Msiwe wabishi, Polycarp Cardinal Pengo alishajiuzulu na hayumo tena madarakani

Mdanganywa

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
592
500
Kuna watu bado hawaamini kwamba Polycarp Cardinal Pengo hayumo tena madarakani na lakini bado wanaendelea kumtukuza huenda asisahaulike.

Ukitembelea baadhi ya Parokia na nyumba za kanisa bado picha ya Polycarp Pengo inaonekana kana kwamba yeye ndiye askofu wa D'Salaam.

Halafu jimbo la D'Salaam limeanzisha mtindo ambao haupo kabisa. Misa inapofika ile sehemu ya kumtaja askofu huwa tunasema "Yaani mtumishi wako Baba Mtakatifu Francis na askofu wetu Jude Thadaues na askofu msaidizi Eusebius".

Sasa siku hizi baadhi ya parokia za D'Salaam zimebuni zikisema "na askofu wetu mstaafu Polycarp Cardinal Pengo".

Sijui hii wamefundishwa na nani tena nimeisikia ikitamkwa palepale St. Joseph ambako ni makao makuu ya kanisa.

Nasema hivi kwamba hii haitakiwi. Maadam Pengo ameshajiulu hatakiwi kabisa kufanyiwa hayo na hastahili.

Tukianza na picha, picha iliyopo ni picha ya Papa Francis wala hakuna picha ya Papa Benedict XVI aliyejiuzulu. Hata ile sala hatusemi "na Papa Mstaafu Benedict XVI" tunaishia kumsema Francis tu.

Hivyo, tukumbushane ukweli. Picha ya Polycarp Pengo iondolewe kwenye ofisi zote za jimbo la D'Salaam kama ilivyoondolewa ya Lebulu (Arusha), Mtega (Songea), Msarikie (Moshi), Butibubage (Mwanza), Papa Benedict XVI (Roma).

Na ile sala Pengo asitamkwe kwani hastahili kama ambavyo hatumtamki Papa Benedict XVI.

Kukumbishana ni vizuri. Jadili kwa hoja.
 
Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
21,556
2,000
Nijuavyo mimi Kardinali wa Tanzania ni P. Pengo, na huyu ndiye atashiriki kwenye kupiga kura ya Papa mpya huko Roma kama ikihitajika kufanya hivyo.

Labda unachanganya kati ya Askofu Mkuu wa Jimbo la Dar na Kardinali!
 
The only

JF-Expert Member
May 19, 2011
5,469
2,000
Mstaafu wa nini?
Uaskofu mkuu wa jimbo la Dar (jimbo kuu) yeye ndiye kiongozi mkuu wa kanisa katoliki Tanzania. Pengo ni cardinal yaani anawakilisha mamlaka ya Papa kwa Serikali, kazi za Arch bishop wa main diocese ni kuongoza jimbo kuu la nchi na mwenyekiti wa maaskofu, kukusaidia cardinal ni kama Jafo na Makonda.

Makonda ndiye bosi wa Dar, ila Jafo yuko juu ya Makonda kiprotocal si kiutendaji level ya mkoa. Hivyo mtoa mada yuko sahihi anaetajwa kwenye sala na mlezi mkuu wa kanisa (mwenyekiti wa TEC) Ruw'aich ila Pengo ni kama mshauri mzee wa heshima barazani. Kura yake na askofu mkuu wa Iringa ni sawa barazani ndiyo maana Pengo hakuridhia waraka ule mchungu wa Serikali lakini alizidiwa kwa kura za wajumbe wengi Arch bishop huwa ni mmoja kwa nchi ila Makaldinali mfano Misri wako wa 3
 
Kawe Alumni

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
8,483
2,000
Pengo ni nembo ya Ukatholic Tanzania

Hawezi akaondolewa kizembe

Ni mtu muhimu sana
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
4,267
2,000
Pengo ni nembo ya ukatholic Tanzania

Hawezi akaondolewa kizembe

Ni mtu muhimu sana
Wewe utaendelea kubakia msukule milele! Haitakuja itokee siku ukarudi kuwa binadamu wa kawaida. Ccm wamekufanyia kitu kibaya sana. Sasa Pengo ana nembo gani ya Ukatoliki Tanzania! Ana umuhimu gani zaidi kwa kanisa la Tanzania kuliko Maaskofu wengine wanao endelea kuhudumu na pia wale waliostaafu?

Si bora hata ungemtaja marehemu Kardinali wa kwanza mzawa Laurean Rugambwa kuwa ndiye nembo ya huo Ukatoliki nchini! Au kwa sababu Kardinali Pengo wakati akiwa Askofu Mkuu alikengeuka na kujihusisha waziwazi na siasa za ccm, ukaona umzawadie hiyo hadhi ya kuwa nembo!!
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
4,267
2,000
Inakuaje katika sala anatajwa pengo au papa?

Inamaana watu huomba kutoka kwa hao watu?
Huo ndiyo utaratibu wa kawaida kabisa wa ibada za misa ya misa Takatifu ya kikatoliki kumuombea Baba Mtakatifu, Askofu wa Jimbo husika na Mapadre wake wote katika kuuendeleza Utume wa Yesu Kristu.

