Mkuu umeanza uchambuzi wako vizuri na hata ukaonekana kufanikiwa kujenga hoja na kuoneka kuwa balanced lakini mwisho conclusion yako kama vile imekuumbua, imeweka wazi hoja yako kuwa yale mengine yote ilikuwa tu kuipaka qunini sukari. your conclusion does not logically follow from your analysis unless you ommitted something ..
MSIMAMO wa balance katika maelezo yangu ya mwanzo kabisa ni kweli kwamba nilikuwa nao, japokuwa ningependa katika kukujibu nitumie neno objectivity. Haya maneno mawili kadri ninavyoelewa mimi yanao uhusiano. Objectivity ndiyo huzaa balance. Kwa hiyo nadhani unajaribu kuhoji kama nilikuwa objective katika hoja.
Kwanza nikushukuru Mkuu Sungurampole kwa mchango wako kwenye uzi huu. Unatoa hisia kwamba majumuisho ya hoja yangu ya mwanzo wa uzi yanapishana na maudhui ya hoja inayojengwa tangu mwanzo. Lakini "conclusion" haijaondoka kwenye mada kama unavyoona wewe mkuu wangu.
Objectivity na balance ni nini? Objectivity na balance kadri ninavyoelewa mimi ni dhana ya kutoa haki ya kusikilizwa kwa mitizamo yote inayoweza kupishana katika hoja iliyopo. Hili nimelifanya katika mada. Mada ina masuala makuu mawili: Nimejadili suala la MANAGEMENT ya chama, na suala la UMAMLUKI wa Zitto Kabwe, nikasema huu ndo msingi wa mgogoro uliopo CHADEMA. Katika kujadili MANAGEMENT ya chama, nimejadili kwa kirefu kidogo suala ya matumizi ya fedha kwa sababu lilipewa uzito na kambi ya zito, lakini pia kutokana na fedha kuwa kitu nyeti sana katika management ya kitu chochote chenye wadau wengi. Najadili suala la Umamluki mwishoni kumalizia hoja.
Nilieleza, japo si kwa maneno haya ninayoyatumia hapa, kwamba Mgogoro uliopo CHADEMA una pande mbili. Kuna Upande wa Freeman Mbowe, na Upande wa Zitto Kabwe, na kwamba inaelekea wanachama wamejigawa katika makundi mawili ya ufuasi.
Katika kujadili management ya fedha nimesema naamini Mbowe na Zitto wamepishana kutokana na taaluma kugongana; kwamba ninavyouona mgogoro wenyenye ni kwamba mmoja wa hawa anataka matumizi ya fedha kutekeleza mipango cha CHAMA yafanywe kwa mbinu za kirasimu, wakati mwingine anatekeleza mipango ya chama kwa njia za mkato, ambazo nimeziita mtindo wa ma-entrepreneur kuharakakisha results. Katika Management unaweza kuchagua mbinu yoyote katika hizi. Opinion yangu ikawa kwamba hapa ni mpishano wa management style ambao umeleta mzozo, lakini pia kwamba binafsi sikuona tatizo katika management ya ki-entrepreneur kama malengo ya CHAMA yanatimia.
Nilimaliza kujadili mzozo wa management ya fedha kwa kusihi Kambi ya Mbowe ku-address issues ambazo kambi ya Zitto ina-raise. Hilo ni kutoa nafasi kwa pande zote kuthibitisha nia njema ama wizi. Huko ni kuwa objective.
Katika kujadili Umamluki wa Zitto nimeweka scenario ambayo ingeweza kuthibitisha Zitto ni Mamluki. Lakini nilitoa nafasi kwa hawa wanaodai kuwa Zitto ni mamluki kutupatia ushahidi wa kimazingira kuthibitisha kuwa Zitto ni Mamluki; hilo lilikuwa na maana kwamba wakishindwa kuonesha mambo yanayoelekeza kuwa Zitto ni Mamluki, basi tutajua kuwa Zitto si Mamluki. Maneno yangu haya yanatoa haki kwa pande zote mbili. Huko ni kuwa Objective.
Nilijadili masuala mawili: MANAGEMENT ya chama na UMAMLUKI wa Zitto Kabwe kutokana na haya mawili kuwa msingi wa mgogoro katika CHAMA kadri nilivyoelewa mimi. Hapakuwapo kuondoka kwenye hoja kutoka mwanzo hadi mwisho. Hoja yangu ililenga kutafuta suluhu ya mgogoro katika Chama pasipo upendeleo. Kuna pahala nilipendekeza Zitto na Mbowe wote wawili waondolewe kwenya nafasi zao ili kusudi tuweke watu wapya pasiwepo yeyote katika wanaogombana kuonekana kashinda, kwani kwa kubakiza mmoja hiyo ndiyo taswira ambayo ingejengeka. Ingawa sikufafanua malengo ya msimamo huo vizuri, malengo yalikuwa kukubali kuwa hawa wawili, kila mmoja kwa namna yake, wamekifanyia chama mema, na tunaweza kuendelea kutumia busara zao wakiwa nje ya uongozi.
Kuwafuta uongozi wote wawili kungeweza kufanywa kwa kuharakisha uchaguzi wenye nia ya makusudi kabisa kuondoa majina yote mawili katika orodha ya wagombea. Hii ingekuwa kama kuondoa jogoo mbili zinazodonyoana na kuparurana kucha kwene banda ziende kupigana nje ya banda, na sisi huku tuweke jogoo ingine kwenye banda uzalishaji uendelee.
Nadhani sasa utakubaliana nami kwamba nilikuwa objective tangu mwanzo, ingawa uhai wa CHAMA ulipewa nafasi fulani ya kipekee katika mimi kupendekeza kwamba jogoo zinazoparurana ziende nje. Hili la mwisho halikuzingatia ushahidi wa madai yenye kuleta mgogoro. Labda hapa niseme ushahidi katika madai yote mawili ukijitosheleza ni kweli kwamba jogoo moja ikibaki katika banda hapata kuwa na shida. Nilikuwa balanced Mkuu.
Hiyo unaipokeaje?