Pengo na Maendeleo yaletwayo na CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pengo na Maendeleo yaletwayo na CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Feb 23, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hivi mtu kama huyu ambae anataka kuwashauri waTanzania juu ya kuendelea kuichagua CCM tumuelewe vipi ?

  Ni kweli wakatoliki wanaridhika na uongozi wa CCM ,Pengo kwa maoni yake ya kujipendekeza anaelekea kuigawa nchi maana unaposema utawashauri wakatoliki waipigie CCM kura tayari utakuwa umeshaitenga jamii ,Je asilimia kubwa ya kura wanazo wakatoliki , Pengo awache kujipendekeza kwa kuona yeye ndie anaewaelekeza watanzania wamchague nani ,huku ni kuwapotosha WaTanzania . Aidha ajijulishe kuwa yeye ni Mwanachama wa CCM hapo haitawezekana kumuingilia katika maamuzi yake ,hivi Mtanzania huyu anaweza kuwapigia makelele mafisadi ? Hivi Pengo anamwambia nini Kikwete juu ya mafisadi ?

  WaTanzania washauriwe kuchagua Chama kile ambacho kitawaletea maendeleo bila ya kushawishiwa wampigie nani kura ? WaTanzania washauriwe kuwa tayari kulinda kura zao zisiibiwe ,WaTanzania wapime na kuona utawala wa CCM umefikia wapi na unaelekea wapi.Pengo anaomba rushwa maana ukimwambia mtu tuzungumze vizuri ,kwa Tanzania ya leo inaeleweka umekusudia nini.
  ______________________________________________________

  Pengo alisema hayo mbele ya Rais Kikwete, marais wastaafu wa awamu ya pili na tatu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa Jaji Mkuu, Augustine Ramadhan na Spika wa Bunge, Samuel Sitta.

  Alitoa mfano kuwa ikiwa Rais Kikwete atahitaji kura za urais kutoka kwa waumini wa Katoliki nchini ni dhahiri kwamba atazungumza naye (Pengo) vizuri ili awashawishi waumini wa kanisa hilo wamchague.

  ``Ikiwa hivyo, mimi nitazungumza nao na kuwaambia, huyu ndiye wa kumchagua, utapata kura nyingi za Wakatoliki, lakini kama hazikuwa zinaridhia Watanzania kwa ujumla, kesho na keshokutwa hali itakuwa ngumu nchini,`` alisema

  _________________________________________________

  Yaani Pengo atawadanganya wakatoliki na kuwambia CCM ni Chama kizuri kipeni kura .
  Kasome utumbo wake kamili hapa ,hawa ndio waliotuambia kama ni chaguo la Mungu ,sasa wanasema maneno yao ni ya unabii :-
  http://ippmedia.com/ipp/nipashe/2009/02/23/132181.html
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ndg. Mwiba ni lini utaerevuka mkuu? Hizi point zote ulizozisema either hukuzielewa au um ezielewa kinyumenyume.

  BTW: Hivi ile ndoa na fiftini yurold gelo iliishia vipi :D?
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Sasa zieleze kimbembele wengine tielewe ila nilivyomuelewa kuwa jamaa ni pandikizi la CCM ndani ya wakatoliki ,safu nzima ya mijigogo ya CCM ipo kwenye meza kuu unategemea nini kama hayupo hapo kuwahakikishia kuwafanyia kazi yao.

  Kuhbtw: Nimemuelekeza asipeleke ada kwa muda wa miezi mitatu :D
   
 4. K

  Kaka Mdogo Member

  #4
  Feb 23, 2009
  Joined: Aug 4, 2008
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mwiba, inawezekana una hoja lakini umekurupuka na kuanza kutumia maneno ya ajabu ajabu kufikisha hoja yako. "Kasome utumbo wake kamili hapa ,hawa ndio waliotuambia kama ni chaguo la Mungu ,sasa wanasema maneno yao ni ya unabii" Sidhani kama Pengo aliongea utumbo. Alichokiongea anakimaanisha. Vilevile sijui kama umeisoma hotuba yote ya Mwadhama Kardinali Pengo kabla ya kuamua kuchagua kipande ambacho kilichaguliwa na Mashaka Mgeta (mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe). nina imani unaufahamu vizuri uandishi wa habari wa Tanzania. Unafahamu vizuri kila shirika la habai lina mlengo gani. Hii ndio Tanzania ya leo. lakini nikirudi katika hoja ya msingi, nina imani Kardinali Pengo aliongea mengi mazuri tu. Hilo lililokuudhi Pengo hajasema atawaambia Wakatoliki wampigie kura Kikwete. Kuna mambo mengi ambayo Kardinali Pengo anayaona kwa mtazamo wake, labda ndio mtazamo wa kanisa katoliki kwamba ni tatizo na kwamba kama yatarekebishwa basi yuko radhi kuwaambia wakatoliki wampigie kura. Kumbuka kuwa ukatoliki ni taasisi yenye viongozi wake na wafuasi wake kama zilivyo taasisi zingine za kidini na kijamii ambao wana haki ya kupiga kura na kuchagua kiongozi yoyote wa kisiasa. Sheria inaruhusu. Na kanisa linaweza kuweka msimamo wake na hakuna sheria inayowakataza. Wana uwezo wa kuitumia haki yao ya kupiga kura kwa matakwa na utashi wao. Wanaweza kusema wameongozwa na roho mtakatifu kwa imani yao na kusema kiongozi bora na anayefaa kupigiwa kura (as per the holy spirit) ni fulani. Na Viongozi wa dini wana uwezo mkubwa wa ku influence maamuzi ya wafuasi wao. Kwahiyo hilo la Pengo kuwaomba wakatoliki kumpigia kura Kikwete linawezekana. Kulingana na sentensi uliyopigia mstari issue kubwa kwako ni mtu atayepigana na kuwapigia kelele mafisadi. Ukishawapigia makelele so what??? ukishawaambia nyie ni mafisadi so what? ukishawapeleka mafisadi mahakamani na wakafungwa bila kurudisha hicho kilichowafanya wawe mafisadi so what? hizo ni siasa za kulipiza kisasi. Tatizo la nchi ya Tanzania siyo mafisadi bali mfumo mzima wa utawala. Kwani sasa hivi watu wanaogopa kuiba kwa sababu watu wamepelekwa Kisutu?? kuna uchafu mwingi unaendelea kwa sababu mfumo mzima uko legelege! Sheria zina mianya mingi, watendaji hawajui wanachofanya, serikali haijui watanzania wanataka nini, mwisho wanaishia kuyafanyia kazi majungu kwa kutumia pesa nyingi za walipa kodi. Tanzania ya leo tunataka kumuona rais yuko busy kwenye majukwaa na Ikulu akifanya vikao na DPP, DCI, TAKUKURU, AG ili watu wapelekwe mahakamani. Wanaoshangilia na hao kupelekwa mahakamani ni group ndogo ya watu wa oysterbay, masaki na mbezi beach. Nachingwea, sengerema, babati, bombo, uyui, kasenene, tandale, msondo primary schools, hawahitaji siasa za mafisadi, bali maji, madawa, wataalamu wa kilimo na mifugo, mabarabara, mitaji kwa njia ya mikopo yenye masharti nafuu, soko la mazao yao, walimu, ajira hata za kima cha chini cha mshahara, umeme, na kubwa zaidi UTU wao. Vyote havipatikani kwa watu kupelekwa kisutu. Kama rais ningesema 'kuna mamlaka zilizoundwa kisheria kushughulikia makosa kama hayo ya ufisadi, watanzania hawakunituma kuja kuwashughulikia mafisadi bali kuwasaidia ili wafikie malengo yao ya kimaendeleo!
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Feb 23, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kwa hili sina msaada, maana mwenye macho ameshaona, tena na source umetuwekea mwenyewe!

  Aisee kumbe wewe ni mpinga maendeleo! Ila sikutegemea jibu la maana, maana hata posts zako zimekaa kihivyohivyo!
   
 6. AljuniorTz

  AljuniorTz JF-Expert Member

  #6
  Feb 23, 2009
  Joined: Jan 6, 2009
  Messages: 544
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Huyo ndio Askofu Mkuu wa wakatoliki.

  Cku zote akizungumza unaweza kudhani anapenda maendeleo ya watanzania but kwa upande mwengine anapenda watz wadumae daima dumu chini ya ccm (anapenda watawale daima)

  Huyu huyu amemsifia Mkapa kwa kulinda amani ya tza but wale wananchi wa pemba waliouwawa wkt wa uchaguzi uliomuingiza kikwete madarakani. Sasa amani anayoiona na kuitafsiri pengo ni kutokuwa kupigwa au kuuwawa kwa wakristo. Wakati wa mkapa ndio kilikuwa kipindi kikubwa cha ufisadi na ujambazi wa hali ya juu kutokea tza, mifano mnayo ya wazi.

  Kwa mtazamo wangu, oengo ni kiongozi mwenye double standard.

  Thnx
   
 7. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #7
  Feb 23, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Naona Kaka Mdogo una jazba ,tafadhali tenganisha cheo cha mheshimiwa Pengo ,hotuba ya pengo ipo wazi kisiasa kuliko kidini,Pengo amerusha dongo kusema serikali imekumbatia au ikikumbatia dini moja ,hapo ameihadharisha serikali na madai ya Waislamu,mimi sikutaka kwenda huko ila pale aliposema serikali izungumze nae ili aipigie debe.
  Inaonyesha unakanusha aliyosema Pengo (Samahani huwa sipendi kuweka vibwagizo kama kutumia maneno Muheshimiwa ,Raisi ,Mwenyekiti ,Shehe au Mwenye upawa ndani ya siasa naamini tukianza kuitana hivyo tutaogopana badala ya kuheshimiana).

  Pengo anaonekana kujilinda kwa wananchi pale aliposema ni yuleyule wa zamani,Pengo anaonyesha woga pale anaposema kumwambia raisi kuwa utaitwa Dikteta ,kwa maana nyingine anamwambia au anaiambia serikali usiyape uhuru magazeti akimpiga dongo Mengi na wengineo ,upo ,risala ya Pengo imejaa undani ndugu kama utaisoma kwa kuwa tu wewe ni mkatoliki na unaridhia yale ayasemayo Mkuu Pengo hapo patakuwa poa,ila kama unaisoma hotuba yake kisiasa basi inatakiwa uitazame kisiasa ndipo utamuelewa jamaa ana muelekeo gani ndani ya siasa za Tanzania inayozama na kuzamishwa.
  Mwengine anasema pengo ni kama Baba yetu ,jamani tukishaanza kuonana kinamna hivyo mjue hatufiki mbali, WaTanzania walio wengi wapo ndani ya mapambano kujiokoa nafsi zao na vizazi vyao ,hivyo haitokuwa vizuri viongozi wa kidini wakaanza kuweka chokochoko ,kama mlivyoona alipogusia mambo ya vyombo vya habari ,ujue hata JF imo humo ,sasa siajabu JF ikawa blocked ndani ya Tanzania ,itatubidi tutumie njia za panya.Mimi siiungi mkono hotuba yake kwani ni ya kujidhalilisha na utaona namna wanavyopakana siagi ,Pengo anapaka kivyake na Kikwete anapaka kivyake ,katika kutafuta maelewano.
   
 8. AljuniorTz

  AljuniorTz JF-Expert Member

  #8
  Feb 23, 2009
  Joined: Jan 6, 2009
  Messages: 544
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Je, kushamiri kwa ujambazi ndio kuwa na amani? wananchi kuwa kuishi maisha ya dhiki na mashaka ndio amani? kuwepo kwa pengo kubwa kati ya wenye nachi na maskini wa kutupwa ndio amani?

  TAFAKARI MWANANCHI WA TZA, BAADHI YA VIONGOZI WETU WA DINI NA WANASIASA WANATUPELEKA PABAYA SANA, TUWE MACHO NA KAULI ZAO NA MATENDO YAO.
   
 9. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #9
  Feb 23, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Serikali ikikumbatia dini moja hatari - Pengo

  2009-02-23 10:03:38
  Na Mashaka Mgeta


  Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amemuonya Rais Jakaya Kikwete kuwa majadiliano kati ya serikali na upande mmoja na waumini wa dini moja yanaweza kuhatarisha amani nchini.

