kufufua wafu wa kiroho, lakini sio wafu wa mwili!!!Tatizo lako ni kuwa umezoea mafundisho manyonge na ukiona yale ambayo Biblia imeagiza watumishi wa Mungu watende unadhani ni nguvu za giza. Hauna tofauti na mafarisayo ambao walipoona Yesu anaponya wagonjwa, anatoa pepo na kufufua wafu wakasema anatumia nguvu za giza (Belzebubu).
Maandiko yako wazi kuwa mtu akimwamini Yesu kazi alizofanya Yesu na zaidi ya hizo atafanya. Yesu alitoa pepo, alifufua wafu na kuponya wagongwa. Kwa hiyo wanaomwamini Yesu nao wamepewa mamlaka ya kutenda miujiza ikiwemo kufufua wafu, kuponya magonjwa na kutoa pepo (Mathayo 10:2-8).
Pengo hana mamlaka yeyote kuwaonya wale wanaotenda miujiza kwa jina la Yesu. Yeye ni kiongozi wa dini ya Katoliki na nadhani alikuwa anawaonya washirika wake. Tusidanganyike kwa kufuata maneno matupu ya watu wanaojiita watumishi wa Mungu wakati hawatendi yale Mungu anayoagiza watumishi wake watende. Na kama sisi tumeshindwa kutenda miujiza tusianze kuwabwatukia wale wanaoitenda kwa Jina la Yesu. Kwa taarifa yako Mungu bado anatenda miujiza (ikiwemo kufufua wafu) na anawatumia watu wa kawaida.
kufufua wafu wa kiroho, lakini sio wafu wa mwili!!!
Lakini kama Mungu kasema anaweza kuponya watu, kwa nini iwe muujiza? Muujiza ni nini hasa???
Wednesday, 07 July 2010 21:07
Gazeti la mwananchi.
Geofrey Nyang'oro
ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo , amewaasa viongozi wa kanisa hilo kuepuka mafundisho ya upotoshwaji yenye lengo la kujitafutia sifa akidai mafundisho ya aina hiyo ni hatari kwa ustawi wa kanisa la Mungu.
Askofu huyo alitoa kauli hiyo kwenye ibada ya misa takatifu ya upadirisho wa mapadri watatu wa kanisa hilo iliyofanyika jana katika Parokia ya Kristu Mfalme ya Tabata jijini Dar es Salaam.
Alisema katika karne hii, wapo watu wanaoweza kufikiria kutumia nafasi walizonazo kufundisha neno la Mungu kwa lengo la kutafuta umaarufu miongoni mwa jamii na kwamba vitendo hivyo ni hatari kwa ustawi wa kanisa.
Kauli hiyo aliitoa wakati Watanzania wa sasa wanashuhudia kuibuka kwa madhehebu na wahubiri wa aina mbalimbali ambapo baadhi yao wanajitangaza kuwa wana uwezo wa kufanya miujiza ya kutisha ikiwemo ya kufufua wafu, upako katika biashara, kuondoa mikosi, kurudisha ndoa, kufaulu mitihani , na hata kufanikiwa katika masuala ya kutafuta kazi.
Baadhi ya viongozi wa madhehebu hayo wanaomba kwa kupayukapayuka kinyume cha maagizo ya Mungu kupitia kwenye Biblia Takatifu ambamo ameagiza sala zote zifanywe kwa unyenyekevu na hata kwa siri kwa kuwa yeye anaona yote ya siri...
Pengo alisema viongozi wa kanisa wawe tayari kuteketea kama chumvi inayoyeyuka kwa ajili ya kunogesha radha ya chakula.
"Maaskofu, Mapadiri na Mashemasi, ninyi mnapaswa kuwa chumvi na si mawe, chumvi ni kiungo kinachotumiwa katika kunogesha radha ya chakula, kiungo hiki hukubali kuteketea na kupoteza hata uhalisia wake ingawa uwepo wake huonekana kwenye ladha ya chakula,"alisema Pengo.
KWA HIYO?: suala langu wana jf ni hapo pekundu, je hawa viongozi wa dini za kisasa sio sawa na waganga wa kienyeji tunaowasikia kila siku uswazini? hivi ni kweli wana uwezo wa kutenda mambo hayo?
kufufua wafu wa kiroho, lakini sio wafu wa mwili!!!
Lakini kama Mungu kasema anaweza kuponya watu, kwa nini iwe muujiza? Muujiza ni nini hasa???
