Kwa kuwa umri wangu ni mkubwa kidogo nianze kwa kueleza hali ya umiliki wa ardhi hapa nchini ilikuwaje enzi wa Nyerere. Enzi hizo kwa mujibu wa sheria ardhi ilikuwa haina thamani. Serikali ilipokuwa ikitwaa ardhi kwa ajili ya maendeleo mbali mbali kama mvile kupima viwanja n.k ilikuwa ikilipa fidia ya maendelezo ya ardhi tu yaani nyumba na mazao yaliyopandwa na aliyekuwa akiitumia ardhi husika. Hakuna fidia yeyote iliyokuwa ikitolewa kwa ajili ya ardhi.
Hivyo watanzania hawakuwa na tamaa ya kushika na kujilimbikizia ardhi kwa matarajio ya thamani ya ardhi kuongezeka. Wakati huo kila mtu alichukua ardhi anayoweza kuihudumia tu kwa kuwa ni gharama kuhudumia ardhi, tena ikiwa ni kubwa ndio gharama zinvyoongezeka maradufu. Na kuacha ardhi ingine kwa matumizi ya watanzania wengine. Wakati huo Serikali iliweza kupima viwanja na kuviuza kwa bei ndogo ambavyo kada mbali mbali za watanzania ziliweza kuvinunua kama vile waalimu, manesi n.k kwa sababu haikuwa imelazimika kulipa fidia ya ardhi kwa walioshika ardhi husika.
Wakati niliweza kushuhudia watu wakinunua mashamba na kuyaacha kwa kitambo na wakirejea na kukuta yameuzwa upya kwa watu wengine wakipuuza vitendo hivyo baada ya kupiga hesabu za kufyeka na kutunza shamba husika kwa muda wote huo. Hawakuwa wakienda kushtaki kwenye mabaraza, mahakamani n.k kwa kifupi migogoro ya ardhi ilikuwa ni michache sana.
Baada ya kufutwa kwa Azimio la Arusha enzi za utawala wa Ruksa ndipo Sheria mpya ya Ardhi Na 4 na n5 za 1999 zikazpitishwa na bunge zikitamka ardhi ina thamani. Tukashuhudia viongozi waliohusika kupitisha sheria hiyo wakitimua mbio kuelekea vijijini ambako wananchi hawakuwa wamepatiwa elimu kuhusu sheria hizo mpya na kukamata na kujilimbikizia mamia kwa mamia ya ekari za ardhi kwa matarajio ya ongezeko la thamani. Tukashuhudia Serikali na halamshauri zikitaka kupima viwanja kwanza ni lazima ziwalipe fidia ya ardhi na maendelezo wamiliki wa ardhi hata kama ni mapori.
Matokeo yake watanzania wachache hususan viongozi waliotambua kuwa Sheria za Ardhi za 1999 zimeanzisha utaratibu wa "Land Speculation" wakajitwalia ardhi kubwa kuzidi uwezo wao wa kuihudumia. Kwa mara ya kwanza kama ilivyokuwa enzi za "Cowboys" tukaanza kushuhudia upandandaji wa nguzo kutambulisha kuwa hii ni ardhi ya fulani. Hivi sasa watu wachache wanamiliki ardhi kubwa kubwa huku idadi kubwa ya watanzania hususan vijana wakikosa ardhi ya kujenga, kulima n.k. Bei za viwanja zimekuwa kubwa mno kiasi kwamba wanyonge wanashindwa kupata viwanja vya kujenga na kulazimika kujenga sehemu hatarishi. Serikalki yenyewe ikipima viwanja inalazimika kuviuza kwa bei ya juu mno kuaniza Milioni 7 kwa mita 20X20 kwa ililazimika kulipa fidia ya ardhi kwa bei ya soko.
Ili kupunguza migogoro ya ardhi hapa nchini hii Sheria za Ardhi za 1999 zinazotamka ardhi ina "thamani" zitazamwe upya ili kurejesha utaratibu wa zamani ambapo fidia italipwa kwa maendelezo yaliyofanyika juu ya ardhi tu na sio kwa ardhi husika . Hatua hii itawarejesha watanzania kuchukua ardhi wanayoweza kuihudumia na kuacha ardhi ingine kwa matumizi ya watanzania wengine.