  Akizungumza katika hafla ya kumpongeza kwa kutimiza miaka 25 ya utumishi wake akiwa askofu juzi usiku jijini Dar es Salaam, Kardinali Pengo alisisitiza kuwa majadiliano yoyote yenye maslahi ya taifa yanapaswa kuhusisha viongozi wa madhehebu ya dini zote nchini.

  Alisema kuwapo kwa majadiliano yenye lengo la kufanikisha upande mmoja (wa dini), inaweza kusababisha hasara kwa taifa endapo amani itatoweka.

  Pengo alisema hayo mbele ya Rais Kikwete, marais wastaafu wa awamu ya pili na tatu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa Jaji Mkuu, Augustine Ramadhan na Spika wa Bunge, Samuel Sitta.

  Alitoa mfano kuwa ikiwa Rais Kikwete atahitaji kura za urais kutoka kwa waumini wa Katoliki nchini ni dhahiri kwamba atazungumza naye (Pengo) vizuri ili awashawishi waumini wa kanisa hilo wamchague.

  ``Ikiwa hivyo, mimi nitazungumza nao na kuwaambia, huyu ndiye wa kumchagua, utapata kura nyingi za Wakatoliki, lakini kama hazikuwa zinaridhia Watanzania kwa ujumla, kesho na keshokutwa hali itakuwa ngumu nchini,`` alisema.

  Kardinali Pengo alisema viongozi wa dini wana wajibu wa kutoa sauti za kinabii katika jumuiya za watu, hivyo sauti hizo haipaswi kuzuiwa.

  ``Haitakuwa kitu kizuri kuzizima sauti hizo kwa sababu yoyote, iwe ya kisiasa, kiuchumi ama vinginevyo,`` alisema.

  Pengo alisema kuna haja ya kupima sauti za unabii, kwa kuwa baadhi ya watu wanatumia mwanya huo kwenda kinyume, ikiwa ni pamoja na kusababisha mafarakano.

  Siku zote dini zina wajibu wa kutekeleza jukumu la unabii wa kweli, kamwe dini zisitumike kama chombo cha siasa,`` alionya.

  Kuhusu madai kwamba kuanzia siku za hivi karibuni amepunguza kukemea maovu katika jamii, Pengo alisema msimamo wake bado uko pale pale.

  ``Pengo wa zamani ni yule yule aliyepo leo, tofauti inayoonekana ni kutokana na mabadiliko ya siasa nchini,`` alisema.

  Alisema mfumo wa sasa unatawaliwa na vyama vya siasa kumiliki ama kuwa na uhusiano na vyombo vya habari, hivyo anapokemea jambo baadhi ya vyombo hivyo haviandiki ili kulinda maslahi ya vyama husika.

  ``Sijapunguza kukemea mambo yasiyokuwa mazuri naposema lakini jambo lenyewe likawa halipendwi la chombo fulani cha habari, halitakichapisha,`` aliongeza.

  Kwa upande mwingine, Kardinali Pengo alionya matumizi mabaya ya baadhi ya vyombo vya habari kwa kuwa vinaifarakanisha jamii badala ya kuiunganisha.

  Alisema kwa maana hiyo serikali inapaswa kuepuka hali ya kutenda majukumu yake kutokana na taarifa za vyombo hivyo.

  ``Usipokuwa makini (Rais), Taifa litaongozwa na magazeti…sisemi uyafungie, utaitwa dikteta, cha msingi tuwe waangalifu, tusiruhusu taifa likaongozwa na vyombo vya habari, ni jambo la hatari,`` alisema.

  Awali akizungumza katika hafla hiyo, Rais Kikwete alisema Kardinali Pengo ni nyenzo muhimu katika kushamirisha mazingira ya amani, maelewano na utulivu nchini.

  Alisema kauli za Pengo mara kwa mara hazitoki kwa kukurupuka, bali zinatawaliwa na kiwango cha juu cha kutafakari kabla ya kutamka.

  ``Kwa maana usipojipa muda wa kufikiri, matokeo yake ni kukurupuka, kuropoka na baadaye kujutia…wewe ni msikivu, mpole, mvumilivu, unatafakari kabla ya kuamua, haukurupuki,`` alisema Kikwete.

  Alisema Pengo licha ya kuwa kiongozi wa dini nchini, amechangia pia maendeleo na huduma za jamii, bila kujali tofauti za kiimani.

  ``Umefanikisha pia maelewano miongoni mwa waumini wa dini zote, hauna sifa ya ubaguzi kama ilivyo kwa viongozi mbalimbali wa dini na hata wanasiasa,`` alisema.

  Rais Kikwete alisema ubaguzi wa kidini ni miongoni mwa hatari kubwa zinazoweza kuliangamiza taifa tofauti na ulivyo ukabila.

  ``Ukabila si tisho, bali kwa eneo dogo, lakini udini unaweza kuliyumbisha taifa, ukawa kama baruti ya kuwasha moto usiozimika, tukiwa na viongozi wa aina yako nchi inaepuka hatari hiyo,`` alisema.

  Naye Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Askofu Alex Malasusa, alisema Pengo anatambuliwa na kuheshimika kama kiongozi wa madhebu ya kikristu nchini na si Wakatoliki pekee.

  ``Viongozi wa madhehebu tunamuona Pengo si kwa ajili ya Wakatoliki tu, bali mshauri na mwenye kuleta ujumbe wa Mungu kwa viongozi wa dini zote ni kama baba yetu,`` alisema.

  Hafla hiyo, ilihudhuriwa na maaskofu wakuu na maaskofu wa kawaida (Wakatoliki) kutoka Malawi, Burundi na Tanzania, watawa na waumini wa kawaida.

  Pengo pia alikuwa anatimiza miaka 38 tangu kupata daraja la upadre na miaka 10 alipoteuliwa na Baba Mtakatifu Yonane Paul II kuwa Kardinali.

  SOURCE: Nipashe

  Tuma Maoni Yako
   
 10. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #10
  Feb 23, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Ninachokiona kwenye matamshi ya Padre/Askofu/Kadinali muadhama Policarp Pengo ni matamshi ya kawaida ya watumishi wa mungu hasa wanapoona kuna kaharufu ka kondoo wake kuibiwa au hata kuasi na kuwa hawashikiki.

  Tanzania kikatiba haina dini japo raia wake wanadini, hivyo kwa kuwa ni watanzania ndiyo wanachagua viongozi wa taifa lisilo na dini, basi kinachoonekana katika matamshi ya muadhama hakina tofauti na vile vikundi vya kina Sheikh Ponda ambao wanatumia dini kama mtaji wa kisiasa. Na ikifika mahali watanzania wakaanza kujua kuwa Chama fulani kinapigiwa chapuo na viongozi wa dini basi chama hicho hakina muda kitapoteza uongozi wa nchi au hakitashika uongozi kabisa.

  Kuiambia serikali ya CCM kuwa ikitaka kura za wakatoliki basi funguo ya kura hizo anayo Pengo ni kukosa ule muendelezo na utamaduni aliotuachia baba wa Taifa kuwa Nchi haina dini. Na je Sheikh mkuu naye akiwaambia CHADEMA au CUF au TLP kuwa funguo za kura za waislamu anazo yeye nchi itafika wapi?

  Mtazamo wangu ni kuwa Pengo yeye aendeleze kutoa huduma ya kiroho na kazi ya kuomba kura awaachie wanasiasa wenyewe kama kweli anataka maneno yake ya kutetea amani yawe na uzito, vinginevyo ni kugawa nchi katika Ukatoliki na wasio-katoliki kwa kuonesha kuwa yeye ni mshabiki wa CCM ila pale tu serikali itakapozungumza nae, sijui kivipi anajua yeye na roho mtakatifu aliyemshukia na kumfanya azungumze haya(hii haina tofauti na yule padre wa Katoliki Marekani aliyewaambia waumini wake kuwa kama umempigia kura Obama hustahili kupewa communion). Katika kanisa Katoliki kuna waumini wenye itikadi za vyama mbalimbali (CCM, CHADEMA, TLP, CUF, SAU etc). Kuchukua one side ni kuwatenga wale wasioamini itikadi za CCM. Sasa sijui atawatangaza hawa wasio wana CCM ndani ya kanisa Katoliki kuwa hawatauona ufalme wa mbinguni wasipoipigia kura CCM kama serikali ikiamua kuzungumza na Mudhama, baba askofu Pengo. Kazi ipo, maana sasa watanzania tunapigiliwa kotekote linapokuja suala la maendeleo yetu ya hapa duniani ambayo ni ya mpito tu, maendeleo ya kweli ni kupewa huduma ya kiroho itakayotuwezesha kupata makazi bora ya peponi mbele ya mungu.
   