Tumsifu Yesu Kristu.
 
dindilichuma

JF-Expert Member
Dec 19, 2015
1,254
2,000
Ni lini Ruwaichi kawa mkuu wa Kanisa katoliki nchini? Nilini pia kawa mwenyekiti wa TEC?
Ruwaichi ni askofu mkuu wa jimbo kuu la Dar Kama alivyo askofu mkuu wa jimbo kuu la Songea Dalu.
Hana mamlaka na nchi ya Tanzania anamamlaka na jimbo lake na kila askofu anawajibika moja kwa moja kwa mamlaka iliyomteua.
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
4,267
2,000
Uaskofu mkuu wa jimbo la Dar(jimbo kuu) yeye ndiye kiongozi mkuu wa kanisa katoliki Tanzania. Pengo ni cardinal yaani anawakilisha mamlaka ya Papa kwa Serikali ,kazi za arch bishop wa main diocese ni kuongoza jimbo kuu la nchi na mwenyekiti wa maaskofu ,kukusaidia cardinal ni kama Jafo na Makonda ,Makonda ndiye bosi wa Dar ,ila Jafo yuko juu ya Makonda kiprotocal si kiutendaji level ya mkoa ,hivyo mtoa mada yuko sahihi anaetajwa kwenye sala na mlezi mkuu wa kanisa (mwenyekiti wa TEC) Ruw'aich ,ila Pengo ni kama mshauri mzee wa heshima barazani kura yake na askofu mkuu wa Iringa ni sawa barazani ndo maana Pengo hakuridhia waraka ule mchungu wa Serikali lakini alizidiwa kwa kura za wajumbe wengi arch bishop huwa ni mmoja kwa nchi ila makaldinali mfano Misri wako wa 3
Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, hajawahi kuwa Mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania. Yeye ni Mshauri tu wa Papa kule Vatican na pia anakuwa na hadhi ya kumchagua Papa Mpya.

Alipokuwa Askofu Mkuu wa Jimbo kuu Dsm, mamlaka yake huishia huko huko Dar! Maana kila Askofu ana mamlaka kamili ndani ya Jimbo lake! Wao huwajibika kwa Papa moja kwa moja na siyo Kardinali.

Na ukumbuke pia Maaskofu wote wa Katoliki nchini, humchagua rais wao kila baada ya muda fulani kuongoza baraza lao la Maaskofu (TEC), na ambaye hugeuka kuwa msemaji wao katika masuala mbalimbali.

Hivyo basi, iwapo ungesema rais wa TEC, ndiye Mkuu wa Maaskofu wote wa Katoliki Tanzania, ningekuelewa sana.
 
JFK wabongo

JF-Expert Member
Aug 11, 2015
3,755
2,000
Kuna watu bado hawaamini kwamba Polycarp Cardinal Pengo hayumo tena madarakani na lakini bado wanaendelea kumtukuza huenda asisahaulike.

Ukitembelea baadhi ya Parokia na nyumba za kanisa bado picha ya Polycarp Pengo inaonekana kana kwamba yeye ndiye askofu wa D'Salaam.

Halafu jimbo la D'Salaam limeanzisha mtindo ambao haupo kabisa. Misa inapofika ile sehemu ya kumtaja askofu huwa tunasema "Yaani mtumishi wako Baba Mtakatifu Francis na askofu wetu Jude Thadaues na askofu msaidizi Eusebius".

Sasa siku hizi baadhi ya parokia za D'Salaam zimebuni zikisema "na askofu wetu mstaafu Polycarp Cardinal Pengo".

Sijui hii wamefundishwa na nani tena nimeisikia ikitamkwa palepale St. Joseph ambako ni makao makuu ya kanisa.

Nasema hivi kwamba hii haitakiwi. Maadam Pengo ameshajiulu hatakiwi kabisa kufanyiwa hayo na hastahili.

Tukianza na picha, picha iliyopo ni picha ya Papa Francis wala hakuna picha ya Papa Benedict XVI aliyejiuzulu. Hata ile sala hatusemi "na Papa Mstaafu Benedict XVI" tunaishia kumsema Francis tu.

Hivyo, tukumbushane ukweli. Picha ya Polycarp Pengo iondolewe kwenye ofisi zote za jimbo la D'Salaam kama ilivyoondolewa ya Lebulu (Arusha), Mtega (Songea), Msarikie (Moshi), Butibubage (Mwanza), Papa Benedict XVI (Roma).

Na ile sala Pengo asitamkwe kwani hastahili kama ambavyo hatumtamki Papa Benedict XVI.

Kukumbishana ni vizuri. Jadili kwa hoja.
Ndugu inategemea na sala ipi ya Ekarist ilisomwa, zipo namba I - IV, nyingine ni flexible kuongeza na wastaafu ila nyingine zimebana. Hata hivyo Cardinal Pengo alishaimbiwa "Ndiwe kuhani hata milele kwa mfano wa Melkisedeki" hivyo anastahili kuendelea kumuombea.
Suppose Pengo akikengeuka na kuamua kuwa Mganga wa kienyeji, ni nini itakuwa impact yake kwenye ukatoliki? Acha aendelee kuombewa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom