Pengine, linaweza kutimia kwa njia hii. B+

Pengine, linaweza kutimia kwa njia hii. B+

Nevilly

Senior Member
Joined
Jul 9, 2014
Posts
168
Reaction score
312
Wadau,

Mwaka jana nilikuwa nilikuwa nko katika msongo wa mawazo ambao ulinipelekea kujiona kama vile Nimechelewa na looser fulan kwa sababu nlikuwa naona umri (30) wangu na kiwango cha mafanikio niliyonayo haviendani kabisaa na sina kipato cha uhakika na kinachoeleweka, nkaona isiwe tabu ngoja ntengeneze post nisikie wanajamii wanasemaje juu ya huu mtazamo wangu nilio ubeba kichwani,nikaandika post ambayo iko na title hii kucheclewa kwang kunantisha
Kuchelewa kwangu kunanitisha sana

Ushauri niliopata kutoka kwenye comments ulikuwa ni mzuri sana, ukanipelekea nijikute nko kwenye mpango wa kutengeneza mradi (project) ambazo ntaweza kusimama nazo siku za mbeleni, maana hadi sasa nuru ya ajila/ kuajiriwa imepotea kabisa usoni hata akilini mwangu.. yaa niko na 31 mwaka huu na sijawahi ajiliwa Tuachane na huko

Sasa Kwa mwaka mzima nmejisumbua kujifunza maswala ya kutengeneza app hususani aina ya social media kama instagram ,tiktok , na nkaamua kutumia ujuzi niliojfunza kutengeneza app ya maswala ya uwakala wa harusi (wedding Agency & wedding Planning), kwa lengo la ikifika mwaka 2023 iwe ndio project ntakayo anza nayo mwaka na ntakayo simama nayo, na kuwa na hii vision atlist ndani ya mwaka huo 2023 niwe nmefanikiwa kufanya sherehe zisizo pungua tatu.. najua inawezekana .. Aimen!

Nia nilio tia mwaka 2022 huu ni kwamba nikimaliza kutengeneza tu hii app version ya kwanza .. ded or alive lazima niaupload hiyo app playStore ..

Sasa kinachotokea nmemaliza kutengeneza mwaka huu mwezi wa kumi na mmoja mwishoni lakini kila nikfurukuta npate kiasi cha kama shilingi 308,327 za kitanzania kwa ajili ya kuapload app playstore na kupata kununua server (database), naona mishe zinagonga mwamba pesa hiyo sipati na siku zinayoyoma vibaya mno

Sasa nkaona isiwe tabu.. inawezekana aibu yangu ikawa ndo umaskini wang,,, nmeona nilioandishe hewani tu pengine naweza nikapata connection ya watu ambao wanamatamanio ya kufanya project kama hizi na kuunganisha nao energy katika hili na kufanya jambo hili lisonge

kwa wanaohitaji kujua labda kamchanganuo wake kupata Google Play Store account gharama yake $25 ambayo ni sawa na 58,327.97 tzs, na gharama za kuweka data za app katika server Bluhost Serve ni $107.16 / year ambayo ni sawa na 250,000 tzs na hiyo ni Basic Plan yenye 2 extra packages activated, ambapo ukijumlisha apo inakuja kama kiasi $132.16 ambayo ni sawa 308,327 Tsh inategemea na siku iyo currency imekaaje

Yangu ni hayo Tu.

Contact: 0743 88 24 55;

Asanteni, Na karibuni kwa mawazo
 
Sasa hela ya playstore tu inakutoa jasho, kuipromote utaweza kweli?
 
Mungu atakufungulia milango na kila kitu kitaenda sawa mzee
 
Uko vizuri, ukipata mtu wa kukusimamia na kukuongoza utafika mbali sana. Changamoto; baadhi ya vijana si waaminifu hasa pale pesa itakapoanza kuonekana.
Wataanza kulalamika baada ya kuona mafanikio, ananinyonya huyu n.k​
 
Uko vizuri, ukipata mtu wa kukusimamia na kukuongoza utafika mbali sana. Changamoto; baadhi ya vijana si waaminifu hasa pale pesa itakapoanza kuonekana.
Wataanza kulalamika baada ya kuona mafanikio, ananinyonya huyu n.k​
Hiyo inatokea kama makubaliano ya awali yanakuwa hajakaa vzuri.... kama kila mtu akiwa muwazi na wanasheria wamechukua nafasi yao vzuri akialibiki kitu
 
Back
Top Bottom