Pengo: Uovu ushindanishwe na Wema!

Pengo: Uovu ushindanishwe na Wema!

Status
Not open for further replies.

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Policarp Kadinali Pengo amesema kuwa wakristo washinde uovu kwa uovu. Lakini, washindanishe wema pale kwenye uovu.

Anayasema hayo sasa Arusha kwenye Misa takatifu ya mazishi ya wahanga wa bomu la Parokia ya Olasiti Arusha. 'Msishindane uovu kwa uovu' anasema Kadinali Pengo. Mahubiri yake yanaendelea. Anazungumza taratibu lakini kwa umakini mkubwa
 
'Tusidiriki kulipia ovu juu ya ovu.Lakini tutende mema ili kusahihisha uovu. Hii haina maan kuwa majukumu ya Serikali hayapo katika mambo kama haya.Sitaki kuikumbusha Serikali majukumu yake.Tusilipe ovu kwa ovu' anaongeza Kadinali Pengo
 
'Uovu huu udhibitiwe haraka kulinusuru Taifa letu lisisambaratike. Wenye mamlaka watekeleze wajibu wao.Taifa letu lidumukatika umoja na amani.'anasema Kadinali Pengo
 
Kadinali Pengo amemaliza mahubiri yake kwa ujumbe wake mfupi: tusilipe ovu kwa ovu;uovu udhibitiwe;Serikali itemize wajibu wake kudhibiti uovu
 
By the the rivers of Babylon
There we sat
When we remember Zion...
 
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Policarp Kadinali Pengo amesema kuwa wakristo washinde uovu kwa uovu. Lakini, washindanishe wema pale kwenye uovu. Anayasema hayo sasa Arusha kwenye Misa takatifu ya mazishi ya wahanga wa bomu la Parokia ya Olasiti Arusha. 'Msishindane uovu kwa uovu' anasema Kadinali Pengo. Mahubiri yake yanaendelea. Anazungumza taratibu lakini kwa umakini mkubwa

AMESEMA MTUME S.A.W '.... Na libadili ovu kwa jema lile jema litafuta ovu na uchangamane/uishi na watu kwa tabia nzuri' naona Askofu kalachabo kwenye vitabu vya hadith za mtume muhammad s.a.w. Inapendeza sana. Viva baba Askofu.
 
Warumi waliwatesa wakristo karne tatu, lakini Mungu aliwakomboa kutoka mikononi mwa wadhalimu
 
Zion train is comin our way,oh people get on board,you better get on board,thank the Lord.....
 
Mimi nawaambia "Tujifunze kutoka kwa Bwana wetu Yesu Kristo: 'Tusidiriki kulipia uovu kwa uovu, lakini tutende mema ili kushinda uovu'."

Lakini haya hayaondoi majukumu ya serikali, ambayo yanabaki, na si mimi ninayepaswa kuyasema, wenye mamlaka wanayajua majukumu yao. Mimi nawaambia ninyi waumini.

Uovu si kitu kinachopendeza. Warumi waliwatesa wakristo kwa karne tatu, na haikusaidia chochote Himaya ya Warumi, ambayo baadaye ilisambaratika. Lakini imani yetu imebaki.

 
Nimeguswa. Wakristu wengi tunamwangalia Baba Kadinali kwa majibu ya kinachofuatia au msimamo mkali wa Kanisa dhidi ya wadhalimu hawa lakini yeye amewajibika kwetu kiroho nami na ninaamini na Wakristu wengine nimepata faraja
 
KWELI ULIOSEME YANATUFARIJI SANA BABA Kardinali. poleni sana wafuasi wote YESU kwa yaliyotokea huko ARUSHA.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom