magode
JF-Expert Member
- Oct 2, 2014
- 2,204
- 3,337
Wanabodi,
Salaam;
Tangu awaamu hii ya 5 iingie madarakani,imekuwa ikiibua ufisadi mkubwa kila mahali. Ukimsikiliza Rais ktk hotuba zake anavyosikitika utadhani nchi haikuwa na uongozi kabisa huko nyuma.
Kwa hali jinsi ilivyo ktk nchi yetu,ili kujenga nidhamu ya kweli ya kuzuia ubadhirifu wa mali za umma,napendekeza adhabu ya kifo kwa mafisadi na wala rushwa. Kwa bahati nzuri sheria ya kunyonga watu bado tunayo ni kitendo tu cha serikali kupeleka muswada bungeni kuongeza idadi ya wanaotakiwa kunyongwa.
Lengo hapa siyo kuua watu,lengo ni kuweka adhabu kali ili watu wasiibe mali ya umma au kupoka haki za wengine kwa kupokea rushwa. Wale wa haki za binadamu tafadhali mkae kimya ktk hili nchi imeharibika sana hii..!
Kule korea kaskazini hivi karibuni wamemnyonga mkuu wa majeshi kuonyesha hakuna aliye juu ya sheria. Bila kuwanyonga hawa watu watazidi kunyonya nchi.
Nawasilisha!!