  Last edited: Feb 23, 2009
 11. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #11
  Feb 23, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Sijui kwa nini umeamua kwa makusudi mazima kupindisha ukweli wa mambo kuhusu hii vita tuliyo nayo dhidi ya wahujumu wa taifa. Wanaoshangilia kupelekwa mahakamani kwa wezi na mafisadi nchini si watu wa Oysterbay, Masaki na Mbezi beach kama unavyotaka tuamini. Wanaoshangilia ni watu wa Nachingwea, sengerema, babati, bombo, uyui, kasenene, tandale, msondo primary schools kama ulivyoorodhesha.

  Hawa ndio wanahitaji maji, madawa, wataalamu wa kilimo na mifugo, mabarabara, mitaji kwa njia ya mikopo yenye masharti nafuu, soko la mazao yao, walimu, ajira hata za kima cha chini cha mshahara, umeme, na kubwa zaidi UTU wao. Vyote hivyo naamini vingepatikana kama Mafisadi hawangekwapua mabilioni kupitia Richmond, EPA, Deep Green, Tangold, Meremeta, IPTL, Radar, Ndege ya Raisi, ATCL, Minara Pacha ya Benki Kuu n.k.

  Kaka Mdogo, pamoja na kwamba yawezekana Mwiba kapotoka kwa kiasi fulani, lakini ukweli ulio wazi ni kuwa taasisi za dini zimetoa mchango usioridhisha kwenye vita dhidi ya uovu ndani ya jamii. Dini haitakiwi kufumbia macho mapungufu ya utawala ambayo yanaonekana wazi hata kwa kipofu, kwamba yanawaathiri waumini wake. Kanisa Katoliki lina nafasi kubwa hapa badala ya kukumbatia viongoji ambao wametuhumiwa kuhusika na athari hizi.

  Toka kashfa hizi zimeanza kuanikwa, Taasisi za dini zimekuwa kama zimemwagiwa maji baridi lakini ndizo zilizokuwa msitari wa mbele kumpigia kampeni Kikwete kuwa ni chaguo la Mungu. Huu ndio ukweli na kama viongozi wa Kanisa wangekuwa na uchungu na mateso wanayopata wengi wa waumini wao hivi sasa, wangewaomba msamaha kwa hilo. Kwao kukaa kimya kunajenga hisia kuwa Kanisa lina maslahi ndani ya chama cha CCM.

  Tulishuhudia kwa jirani zetu Kenya jinsi Kanisa Katoliki ilivyoleta utengano na uhasama baina ya waumini wake kwa kukosa msimamo sahihi dhidi ya maovu. Viongozi wa dini wana uwezo mkubwa wa ku"influence" maamuzi ya wafuasi wao. Kwa hiyo hilo la Pengo kuwaomba wakatoliki kumpigia kura Kikwete ni jambo la hatari na lisilokubalika hata kidogo. Yeye afanye hivyo kwa nafsi yake binafsi kama Pengo lakini kamwe asitumie jukwaa la Kanisa.
   
 12. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #12
  Feb 23, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kama nimepotoka sawa na niendelee hivyo hivyo,maana ukipenda hata chongo utaliona kengeza ,ila Mkuu amekosea na aidha dhamira yake ni kutaka kuvutwa kwenye jukwaa baada ya kuonekana hapo kale kuwa mtu mwenye msimamo mkali ,si tunawajuaga CCM wakikuona mkali mkali hukutafutia kamati na cheo juu yake wakakwambia hebu tulia .

  Pengo amezidi kujipendekeza alipovikandia vyombo vya habari , jicho la walala hoi ,jicho ambalo ndio taa ya kuwamulika viongozi wazembe na wababaifu ,ndio jicho ambalo linatakiwa kuwa mstari wa mbele kuwaonyesha waonyesha na kuwasomesha wananchi juu ya mienendo ya viongozi walioko madarakani ,kufika kusema kumwambia Kikwete itafikia kuitwa dikiteta maana yake nini ?

  Kama hali ya Kikwete ikionekana ya kidikiteta ataitwa dikiteta hakuna mjadala na hilo ,dalili za kuwa Kikwete ni dikiteta zimeanza kuonekana alipokwenda Zanzibar na kuwambia wapinzani wasahau ushindi , unafikiri hapo kuna nini ndani yake ? Wapinzani msahau ,chagueni wabunge wawakilishi lakini huku kweye uraisi hapishwi mtu ? Kikwete amekusudia nini hapo ,iwe watu wajikusanye wachague lakini yeye hatoki ,ndio maana yake ,ametegemea Ujemedari au sio ? 10yrs au sio ,kwa walivyojiekea haondoki mtu ndani ya miaka mitano, itakuwa ni aibu ,hashindwi mtu ndani ya miaka mitano ,ndio maana yake ,CCM itatawala milele fanyeni mtakavyo ndio maana yake ,kwani alisema kwa miaka ya karibu msitegemee ushindi au hamtoupata kabisa , halafu Pengo anamwambia Kikwete tuzungumze !!! Wazungumze nini ? Kipi cha kuzungumzwa ? Namna ya kuiba kura au namna ya kupanga majeshi na mapolisi ? Au namna ya kupanga matokeo ? Au kurahisisha mambo ?
   
 13. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #13
  Feb 24, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kanisa liliingiliwa muda mrefu uliopita mnaona leo?

  Hawa ndio wanamwalika Mkapa na kukaa naye meza kuu,mafisadi ndio watoa sadaka wakubwa hivyo haw3awezi kamwe kuwakemea . OLE WAO SIKU YAO INAKUJA YA KULIA NA KUSAGA MENO.
   
 14. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #14
  Feb 24, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Naona unawatolea mistari , hawa ni mamluki tu hawana tofauti na wale wa Bakwata.
   
 15. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #15
  Feb 24, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kazi ya viongozi wa dini ni kukemea maovu yanayofanywa na watawala na sio kukaa na kuwapigia makofi.

  Kazi ya viongozi wa kweli wa dini ni kusema ukweli hata kama ukweli huo utayagharimu maisha yake , kwani heri walio wasafi maana wataweza kuzionja mbingu.
   
 16. K

  Kwaminchi Senior Member

  #16
  Feb 25, 2009
  Joined: Dec 30, 2007
  Messages: 154
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Mwadhamu Pengo ni matokeo ya jinsi alivyolelewa tangu awamu ya kwanza. Baada ya kifo cha Mwlimu, huyu jamaa kaota pembe. Wamemwendekeza na kumdekeza, sasa kafia wakati, anathubutu kumtishia nyau Rais wa nchi, kuwa hawezi kushinda kama hatamwendea yeye.
  Ukishangaa ya Musa, subiri ya Firauni.
   
 17. K

  Kwaminchi Senior Member

  #17
  Feb 25, 2009
  Joined: Dec 30, 2007
  Messages: 154
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Mwadhamu Pengo ni matokeo ya jinsi alivyolelewa tangu awamu ya kwanza. Baada ya kifo cha Mwlimu, huyu jamaa kaota pembe. Wamemwendekeza na kumdekeza, sasa kafikia wakati, anathubutu kumtishia nyau Rais wa nchi, kuwa hawezi kushinda kama hatamwendea yeye.
  Ukishangaa ya Musa, subiri ya Firauni.
   
 18. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #18
  Feb 25, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Pole sana ndg, hapan shaka uelewa ni kitu muhimu sana, sikuwa najua.
   
 19. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #19
  Feb 25, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Unatumia basis gani kusema hasemi ukweli?
   
Loading...