Tatizo lako ni kuwa umezoea mafundisho manyonge na ukiona yale ambayo Biblia imeagiza watumishi wa Mungu watende unadhani ni nguvu za giza. Hauna tofauti na mafarisayo ambao walipoona Yesu anaponya wagonjwa, anatoa pepo na kufufua wafu wakasema anatumia nguvu za giza (Belzebubu).
Maandiko yako wazi kuwa mtu akimwamini Yesu kazi alizofanya Yesu na zaidi ya hizo atafanya. Yesu alitoa pepo, alifufua wafu na kuponya wagongwa. Kwa hiyo wanaomwamini Yesu nao wamepewa mamlaka ya kutenda miujiza ikiwemo kufufua wafu, kuponya magonjwa na kutoa pepo (Mathayo 10:2-8).
Pengo hana mamlaka yeyote kuwaonya wale wanaotenda miujiza kwa jina la Yesu. Yeye ni kiongozi wa dini ya Katoliki na nadhani alikuwa anawaonya washirika wake. Tusidanganyike kwa kufuata maneno matupu ya watu wanaojiita watumishi wa Mungu wakati hawatendi yale Mungu anayoagiza watumishi wake watende. Na kama sisi tumeshindwa kutenda miujiza tusianze kuwabwatukia wale wanaoitenda kwa Jina la Yesu. Kwa taarifa yako Mungu bado anatenda miujiza (ikiwemo kufufua wafu) na anawatumia watu wa kawaida.
Alisema katika karne hii, wapo watu wanaoweza kufikiria kutumia nafasi walizonazo kufundisha neno la Mungu kwa lengo la kutafuta umaarufu miongoni mwa jamii na kwamba vitendo hivyo ni hatari kwa ustawi wa kanisa.
Kauli hiyo aliitoa wakati Watanzania wa sasa wanashuhudia kuibuka kwa madhehebu na wahubiri wa aina mbalimbali ambapo baadhi yao wanajitangaza kuwa wana uwezo wa kufanya miujiza ya kutisha ikiwemo ya kufufua wafu, upako katika biashara, kuondoa mikosi, kurudisha ndoa, kufaulu mitihani , na hata kufanikiwa katika masuala ya kutafuta kazi.
Huwa natatizika sana na baadhi ya vitendo na maombi yanayofanywa na baadhi ya wahubiri kwa sababu zifuatazo na Mungu anisamehe kama nakosea:
1.Binadamu kupitia wakati mgumu - iwe ni magonjwa, kifo, kukosa kazi, matatizo ya ndoa nk ni kitu cha kawaida kisichokwepeka. Iweje basi binadamu atake kubadilisha hali ya ubinadamu na kufanya kama vile dunia ni paradiso? Utaweza kumlazimisha Mungu kujibu ombi lako au kutenda kama mganga wa kienyeji?( ati watu wananunua vitambaa vye upako, wanapakwa mafuta sehemu mbalimbali za miili yao ili kupata majibu kwa yanayowatatiza).Inawezekana kabisa kuondoa mepepo kwa mambo hilo sibishi maana hayo ni mambo ya ulimwengu wa kiroho.Lakini hainiingii akilini ati kwenda kuombewa wakati naumwa jino kwa sababu limeoza, au naumwa malaria shauri ya kuumwa na mbu waletao malaria, au kuumwa tumbo shauri ya uvimbe wa fibroids kwa akina mama - haya yote ni magonjwa yenye tiba na Mungu kaweka kipaji cha uponyaji kupitia waliosomea kama madaktari. Sasa kama kila mtu ataombewa, madaktari wakikosa kazi nao wataombewa wapate kazi gani ilhali walisomea taalamu ya utababibu? ( Naombeni mnieleweshe vizuri kwenye hili)
2. Kwanini kumezuka madhehebu mengi sana ya kutatua matatizo ya kimwili zaidi ya yale ya kiroho? siyo kweli kwamba binadamu asiyekuwa na imani madhubutu anataka short cut au majibu ya papo kwa hapo kwa kila kitu kama kwenda kwa wapiga ramli? N ahiki kimekuwa chambo ay kivutio kikubwa cha kuwatoa watu kwenye imani zao na kujiunga huko - i the process michango, sadaka etc vinaongezeaka n akuneemesha baadhi ya watu?( NASEMA TENA SINA NIA YA KUKOSOA KWA UBAYA... nisamehewe kama nakosea tafadhalini!)
3. Mwisho wa siku nadhani tunatafuta kumwabudu MUNGU wa kweli... haijalishi kama nasali kwenye dhehebu langu