Pendekezo, Machinga na dodoso la sensa 2022

MUSIGAJI

JF-Expert Member
Dec 26, 2014
2,187
2,461
Wakuu nawasalimu.

Ninapendekezo, ili tuweze kujua uhalisia wa idadi ya wananchi wanaojishughulisha na biashara zisizo rasmi,Ninashauri madodoso ya sensa mwaka 2022 Tufanye marekebisho kidogo.

Katika sehemu ya kazi tubadilishe madodoso tusiishie kuweka option ya MWAJIRIWA au MFANYABIASHARA au MKULIMA.

Katika kipengele cha MFANYABIASHARA ninashauri hapa waingie wale tu wenye TIN na leseni za biashara na mtu akisema ni MFANYABIASHARA iwepo sehemu ya kuandika TIN namba.

Nashauri kipengele cha MFANYABIASHARA HISIYO RASMI kiongezwe, na hapo ifafanuliwe ni ipi.

Mtu atakaye andikishwa Kama MKULIMA awe ni yule tu ambaye kilimo ndicho chanzo kikuu cha mapato yake.

Hii itatusaidia mambo mengi, mfano kujua tatizo la ajira tulilonalo, Ni Watanzania wangapi wanategemea umachinga kuishi, nk.

Ninachokiona katika zoezi la kuvunjiwa machinga vibanda bila takwimu ya Watanzania wangapi wataathirika tunatengeneza matatizo yafuatayo kwa muda mfupi ujao.

Kuongezeka kwa vitendo vya wizi na ujambazi, Vibaka kuongezeka, Ongezeko kubwa la watoto wa mitaani,Ongezeko kubwa la kina mama na watoto waliotelekezwa, Ongezeko la ombaomba na mengine mengi.
 
Back
Top Bottom