Baada ya timu zetu (klab) pendwa kuondolewa "bila zengwe" katika mashindano ya kimataifa yanayoandaliwa na CAF, nimejifunza mambo kadhaa;
1. Ni kweli kabisa kwamba mpira wetu ni kivyetuvyetu kama wasemavyo azam tv.
Ukiangalia namna tulivyoyaendea mashindano kwa msimu huu, utagundua kuwa hata hatukujua tunaenda kufanya nini zaidi ya mazoea.
Simba wakaingia wakijua wao ni favorite wa kundi huku uhakika wa kufuzu kutokana na historia yao katika michuano ya "CAFCL" (badala ya kufanya professional footbal analysis) ukiwapumbaza, hata wa kuwakumbusha kuwa njia hiyo iliwagharimu wydad misimu mitatu iliyopita hawakumpata, maana hata viongozi wao nao hawakulikumbuka hilo, mwishowe wameweka historia mpya kwa mara ya kwanza, wameishia makundi .
2. Mpira wetu ni chotara wa professionalism na uswahili wa kipwanipwani. Jangwani walitishwa kuwa wamepangwa kundi la kifo, wakatishika, wakakaa kitako na kuweka mikakati (walijitahidi kuwa professional), raundi ya kwanza mkakati ukawalipa. Mkakati ulipowalipa raundi ya pili wakajisahahu wakaanza uswahili (walisikika wakisema, tuliambiwa tumepangwa kundi la kifo kumbe sisi ndio wauaji wenyewe), kuna viongozi wakaanza kutamba eti hata wangepangwa na man city, barca, arsenal na madrid bado wangefuzu (pure uswahili na ujinga juu). Cha ajabu akaja tai wa farao akawatonya kwamba msijisahau lakini hawakuzinduka, wakasare na ahly, wamekuja kukumbuka kwamba walipaswa wamkomalie tai wa farao wampige gori la pili katika kipindi ambacho tayari wameshashinda tatu bila kwa kabylie, na ni tatu bila kweli kweli maana wameshinda goli tatu bila kufuzu, wameishia makundi.
3. Timu zetu hazichezi mechi zao tu bali zinacheza pia mechi za majirani.
Unaanza na mchezo wa usajili, huyu akisajili kante yule anasajili konte, hapo kigezo sio quality bali a na o. Huyu akisajili Joyce yule anasajili Deborah, hapo kigezo sio quality bali aina ya jina, akili za wapi hizi?
Imekuwa ni kawaida sana wana5imba kuiombea mabaya jangwani, hii hufanya watumie muda mwingi kuihujumu jangwani badala ya kujenga kikosi chao, utaratibu huu hauko m5imbazi pekee, ndio jadi ya sokoni kariakoo.
Wakati 5imba anapambania roho yake ili apate point mbele ya esperance, yanga wanashangilia esperance ampige Simba badala ya kupambana na ahly wao. Matokeo yake 5
Simba akasare na Esperance, jangwani akasare na ahly. Hizi ndizo mechi zilizozika ndoto za hawa mabwana mapacha, wameishia makundi.
4. Timu zetu zinajipambanua katika ubora mithili ya firigisi nyama nje ngozi ndani.
Ukireplay 5imba day na jangwani day za msimu huo utakutana na mapro watupu kuanzia benchi la ufundi hadi wachezaji. Ni mapro kweli kweli maana utasikia wamesajiliwa kutoka nchi za ulaya sijui norway sijui wapi huko (maana sijawahi kufika). Hapo hapo utaisikia mipango kabambe ya kitaalamu kutoka kwa viongozi wao mithili ya
Florentino Perez na bernabue yake, makundi yalipoanza tu upande mmoja wakasema hawazitaki mbichi hizi raundi ya pili tu huku upande mwingine wakimaliza calculator pale mjini kariakoo.
Kumbe walisajili quality players wa ligi pendwa badala ya quality players wa ligi ya mabingwa, matokeo yake; wameishia makundi
MAPENDEKEZO YANGU
1. Mpira ni mchezo wa wazi, hakuna uchawi wala ujuaji wa kisela bali ujuaji wa mpira. Na uzuri mpira ni kama baiskeli tu, anayeujua anaujua tu. Wekeza pesa ya maana kamq unayo, sajili vyuma vya kazi, huwezi kupambana na trezget kwa kumtumia bokkar wala hutaweza kumzuia Youcef Belail kwa kumtumia kibawabage.
2. Kwakuwa tunataka kuwa wakubwa afrika, ni vena tuachane na soka la kivyetuvyetu, tuingie kwenye soka la kitaalamu, tusihangaike na mechi za majirani tuangalie mechi zetu tu kitaalamu na sio kijanjajanja. Pale kwa farao kuna vita kubwa sana ya wakubwa wawili lakin hawa jamaa linapokuja suala la uendeshaji wa timu zao hawasajili mtu eti kisa jirani kasajili, wanasajili kwa sababu wanauhitaji wa nafasi husika kwa mtu sahihi.
Tusipobadilika mapema, tutaendelea kuthibitisha kwamba linapokuja soka la kimataifa, kulipata kombe la "mwakarobo" sio kazi nyepesi, na mwaka huu huo wimbo hautaimbwa nchi hii maana wanakwaya wameshauona ugumu wa shoo kuipata hiyo mwakarobo.
Msisahau kuwasalimia kurwa na Dotto, nawakaribisha kwenye soka letu, kivyetuvyetu.