahakamani,na huko kuna haki,si uliona bwana zombe,wengi tulipenda afungwe au anyongwe akiwemo rais lakini kwa kuwa mahakama zetu ziko huru akapata haki yake...na hakuna aliye juu ya sheria hata pengo au mufti simba.
Nimekusoma mkuu!
Mwisho wa siku kusingekuwa na malumbano kama hatua zinachukuliwa.
Kama hakuna ushahidi wa wazi basi wafanye kama walivyofanya kwa kina Massawe kwa issue ya ujambazi 2006 na nchi ikatulia
kwa mara nyingine umeonyesha jinsi ambavyo hukunielewa. Nimeunganisha vitu vingi kiasi kwamba ukashindwa kabisa kuelewa na kuanza mashambulizi kwangu bure! Kanisa halijawahi kusema.kuna kuvuana gamba! Kuna watu walisema kwa kuwa mtu anatajwatajwa inabidi ajivue gamba bila ushahidi. Nilikuwa nahusisha na hayo maneno. Kama ulivyosema kuwa kama kuna ushahidi afunguliwe mashtaka na wala siyo kuhukumu mtu kwa kutajwa tajwa. Mkuu soma between lines! Sijahusisha gari la Kadinali na madawa ya kulevy na wala silijui gari lake. Nimeeleza vizuri tu jinsi nilivuooanisha vague na vogue kwenye gari la kifahari!Usijidanganye ukadhani unaongea na mtu mwepesi namna ya kunitaka niamini kuwa nilikosea kwa jinsi nilivyokufikiria mwanzo. Baraza la walei ndio linatumika kuhoji uhalali wa mambo ndani ya kanisa letu ikiwa ni pamoja na kuwadiscipline viongozi wabovu katika vikao. Sasa hebu tuyarejee maneno ya Mwenyekiti wa Baraza la Walei la Parokia
Sasa unaweza kunieleza huu ni utaratibu wa parokia yenu au wa wapi? Acha maneno ya kuungaunga. Tena jisikie mwenye mkosi kwa kujikosanisha na Mungu mapema namna hii mwaka ukiwa haujamaliza 24hrs. Kama wewe ni mkatoliki basi lazima ukiri imani yako kwa kanisa na sio kuleta majungu. Pale dhahiri ulimaanisha kulihusisha gari analotembelea Askofu na fedha za madawa, na ni kwa kuwa hujui linapatikanaje. Kama kanisa limefikia kuwa na wenyeviti wa mabaraza wa namna yako na kauli zako, basi Mungu atusimamie kwani tuanelekea kubaya.
Mimi sio mkatoliki namba one. Ila katika hali ya kuheshimu kanisa, sipo radhi kuona likichafuliwa na maneno yasiyo na ushahidi. Ni wajibu wa serikali kumkamata Askofu na kumfungulia mashtaka ili kanisa letu libakie kuwa safi. Otherwise ni uzushi na unashusha heshima ya aliyeutamka. Hatuhitaji serikali domokaya wala askofu muuza madawa.
Na bado nitaendelea kusema; Lowassa ameomba kushitakiwa kwa makosa yake anayoshutumiwa kwayo, mbona hashitakiwi? Tutumie akili zetu kama tunazo, kama hatuna tuendelee kujiita wenyeviti wa mabaraza bila aibu kwa kuwa hatujuani, ila Mungu anatujua.
siwezi kusema lolote..kwasababu wauza madawa ni binadamu na Pengo ni binadamu, ila napata mashaka kama anaweza kufanya hivyo kwasababu ya kazi yake..najaribu kuwaza chanzo cha jina lake kutajwa kama muuzaji wa dawa ni kipi na askari wetu kwann wasitumie chanzo hicho kuthibitisha au kumsafisha?
masabuda sio masaburi! nimekuelewa ila ulimhukumu pengo kwa kulizungumzia hilo jambo ambacho mi niliona sio sahihi mwache abwabwaje atakavyo mbona jk nae anamisemo ya kuwa "uongo ukisemwa semwa sana hua ukweli nimeona hilo nilizungumzie"
mimi serikali yake imeprove failure kwenye mafisadi papa, drug dealers wanabaki kukimbizana na wale walio meza pipi airport! je wanaoingiza makontena na yanapita! wea is the government? vyombo vya dola polisi, tiss, takukuru? yote ni jk ndio anayalea na kuyaendekeza
mimi ningefurahi sana kusikia pengo kakamatwa kafikishwa kwenye vyombo husika na sio kumsema kwa mafumbo utafikiri ww mwanamke kumbe rais wa nchi!
tunakazi ya kuweka haki sawa kwa wote, na hapa lazima tuzichape kwanza yaani tupigane vita siku moja ndio tutaheshimiana na kutengeneza system kama rwanda, mambo ya kulindana yamepitwa na wakati
HAKI SAWA KWA WOTE, FULSA SAWA KWA WOTE, MKONDO WA SHERIA SAWA KWA WOTE!
Na yeye jk kasema "Mimi mwenyewe nimewekwa katika orodha ya dawa za kulevya"?
kila kitu si siasa,hizi issue za kudhalilisha watoto zinzolikabili kanisa dunoa nzima sasa na wakatoliki wenyewe wanalalamika kwambapapa hachukui hatua anaficha madhambi,JE NI HABARI LEO,CCM AU SIRIKALI INAHUSIKA.yule pdre alomnajisi mtoto chuo kikuu kweye gari ni serekali imetunga au habari leo.anachotakiwa pengo kusema ni kuilazmisha serikali ithibitishe.HE WHO ALLEGE MUST PROVE
yeye kasema anapakaziwa...na serikali inaweza kesho kukanusha..likaishia hapo..
Mkuu hiyo ilikuwa inajibu post ya mtu ambaye awali alisema post yangu ni vague (haieleweki) nami nikajibu Gari la Kifahari? Nikiwa na maana ya kumtania kuwa alikuwa akimaanisha gari ya kifahari Vogue! Anatokea mtu mwingine anasema nimeunganisha gari ya kifahari anayotumia Muhashamu na madawa ya kulevya! Narudia tena sijawahi kuiona gari ya Muhashamu Polycarp Kadinali Pengo na sijui anatumia gari y kifahari ama la. Na kama ni ya kifahari siijui ni make gani!Nilidhani gari la kifahari ni Vogue sio Vague
Hivi jamani hii thread umeisoma kweli au mnakurupuka tu kuchangia baada ya kusoma comment za wachangiaji?hebu someni kwanza bwana,ni wapi kwa mfano umeiona hii "mimi ningefurahi sana kusikia pengo kakamatwa kafikishwa kwenye vyombo husika na sio kumsema kwa mafumbo utafikiri ww mwanamke kumbe rais wa nchi!"
Rais ndio kamtaja bwana pengo au bwana pengo hapa kajitaja mwenyewe na hakuna mwenye uhakika na anachokisema
Mnafiki mkubwa huyo anafanya watu wazima watoto! achie ngazi basi ili uchunguzi uwe fair sio! kwani si ndio kawaida tukichunguzwa twaachia nafasi tulizonazo!
kwa hili jk huniambii kitu na nakuchukia mbayaa mno sio kwa sababu ya dini yako bali kwa mambo na sanaa zako! chaguo langu likuwa Ahmed Salim Ahmed that was the best president ever!
Kwani Pengo katajwa?
kanisa sio cuf,kutumia tricks za kuwaumiza cuf kwa kanisa catholic ni kama serikali kutaka kujimaliza wakati tayari ipo hai.